KIBAHA: Wakili Riziki Majallah auwawa na mwanaye wa kumzaa kisa kumnyima pesa


Hii nimeitoa Facebook naona jamaa nyumba ilishamshinda maana dogo alikuwa amezidisha hatari lakini yeye hakuona umuhimu wa kumuwahi,halafu jamaa alikuwa amepewa kitengo Dodoma ndiyo alikuwa anajiandaa kwenda ku-report
 
Safi sana
 
Kumsomesha mtoto shule nzuri haihusiani na kuwadekeza. Kuna matajiri wanawasomesha watoto shule nzuri ila ikifika likizo ni kazikazi.
 

ndio maana nitaendelea kuamini kutafuta vya kwangu si kusubiri mzazi anipe.

kurizika ni kitu chema sana
 
Apumzike kwa amani marehemu. Huwa inasemwa, kila kifo huacha funzo kwa waliobaki, lakini kifo hiki kina funzo kubwa zaidi kwa tuliobaki duniani.

Kiukweli, wazazi kuna umuhimu wa kujiimarisha kwenye malezi, siyo tu kwa sababu Mungu amekupa watoto ndiyo ujione unajua kulea. Tujifunze kulea.

Sio suala la kusema kizazi hiki kina kasoro, ila ni sahihi kusema kwamba malezi tu ndiyo yenye kasoro zinazosababisha matukio kama haya kutokea, bila kujali nyakati.

Kwani, hata miaka ya themanini, mtoto wa Jenerali Ulimwengu aliwahi kujiua kwa kuwa alizuiwa na wazazi wake kwenda kwenye sherehe ya rafiki yake.

Tujifunze kulea watoto wetu.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…