Kevin Carter, Mwanahabari aliyejiua baada ya kupiga picha watoto waliokuwa wakifa kwa njaa sudan

Duh hatari sana juzi tu nliona tangazo la kuwasponser watoto wa africa ambao most of them wapo katika hali duni na afya zako zilivo mbaya kupita maelezo nlitokwa na machozi nkajiuliza africa yangu ndo ilivo hivi inasikitisha sana....
 
Huyo jamaa nasikia baada ya habari zake kusambaa alidata kama aina ya uchizi kwa msongo wa mawazo na kama baada ya miezi kadhaa alifariki,ilitangazwa pia taarifa yake kwa vyombo vya habari kipindi hicho,nadhani alijiona ameplay part kusababisha kifo cha mtoto huyo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kuna yule mzungu mwingine aliyepiga picha ya mtoto wa kiafrica akiwa amesokotwa mguu na chatu.....mwenye details zake plz
 
Mtoto yupo kwenye wakati mgumu sana, Inaumiza mno, Mungu Mwingi wa Rehema aturehemu tu!!!!
 
picha yake hiyo ilishinda tuzo ya picha ya mwaka,halafu akaulizwa ulimsaidiaje mtoto yule?akakosa maneno,nafsi ikamuuma,akakataa kuchukuwa zawadi alizotakiwa kupewa,baadae alikutwa amejinyonga

Unaweza kuona mtu anaetambua makosa yake nakujutia! Ingekuwa huku kwetu! Wala acngejali sanasana! Angenunua hata Airtym kwenye TV na Radio kujifagilia,,,!
 
The irony is, kwa kupiga picha hiyo, hata kama hajamuokoa huyo, kasaidia kuokoa mamilioni wengine kwa awareness.
 
Dunia nzima ilizizima kwa machozi picha inaonesha mtoto akiwa amelala chini huku kunguru akiwa anaelekea kudonoa mwili wa mtoto jamaa badala ya kuweka kamera chini kumwokoa mtoto yeye aliendelea na kazi yake ndipo dunia ilipohoji mpaka kupelekea kifo

si kwamba alijiua baada ya issue ya hiyo picha. Sababu aliyotoa ya kujiua ni hii hapa chini

KEVIN CARTER
Death

On 27 July 1994 Carter drove his way to the Braamfonte near the Field and Study Centre, an area where he used to play as a child, and took his own life by taping one end of a hose to his pickup truck’s exhaust pipe and running the other end to the driver's side window. He died of carbon monoxide poisoning, aged 33. Portions of Carter's suicide note read:

"I am depressed ... without phone ... money for rent ... money for child support ... money for debts ... money!!! ... I am haunted by the vivid memories of killings and corpses and anger and pain ... of starving or wounded children, of trigger-happy madmen, often police, of killer executioners ... I have gone to join Ken if I am that lucky."
 
Dunia nzima ilizizima kwa machozi picha inaonesha mtoto akiwa amelala chini huku kunguru akiwa anaelekea kudonoa mwili wa mtoto jamaa badala ya kuweka kamera chini kumwokoa mtoto yeye aliendelea na kazi yake ndipo dunia ilipohoji mpaka kupelekea kifo

sio kunguru,ni tai
 
Dunia nzima ilizizima kwa machozi picha inaonesha mtoto akiwa amelala chini huku kunguru akiwa anaelekea kudonoa mwili wa mtoto jamaa badala ya kuweka kamera chini kumwokoa mtoto yeye aliendelea na kazi yake ndipo dunia ilipohoji mpaka kupelekea kifo

Hii picha ya mtoto nilikuwa naiona sikujua ina maana gani!!!shukrani kwa ufafanuzi.
 
daaa

may his soul RIP, kwa picha hii na nyingine atakuwa ameokoa watoto wengi na jamii kwa ujumla.
 
Mpiga picha mwanahabari aitwaye Kevin Carter toka Afrika Kusini alienda Sudan mwaka 1993 na kupiga picha ifuatayo ya msichana mdogo mwenye utapiamlo na njaa kali akiwa ameelemewa njiani kuelekea kituo cha kugawa chakula na nyuma yake tai mkubwa akimnyemelea amle(mwaka huo kulikuwa na njaa kali sudan.)

Picha hii ya Kevin ilimpa tuzo ya Pulltzer na kuchapishwa kwenye gazeti la New York Times.

Baada ya picha hii kuchapishwa maswali mengi yaliulizwa juu ya mustakabali wa huyo msichana. Wengi walitaka kujua kama huyo msichana alikuwa bado hai. Na wengi walimiminika kutoa msaada kwa waathirika wa njaa huko sudan. Pia walitokea watu waliomshutumu sana Kevin na kumfananisha na huyo tai, kwamba Kevin alitaka huyo msichana afe kwa sababu badala ya kumsaidia yeye aliona raha kupiga picha.

Lakini watu hawa hawakufahamu ukweli kwamba baada ya kupiga picha Kevin alimfukuza huyo ndege na Kevin alijua kuwa mama wa huyo mtoto alikuwa karibu kwenye kituo cha msaada akipokea msaada wa chakula. Hata hivyo shutuma na lawama vilizidi kumwandama Kevin.

Hatimaye siku moja mwaka 1994 Kevin akiwa kwao Afrika ya Kusini aliendesha gari yake mpaka sehemu tulivu isiyokuwa na watu wengi. Akachukua bomba la mpira na kuliunganisha na bomba la moshi wa gari (exhaust pipe) na kuweka bomba hilo la mpira kwenye chumba che dereva kisha akawasha gari. Moshi wote ukajaa sehemu ya dereva.Moshi una sumu kali iitwayo carbon monoxide na ikiingia kwenye mapafu kifo hutokea. Maandishi aliyoyaacha kabla ya kujiua yalisomeka hivi, "Nafsi yangu imechoka na kufadhaika sana kwa mateso ya binadamu niliyoyaona huko Sudan. Nashindwa kuishi kwenye hali ya namna hiyo"






 
Kuna sehemu niliisoma hii habari, hakukua na maelezo yakua Kevin alimsaidia huyo mtoto baada ya kupiga picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…