Kiasi chake Lema yuko sahihi, niliishi USA miaka kumi niliporudi nchini niliamini Watanzania tuna laana

Nimesoma HGL nilisoma sehemu kuwa karne ya 15 Africa na Europe zilikuwa almost the same,niko tayari kukosolewa

Wenzetu walikuja kutuzidia kwenye izi revolution...

Britain Revolution

French Revolution

German Revolution

USSR Revolution

Greece revolution

Kuleta zile agriculture revolution
Industrial revolution

Kuondoa mambo ya kina king Luis
 
kwanza unatakiwa ujue Christopher Columbus sio aliyevumbua bara la marekani,kwa mujibu wa Christopher Columbus anasema alipofika America aliambiwa kwamba kuna watu wageni walifika kabla yake hapo America na akasema alikubaliana na madai hayo baada ya kuona kuna aina za handkerchief walizokuwa wanatumia wahindi wekundu ni kama zile zilizokuwa zinatumiwa kwenye dola ya Timbuktu..

Again akadai tena kwamba kuna baadhi ya spears( mishale) iliyokuwa gold plated ambapo baadae baada ya kufanya uchunguzi ikagundulika ile dhahabu inatoka Africa Magharibi...

Twende taratibu kwanini dhahabu itoke Africa magharibi?!.Mfalme Abubakari wa pili ambaye ni kaka yake na Mansa Musa siku zote alikuwa na wish ya kutaka kujua mwisho wa Bahari ya Atlantic ni upi? Akakusanya crew ya mainjinia kutoka Lake Chad na kuwaambia watengeneze mashua strong sana zinazoweza kufika deep sea kabisa Atlantic..baada ya hizo process kukamilika akaandaa fleet iliyokusanya meli zaidi ya 200 iliyohusisha sailors, traders, engineers,builders, creative artists, brave warriors, na intellectuals. Na akawaambia muende huko mtagute mwisho wa hii bahari msirudi mpk muone chakula kimewaishia au kuna sababu ya lazima itakayowafanya mrudi..

Siku zikaenda miaka miwili ikapita ghafla wanaona kwa mbali kuna mashua moja inarudi kati ya zile mia mbili,mfalme Abubakar akauliza nini kimewakumba huko!? Wakamjibu bhana tumefika mbali kabisa ghafla tukakutana na mkondo mkali sana wa bahari kila aliyejaribu kupita hapo akazama sisi tulikuwa wa mwisho tulipoona hakuna uwezekano wa kurudi hapo tukaamua tugeuze turudi huku Mali..

Hii haikumfanya mfalme akate tamaa badala yake akaoda fleet yenye meli zaidi ya 1000 waambatane nae waende huko basi siku ya siku safari ikaanza kuelekea Mashariki mwa Atlantic Ocean..ingawa haijathibitika wazi kwamba safari yao iliwafikisha Marekani au vipi lakini kuna ushahidi wa wazi ambao unaonyesha Christopher Columbus sio wa kwanza kufika Marekani kama unavyoniambia hapa maana hata yeye kwenye maandiko yake alisema nanukuu "Black-skinned people had come from the south-east in boats, trading in gold-tipped spears The natives described the spearheads as “guanin”, a word for “gold” in the Mandinkan, the language of the Mali Empire"(Tafuta journal yake kama hakusema hivi mm najitoa Jf,hii iliwafanya mpaka westerners waedit machapisho na kusema kwamba Christopher Columbus hakuwa mgeni wa kwanza kuvumbua America bali ni mtu wa kwanza kutoka Ulaya kugundua bara la America..

Story hiyo ya mfalme Abubakari alisimulia Mansa mussa alipofika Misri kuelekea safar yake ya hijja ndipo akamua apumzike misri kwanzana mwenyeji wake akamuuliza ufalme wako uliupataje? Ndio akahadithia hayo kumbuka hayo yalitokea miaka zaid ya mia mbili kabla ya Christopher Columbus hajafika Hapo Marekani..

Christopher amefika hapo amekuta jamii ya hapo imeendelea waAztec walikuwa wamefanya mapinduzi makubwa kabisa ya teknolojia ya chuma na walikuwa wanalima mashamba makubwa sana ya mahindi hawakuwa primitive kama unavyotaka kuaminisha hapa kwamba waingerrza walipoingia hapo America walikuta jamii iliyolala haijushugulishi kabisa..maendeleo yalikuwepo makubwa sana tangu enzi hizo lakini walipokuja wageni ndio yakazidi maradufu zaidi
 
Safii,hiyo stori ya mfalme abubakar niliisoma mtandaoni kitambo,mpaka leo haijulikani hiyo fleet iliishia wapi,nilipenda ujasiri wake wa kutaka kuexplore dunia,
 
Wenzetu walikuja kutuzidia kwenye izi revolution...

Britain Revolution

French Revolution

German Revolution

USSR Revolution

Greece revolution

Kuleta zile agriculture revolution
Industrial revolution

Kuondoa mambo ya kina king Luis
So u mean tunahitaji revolution ipi sasa,agrarian,industrial au political revolution?
 
Hatutaki masimango atuache na umaskini wetu vinginevyo aje na njia ya kututoa katika umaskini otherwise ni mashauzi tu ya kisiasa. Lem anakaa wapi huko Arusha, tuanzie hapo
 
Ulipovunjika mguu USA ukarudi Tanzania ukagundua tuna laana? Sisi ndo tulikuvunja mguu? 🤷🏽‍♀️

Kuna watu tangu nchi inapata uhuru yeye anailaumu serikali, kila rais akija yeye analaumu, muulize una hobby gani anakwambia kucheza bao/draft.

Anapandikiza chuki ya kuilaumu serikali kwa vizazi vyake vyote. Hiyo ndo laana. Jitumeni
 
Soma vizuri uelewe,nulivunjika mguu nikiwa USA
 
 
Kinachokukalisha TZ ni Nini wakati unajua ni taifa la watu waliolaaniwa.
.
Mbona usirudi huko USA kwenye maisha mazuri na raha
Huwezi kunipangia pa kuishi.
Hapa tutaishi tu hata kama kuna laana
 
Mbona hutulinganishi ni inchi za Asia ambazo tulizizidi kiuchumi, leo hii ziko mbali zaidi yetu,Tatizo la viongozi wa Afrika Uwizi wa mali za uma, kupeana madaraka kindugu, kutokuachia madaraka kwa demokrasi, wizi wa kura mfano CCM, kutosimamia rasilimali zake ipasavyo, kugeuza misada kama mitaji binafsi na mengineyo mengi
 
Ukitoa mfano wa marekani toa mfano na nchi km singapore, malaysia na Indonesia ambao wakati tunapata uhuru tulikuwa nao sawa kiuchumi.
 
Madhira ninayopata Tanzania toka nirudi kutoka masomoni na kuanza kuishi rasmi nchini kwangu uwa naishia kumkumbuka baba yangu na huu uzee wangu ila laiti baba angelikuwa hai nisingeishi kwenye hili jangwa .

Allah aendelee kumrehemu tu mzee wangu .

Tanzania bado sana ni ujinga mtupu.
 
Asa kwa nn ulikubali kurudi mkuu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…