Kiafya masikini wana muda wa kupumzisha akili kuliko matajiri!

Kiplayer

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
1,180
Reaction score
1,964
Tajiri sehemu kubwa ya maisha yake anawaza kutafuta na kulinda alichonacho.

Masikini hana cha kulinda anawaza kutafuta chakula na kulala.

Ukiachana na nature masikini yu salama sana wakati tajiri usalama wake umejaa mashaka, ndio maana ulinzi ni wa kutosha.
 
Maisha ya wenyeji wa pwani yaani hawanaga complications ukilinganisha na wageni wale wa kwenda kuhiji Christmas big up watani zanguu
 
Sio kwa dunia ya leo ambayo pesa ndio silaha, kila unachogusa ni pesa, hapa lazima maskini aumie
 
Masikini mna tabu sana
 
Tajiri asiyeridhika na alichonacho ndio hupata tabu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utajiri ni nini ?

Kuna hierarchy of Needs mtu akishapata Basic Needs.., Chakula, Malazi na Mavazi kinachofuata ni Safety Needs, Love and Belonging, esteem alafu mwisho ni self actualization (yaani the best you can be/ you want to be) huenda Diamond pale alipo amefikia hilo sababu katika anachopenda (kuimba) ameweza kuimba na watu kukubali kazi yake...; Huwezi ukawa Fukara hauna hata chakula mavazi wala malazi alafu useme una muda wa kupumzisha akili

Ila sasa kuna chasing an illusion (tamaa na kutokuridhika) unakimbiza ambacho hakipo au mashindano ya kushindana na watu ambao hata hawajui kama unashindana nao (na huo ni utumwa wa maisha) na kama mtu yupo hivyo maisha yake yote roho yake itakuwa haijatulia..., Kwahio utakuta watu waliogundua hilo fumbo la maisha wana furaha with less materialistic things.... Kwahio wewe unaweza kuona mtoto kifua wazi yupo mtoni anavua samaki na ndoano ili amchome kwenye vijiti vyake vya kuni kwamba ni masikini ila kumbe ni tajiri amekidhi needs zake zote sustainably
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…