Kibatala awataka Ndugai na Mahera mahakamani

Wakili Peter Kibatala amesema atawahitaji aliyekuwa spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai na aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Charles Mahera ili wahojiwe kuhusu wabunge 19 walioapishwa kwa tiketi ya CHADEMA.

Kibatala amesema ni lazima viongozi hao wahojiwe kwa kuwa ndio waliowapitisha na kutoa kaulinza kuwalinda kwa hali youote ili wabaki bungeni.

Kati ya maswali ambayo Kibatala atapenda kuuliza ni pamoja na mbunge mmoja kuapishwa japo hakupitia mchakato wa uchaguzi.

Dkt. Mahera atatakiwa kueleza alipoipata barua ya majina wakati katibu wa chadema aliikana barua hiyo.

Pia majina ya wabunge hayakutangazwa kama utaratibu unavyohitaji.

Wabunge 19 wamefungua mashtaka ya kufukuzwa uanachama bila kufuata itaratibu
Ndugai: Mheshimiwa Hakimu naomba nikakojoe

Hakimu: Utasindikizwa na askari
 
Naomba niulize swali kwa manguli wa sheria hapa jukwaani......

Nadhani kesi ya msingi ni wakina Halima Mdee dhidi ya CHADEMA wakipinga kuvuliwa uanachama wao bila kufuata utaratibu wa chama.......madai ya Kibatala kwa Ndugai ni kwanini aliwaapisha kina Halima UBUNGE Hali ya kuwa hawakuwa halali.....na kuhusu mwenyekiti wa time ya uchaguzi ya kupokea barua ya majina ya akina Halima hali ya kuwa hayakuwa na baraka za chama...... nadhani hizi ni hoja mbili tofauti na hazihusiani na kesi ya msingi iliyopo mahakamani kwa sasa....Mimi si mjuzi wa masuala ya sheria bali ni mtazamo wangu.....ningependa manguli wa sheria hapa jukwaani wanifafanulie kwa faida ya wengi.....natanguliza shukrani zangu za dhati......
Kupata ukweli wa jambo unahitaji kuwa na muono mpana na mpaka mbali (wide and long vision).
Haiwezekani kuangalia kitu kimoja tu kama mawazo ya kuku anayelinda yai moja.
Uamuzi wa haki hupatikana kwa mahakama kupata ushahidi wa namna hiyo.
 
Huna akili kwani Ndugai aliwapitisha kama watoto wake au kama Spika??

Kwani kahama na ofisi yake??

Si kuna spika mwingine??

Wakati mwingine utumie ubongo badala ya miguu kufikiri.
Stroke, usijifanye unajua wakati inaonekana unastahili kupelekwa darasa la awali katika masuala yakisheria.

Hata siku moja, ofisi haitoi ushahidi bali ni mtu. Mtu huyo anaweza kutoa ushahidi kama mtu binafsi au kama mwakilishi wa ofisi . Ndiyo maana Mkapa akiwa Rais Mstaafu alienda kutoa ushahidi kwenye kesi ya Prof. Mahalu. Hakwenda Kikwete.

Mahakama kwa ujumla hutaka kusikia ushahidi kutoka kwa mtu mhusika. Mtu aliyeshuhudia.
 
Aliwaapisha kama Ndugai au kama Spika??
Hoja yako hiyo ingekuwa na mantiki, hata kesi za kutumia madaraka au ogisi zisingekuwepo.

Basi uombe na Sabaya afutiwe kesi maana aliyafanya yale kama DC. Ashtakiwe DC wa Hai wa sasa.
 
Unarudia makosa yale yale ya wenzako waliopita.
 
Naomba niulize swali kwa manguli wa sheria hapa jukwaani......

Nadhani kesi ya msingi ni wakina Halima Mdee dhidi ya CHADEMA wakipinga kuvuliwa uanachama wao bila kufuata utaratibu wa chama.......madai ya Kibatala kwa Ndugai ni kwanini aliwaapisha kina Halima UBUNGE Hali ya kuwa hawakuwa halali.....na kuhusu mwenyekiti wa time ya uchaguzi ya kupokea barua ya majina ya akina Halima hali ya kuwa hayakuwa na baraka za chama...... nadhani hizi ni hoja mbili tofauti na hazihusiani na kesi ya msingi iliyopo mahakamani kwa sasa....Mimi si mjuzi wa masuala ya sheria bali ni mtazamo wangu.....ningependa manguli wa sheria hapa jukwaani wanifafanulie kwa faida ya wengi.....natanguliza shukrani zangu za dhati......
Kwenye ushahidi, sheria inatamka wazi kuwa mtu yeyote anaweza kuitwa kutoa ushahidi na upande wowote alimradi upande uliomtaka huyo shahidi kama unaamini shahidi huyo atakuwa na msaada kwenye kesi iliyopo mahakamani.

Na pia inasema, shahidi unaweza kuulizwa swali lolote alimradi lisiwe la kutwezwa utu wako. Una uhuru wa kujibu au kukaa kimya, lakini huwezi kusema kuwa sijibu kwa sababu halihusiani na kesi iliyopo.

Mwisho wa kesi, mahakama ndiyo huamua kuchukua ushahidi wa nani kutegemeana na umuhimu wa ushahidi wenyewe na shahidi mwenyewe. Ndiyo maana mtu ameitwa kwenye ushahidi wa wizi, lakini anaulizwa elimu yake.
 
..msishangilie kabla ya wakati

..huwezi kujua maamuzi ya Jaji yatakuwa nini?

..upo uwezekano wa Jaji kukataa kuwaita Ndugai na Mahera kama mashahidi ktk kesi.

..kama mtakumbuka ktk kesi ya Mh.Mbowe Jaji alikataza jina la Mh.Hussein Mwinyi kutajwa mahakamani, au kumuita kama shahidi wa upande wa washtakiwa.

Cc The Palm Beach. Erythrocyte
Mwanaccm mwenzangu kwani mwisho kesi ilifutwa na nani ?
 
Kwenye ushahidi, sheria inatamka wazi kuwa mtu yeyote anaweza kuitwa kutoa ushahidi na upande wowote alimradi upande uliomtaka huyo shahidi kama unaamini shahidi huyo atakuwa na msaada kwenye kesi iliyopo mahakamani.

Na pia inasema, shahidi unaweza kuulizwa swali lolote alimradi lisiwe la kutwezwa utu wako. Una uhuru wa kujibu au kukaa kimya, lakini huwezi kusema kuwa sijibu kwa sababu halihusiani na kesi iliyopo.

Mwisho wa kesi, mahakama ndiyo huamua kuchukua ushahidi wa nani kutegemeana na umuhimu wa ushahidi wenyewe na shahidi mwenyewe. Ndiyo maana mtu ameitwa kwenye ushahidi wa wizi, lakini anaulizwa elimu yake.
Ubarikiwe sana ndugu kwa kuchukua muda wako na kunipa elimu hii kubwa.....uwe na wakati mwema....
 
Kupata ukweli wa jambo unahitaji kuwa na muono mpana na mpaka mbali (wide and long vision).
Haiwezekani kuangalia kitu kimoja tu kama mawazo ya kuku anayelinda yai moja.
Uamuzi wa haki hupatikana kwa mahakama kupata ushahidi wa namna hiyo.
Asante ndugu kwa ufafanuzi huu....
 
Hao ni waliotoa baraka za wizi wa kura 2020 kwa namna moja au nyingine wana uhusika wa moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom