Kibatala na Mawakili wenzake upande wa utetezi wamesomea mambo ya mtandao? Mbona wanayajua sana? Nijuzeni

Ndugai alipiga malufuku bungeni hilo jambo la kujiita wakili msomi
 
Kunatimu kubwa sana wanafanya nao kazi kwenye hiyo kesi ,usiwaone wapo hspo kumi au ishirini ukadhani ni wao tu.
Kuna wataalamu wa kila kinachohusiana na hiyo kesi wengine ni kutoka nje
Hapo nakuunga mkono,mazingira ya cross zao hakika zinahitaji upana wakimataifa.aliyesomea IT haeleweki kimajibu
 
Kama ni hivyo mbonq wale wa serikali hawana uwezo huo wakati nao ni mawakili wasomi!!mi nadhani ni uwezo binafsi tu wa wakili mwenyewe!!!
 
Kibatala ni noma tuache utani, huyu jamaa nimefatilia hii kesi kuanzia mwanzo hadi mwisho nimejifunza vingi sana kutoka kwake

Mwanzo anapoongozwa shahidi wa serikali na kwa namna ambavyo anadadavua taaluma yake huwa najiuliza hivi kama hapa kibatala atamkamatia wapi huyu shahidi maana kaongelea vitu vikubwa ambavyo ili kuvijua mpaka ukafika level ya kumkosoa unatakiwa uwe umevisomea haswa, lakini kibatala anakuja kuni prove wrong tena hata hajisumbui

Nikasema inawezekana hawa anawakamata kwasababu hawajui sheria hivyo jamaa ni technics za kuijua sheria ndizo zinazomfanya awashike mbavu hawa mashahidi

Lakini ile siku alipokuja shahidi ambaye pia ni mwanasheria nikasema yes hapa kibatala kaletewa spana yake ebu ngoja nione hii league itaishaje, lakini baadae nikaja kugundua afadhali ya wale wengine waliopita ambao hawajui sheria

Maana huyu alikuwa anabananishwa na vifungu vya sheria ambavyo vilikuwa vinaonesha kavunja hadi sheria ya kutunza privacy za mteja kwa ku leak information zao.

Kibatala na jopo lake nimewa nyooshea mikono, na ukumbuke mle mahakamani sio vita kati ya utetezi na jamhuri hadi jaji naye kuna part ana play, so jamaa wako outn umbereed lakini wameweza kuwabana vilivyo
 
Ndio maana ya Wakili msomi lazima ujue kila kitu kuna watu wanachukia na kukuona mjuaji
 
Kibatala: Kwanini tusiseme wewe ni miongoni mwa kikundi ndani ya Jeshi la polisi ambacho kilihusika na kupanga njama za Kumpa Freeman Mbowe Kesi ya Ugaidi Ndiyo Maana mlifanya uchunguzi kipindi fulani hadi fulani?
 
Milembe hospital njoo mchukue mtu wenu huku.
 
Na kibaya zaidi anakutaka ukamuulize bosi wake kuhusu hilo. Lahaullah lakwata!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…