KIBAHA: Wakili Riziki Majallah auwawa na mwanaye wa kumzaa kisa kumnyima pesa

Huko Kibaha kuna pepo mchafu mwezi huu
Si wamemuua mume wa mdaiwa wa OYA majuzi tu!!
Who is next?
 
Uko shallow sana

Watoto wangapi wa st Kayumba wameua wazazi au Walezi wao? Watoto wangapi wa EM hawana shida hizi?

It’s a mental health situation, abuse or even mob psychology

You can’t judge just like that

Anyways …. It seems like una chuki nyingi kidogo
 
Hili nimeshuhudia mzazi ana dekeza litoto mwisho wa siku linakua LIABILITY na mifano ya wazi ipo mingi Sanaa.

Yaan mzee analea mtoto wake wa kiume 30's ana mke na watoto wawili wote wanalelewa nyumbani mtoto hajishuhurishi kwa chochote zaidi ulevi wa bangi na pombe.

Mzee alikua na position nzurii ya kazi permanent & pensionable
Dogo akiomba pesa kwa mzee wake akanyimwa anamletea fujo mzee na mzee anampenda mtoto wake anaweza kopa hata ili ampe mtoto..

Wazazi tulee vijana wetu vyema kwenye maadili mema.
 
Duuh
 
Duh pesa za baba mtoto anazitakaπŸ₯±
 
Hii taarifa mbona haitaji umri wa marehemu wala wa mtuhumiwa?
 
Mbona wewe kuna uzi niliona umeandika wanao wanasoma Olimpio

kwani sio English Medium hiyo...?
 
Walikuwa ni familia bila mama!? Yuko wapi? Je ugomvi ulikuwa pesa tuu? Au kuna ziada?
 
Kama huna familia
Kaa kwa kutulia ....
Nina familia, naongea with experience.

Mtoto unatakiwa umnyooshe awe na adabu hata kumwambia mzazi wake aahh, aogope, nimeona watoto wengi wanaodekezwa dekezwa wanavyobafilika haswa kipindi cha balehe.

Nimeyaona haya kwa familia nyingi sana.
 
Nyendo ameandika uzi watoto wasio na Maadili.

Nadhani ameyapata bila kutumia nguvu.
 
Walikuwa ni familia bila mama!? Yuko wapi? Je ugomvi ulikuwa pesa tuu? Au kuna ziada?
Mtoto ana shida afya ya akili .....dish limeyumba....slways anataka pesa alanywe pombe.....shida iko hapo.....23yrs kijana akili Milembe case
 
Nina watoto 5 lakini sikai na mtoto hata mmoja. Kila mtu achakure chakure kama kuku jalalani kutafuta maisha. Shikamoo/heshima za kuamkiwa asubuhi na mchana kuombea chai na ugali sizihitaji kabisa. Nitakupa mtaji lakini sio hela ya matumizi. Nilitoka kwetu kusini kuja Dar kutafuta, nawe mtoto hangaika.
 
Tusi-jump in the conclusion. Maelezo yako yanatoa hukumu ya moja kwa moja kwa wazazi wa mtoto kumbe pengine haikuwa hivyo. Halafu mawazo yako kuhusu elimu yako primitive sana sana. Nadhani uwezo wako wa kusomesha watoto ni mdogo ndiyo maana unakuwa na inferiority complex kwa wenye uwezo wa kusomesha watoto wao vizuri au hukubahatika kupata elimu nzuri na umekulia kwenye familia chovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…