Inawezekana unaijua tafsiri yake.Sasa hapo wahaya wa nini wakati hiyo verse imeimbwa kwa kiswahili?
Wahaya wanahusika vipi hapo wakati lugha iliyotumika kwenye msingi wa swali lako ni kiswahili?Wakuu habari zenu,
Katika wimbo wa Saida Karoli unaoitwa Maria Salome' kuna mashairi yanasema
'Khalidi na Filimoni walipendana,mapenzi yao yakadumu,
Wenye wivu wajinyonge sana,wenye wivu wajinyonge'
Sasa Khalidi na Filimoni walipendana mapenzi ya namna gani hayo yakadumu?
Hao wote si ni wanaume au kuna mmoja ni mwanamke hapo maana nimejaribu kutafuta mashairi sikupata.
Labda wenzetu mtusaide kwakua mnaelewa maneno mwanzo mwisho inawezekana stori mmeielewa au pengine katika tamaduni zenu kuna majina ya kike yanafanana na hayo?
Karibuni mtujuze
Wakuu habari zenu,

Urafiki wa kuchanjana damu unaobadilika kuwa undugu ndiyo anaoongelea. Mhaya akifanya urafiki unageuka undugu.Imeimbwa kiswahili ndio, lakini kuna maneno kabla ya hio verse na hata baada pameimbwa kwa kihaya kwahio kuna uwezekano zikawa zinahusiana
Mimi ninavyoelewa ni jinsia moja. Siwezi semea kila mtu maana mimi babu yangu alichanja damu na watu wa jinsia zake ambao sasa ndugu zao ni ndugu zetu ambao tunawaheshimu zaidi kuliko wetu sababu mkifarakana wanasema kuna laana. I cant prove it. Sijawahi sikia wanawake wanachanja damu na sijui kwanini. Labda kuna watu humu JF wanajua zaidi.Kwahio kwa wahaya huu utaratibu ni kawaida mwnamke na mwanaume kuchanjana damu au mwanaume na mwanaume?
Mimi ninavyoelewa ni jinsia moja. Siwezi semea kila mtu maana mimi babu yangu alichanja damu na watu wa jinsia zake ambao sasa ndugu zao ni ndugu zetu ambao tunawaheshimu zaidi kuliko wetu sababu mkifarakana wanasema kuna laana. I cant prove it. Sijawahi sikia wanawake wanachanja damu na sijui kwanini. Labda kuna watu humu JF wanajua zaidi.