KIBAHA: Wakili Riziki Majallah auwawa na mwanaye wa kumzaa kisa kumnyima pesa

KIBAHA: Wakili Riziki Majallah auwawa na mwanaye wa kumzaa kisa kumnyima pesa

Hii nimeitoa Facebook naona jamaa nyumba ilishamshinda maana dogo alikuwa amezidisha hatari lakini yeye hakuona umuhimu wa kumuwahi,halafu jamaa alikuwa amepewa kitengo Dodoma ndiyo alikuwa anajiandaa kwenda ku-report
 
Ni mambo TU ya kuigana,maraisi wetu wote Hawakusoma hizo English medium,kuna rafiki yangu mmoja kiatu alivaa kuingia form one!,Hata kwenda shule ilipo alikuwa hajawifika,Hivi Sasa ni bonge la boss kwenye taasisi nyeti!Hajajisahu ! Watoto wake pia wamesoma kayumba na ni vichwa hasa,mmoja ni injinia makini sana.
Safi sana
 
Poleni sana mawakili na wanasheria.

Anyways wazazi msisahau kuna tofauti kubwa sana kati ya kulea mtoto na kumtunza mtoto.

Hakuna kitu kibaya kama kumlea mtoto kwa kumdekeza kwa kumpa kila kitu.

Wafundisheni watoto wenu kuhusu maadili mema na namna ya kuishi.

Ndio maana kila siku nawaambia wazazi mnao somesha. Hakuna haja ya kujistress kulipa mamilioni kusomesha watoto shule za English Mediums.

Somesheni watoto wenu Kayumba inatosha. Pesa mnayopoteza huko EMs and Private Schools itumike kwenye mambo mengine.

Kwa issue ya Kifo cha wakili huyu on the prima facie inaonekana kabisa kijana alidekezwa tangu akiwa mtoto.

HAYA sasa twende kazi. Kimbia haraka sana toa watoto wako EMS warejeshe Kayumba haraka sana.

Utakuja kunishukuru.

🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
Kumsomesha mtoto shule nzuri haihusiani na kuwadekeza. Kuna matajiri wanawasomesha watoto shule nzuri ila ikifika likizo ni kazikazi.
 
Poleni sana mawakili na wanasheria.

Anyways wazazi msisahau kuna tofauti kubwa sana kati ya kulea mtoto na kumtunza mtoto.

Hakuna kitu kibaya kama kumlea mtoto kwa kumdekeza kwa kumpa kila kitu.

Wafundisheni watoto wenu kuhusu maadili mema na namna ya kuishi.

Ndio maana kila siku nawaambia wazazi mnao somesha. Hakuna haja ya kujistress kulipa mamilioni kusomesha watoto shule za English Mediums.

Somesheni watoto wenu Kayumba inatosha. Pesa mnayopoteza huko EMs and Private Schools itumike kwenye mambo mengine.

Kwa issue ya Kifo cha wakili huyu on the prima facie inaonekana kabisa kijana alidekezwa tangu akiwa mtoto.

HAYA sasa twende kazi. Kimbia haraka sana toa watoto wako EMS warejeshe Kayumba haraka sana.

Utakuja kunishukuru.

🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻

ndio maana nitaendelea kuamini kutafuta vya kwangu si kusubiri mzazi anipe.

kurizika ni kitu chema sana
 
Katika tukio la kusikitisha lililotokea tarehe 18 Oktoba 2024, Juma Majalla, mtoto wa kwanza wa Wakili Riziki Majalla, amekamatwa na polisi wa Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua baba yake baada ya mzozo wa kifedha. Inasemekana kuwa Juma alimua baba yake kwa makusudi baada ya baba yake huyo kumkatalia kumpa pesa alizokuwa akizihitaji.

View: https://youtu.be/B0CjY6jWcaU?si=kWNdHGBRQGNi_e3p

Taarifa zinaonyesha kuwa huu haukuwa mzozo wa kwanza kati ya Juma na marehemu baba yake, kwani Juma alishawahi kumtishia baba yake mara kadhaa, akisema siku moja atakuja kumuua. Hili sasa limekuwa kweli, kwani Juma ametekeleza kitendo hicho kibaya dhidi ya mzazi wake.

Wakili Riziki Majalla, aliyekuwa na namba ya usajili 8659 katika Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), alikuwa na watoto watatu, ambapo Juma ni wa kwanza. Tukio hili limewashtua wengi, kutokana na mazingira ya kutisha yaliyosababisha kifo cha Wakili Majallah.

Kwa sasa, Juma Majalla anashikiliwa na polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili kubaini undani wa tukio hili la kikatili. Heshima za mwisho kwa marehemu Wakili Riziki Majalla zinaendelea nyumbani kwake Kibaha kwa Mathias, kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda Nzega kwa ajili ya mazishi.

View: https://youtu.be/bLuML81SlFs?si=Zso_f6NPo-N1dRZW

Apumzike kwa amani marehemu. Huwa inasemwa, kila kifo huacha funzo kwa waliobaki, lakini kifo hiki kina funzo kubwa zaidi kwa tuliobaki duniani.

Kiukweli, wazazi kuna umuhimu wa kujiimarisha kwenye malezi, siyo tu kwa sababu Mungu amekupa watoto ndiyo ujione unajua kulea. Tujifunze kulea.

Sio suala la kusema kizazi hiki kina kasoro, ila ni sahihi kusema kwamba malezi tu ndiyo yenye kasoro zinazosababisha matukio kama haya kutokea, bila kujali nyakati.

Kwani, hata miaka ya themanini, mtoto wa Jenerali Ulimwengu aliwahi kujiua kwa kuwa alizuiwa na wazazi wake kwenda kwenye sherehe ya rafiki yake.

Tujifunze kulea watoto wetu.

Ova
 
Back
Top Bottom