G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Kibaha. Diwani mteule wa CCM kata ya Kikongo Kibaha vijijini Fatuma Ngozi pamoja na wajukuu zake wawili wamefariki baada ya kuungua kwa moto wakiwa ndani ya nyumba.
Nyumba ya diwani huyo imeungua moto usiku wa kuamkia leo Novemba 9, 2020.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
"Nipo kwenye kikao, najua unaulizia tukio la moto huko Kikongo ni kweli na watu wangu wapo eneo la tukio toka alfajiri wakifatilia chanzo, nitazungumza baadaye mchana kikao kitakuwa kimeisha," amesema.
Chanzo: Mwananchi