Kibatala na Mawakili wenzake upande wa utetezi wamesomea mambo ya mtandao? Mbona wanayajua sana? Nijuzeni

Kibatala na Mawakili wenzake upande wa utetezi wamesomea mambo ya mtandao? Mbona wanayajua sana? Nijuzeni

Ndo maana ya kuitwa wakili msomi
Kila kitu unatakiwa ujue
Ikija kesi inayohusu anga anatakiwa ajue mambo ya anga
Ikiwa kesi inahusu mwili wa binadamu labda dokta alikosea operesheni anatakiwa ajue kila kitu
Ndo maana waitwa wakili msomi babu .upo nyonyo??
Ndugai alipiga malufuku bungeni hilo jambo la kujiita wakili msomi
 
Kunatimu kubwa sana wanafanya nao kazi kwenye hiyo kesi ,usiwaone wapo hspo kumi au ishirini ukadhani ni wao tu.
Kuna wataalamu wa kila kinachohusiana na hiyo kesi wengine ni kutoka nje
Hapo nakuunga mkono,mazingira ya cross zao hakika zinahitaji upana wakimataifa.aliyesomea IT haeleweki kimajibu
 
Ndo maana ya kuitwa wakili msomi
Kila kitu unatakiwa ujue
Ikija kesi inayohusu anga anatakiwa ajue mambo ya anga
Ikiwa kesi inahusu mwili wa binadamu labda dokta alikosea operesheni anatakiwa ajue kila kitu
Ndo maana waitwa wakili msomi babu .upo nyonyo??
Kama ni hivyo mbonq wale wa serikali hawana uwezo huo wakati nao ni mawakili wasomi!!mi nadhani ni uwezo binafsi tu wa wakili mwenyewe!!!
 
Kibatala ni noma tuache utani, huyu jamaa nimefatilia hii kesi kuanzia mwanzo hadi mwisho nimejifunza vingi sana kutoka kwake

Mwanzo anapoongozwa shahidi wa serikali na kwa namna ambavyo anadadavua taaluma yake huwa najiuliza hivi kama hapa kibatala atamkamatia wapi huyu shahidi maana kaongelea vitu vikubwa ambavyo ili kuvijua mpaka ukafika level ya kumkosoa unatakiwa uwe umevisomea haswa, lakini kibatala anakuja kuni prove wrong tena hata hajisumbui

Nikasema inawezekana hawa anawakamata kwasababu hawajui sheria hivyo jamaa ni technics za kuijua sheria ndizo zinazomfanya awashike mbavu hawa mashahidi

Lakini ile siku alipokuja shahidi ambaye pia ni mwanasheria nikasema yes hapa kibatala kaletewa spana yake ebu ngoja nione hii league itaishaje, lakini baadae nikaja kugundua afadhali ya wale wengine waliopita ambao hawajui sheria

Maana huyu alikuwa anabananishwa na vifungu vya sheria ambavyo vilikuwa vinaonesha kavunja hadi sheria ya kutunza privacy za mteja kwa ku leak information zao.

Kibatala na jopo lake nimewa nyooshea mikono, na ukumbuke mle mahakamani sio vita kati ya utetezi na jamhuri hadi jaji naye kuna part ana play, so jamaa wako outn umbereed lakini wameweza kuwabana vilivyo
 
Ndio maana ya Wakili msomi lazima ujue kila kitu kuna watu wanachukia na kukuona mjuaji
 
Kibatala: Kwanini tusiseme wewe ni miongoni mwa kikundi ndani ya Jeshi la polisi ambacho kilihusika na kupanga njama za Kumpa Freeman Mbowe Kesi ya Ugaidi Ndiyo Maana mlifanya uchunguzi kipindi fulani hadi fulani?
 
Nao huwa wamejipanga hivyo hivyo wakati wao ukifika wa re-examination ili kuweka mambo sawa pale ushshidi wa mteja wao ulipotikiswa wakati wa cross examination. Huo ndiyo ulivyo mchezo wa mahakamani. Mwisho wa mchezo ni hakimu au jaji anayeamua mshindi wa huo mchezo.

Bado ngoma ni mbichi. Tegemea kuona video na audio clips za Mbowe zikiwasiliana na Komandoo Deus Urio ambaye hivi punde atatinga kizimbani akiwa ni shahidi wa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakina Kibatara wako pale kupiga pesa ya chadema isiyopungua 5 million kwa siku. Ndiyo maana kaacha kazi zake nyingine zote. Wahenga wanasema kufa kufaana. Lazima Kibatara aonekane pesa hiyo kaifanyia kazi.
Milembe hospital njoo mchukue mtu wenu huku.
 
Huwa najiuliza wafanyakazi wa serikali walisomea wapi ni weupe mno tena mnoooo
Mimi n bwege ila kwa wafanyakazi wa serikali (wengi wao) siwakuti kwa ubwege

Ila Yana nafasi kubwa dadeq, hela nzuri ila akili za kuvukia barabara

Hizo kesi zote wanapelekeshwa balaa yaani mtu anafanya Kazi za upelelezi anaulizwa kirefu cha idara yake hajui ***** wallah
Na kibaya zaidi anakutaka ukamuulize bosi wake kuhusu hilo. Lahaullah lakwata!
 
Back
Top Bottom