Marekebisho kidogo Mkuu, Hiyo picha ni ya March 1993, ilipigwa na Kevin Carter. Na hiyo shot aliipata kama bahati tu, wakati akifanya adjustment ya lens ili ampige picha huyo mtoto Vulture ndy akatua nyuma ya huyo mtoto. Carter alisubiri hapo dk 20 (Na siyo masaa4, kwani walikuwa na dk30 tu kabla kuondoka ndege iliyowapeleka) kuona kama Vulture ataondoka, lakini hakuondoka, ndipo alipoamua kumfukuza. Habari zaidi zinasema kuwa mtoto huyo ni mmoja kati ya watoto wengi walioachwa na mama zao walioenda kufuatilia chakula kutoka ndege za UN zilzokuwa zikitoa chakulla, mpaka leo haijulikani kama kabinti hako kalikufa au kalipona! Ukifuatilia historia ya maisha ya Carter utaona kuwa alizaliwa na kukulia katika maisha yaliyozungukwa na Ubaguzi na Mauwaji ya kutisha, juhudi zake za kukimbia maisha hayo ndy zilizomtoa jeshini na kumpeleka kwenye u-cameraman ambako alikutana na mambo mazito zaidi yaliyomsononesha na kumfadhaisha mpaka akafikia uamuzi wa kujiuwa kwa kuchomeka mpira wa maji kwenye exost ya gari yake na upande wa pili akauchomeka dirishani huku yeye akiwa ndani, hivyo sumu ya carbonmonoxide kumuua kwa utulivu kabisaa, aliacha ujumbe huu:
"I am depressed ... without phone ... money for rent ... money for child support ... money for debts ... money!!! ... I am haunted by the vivid memories of killings and corpses and anger and pain ... of starving or wounded children, of trigger-happy madmen, often police, of killer executioners ... I have gone to join Ken [recently deceased colleague Ken Oosterbroek] if I am that lucky."