Kibiti mpaka laana ya Cabo Delgado: Part II

Abu Dardai Jongo yeye alikuwa na pikipiki. Alikuwa anfanya kazi ya kusafirisha watu toka mto Ruvuma mpaka Montepuez. Kitambo fulani, akaenda Macomia. Aliporejea, wenzake wanasema hakuwa tena yule Abu walokuwa wanamfahamu.
Hii inanikumbusha kituko cha Juzi juzi wakati Mwenezi Paul Makonda anafanya ziara Mkoa wa Rukwa Nkasi kuna afisa mmoja alituhumiwa Kufafirisha Wahamiaji haramu.
Tuhuma zile za yule mzee ambaye alidai ana ushahidi alihusisha maafisa wa polisi na Uhamiaji.

Je huenda hizi ndio mbinu watu hao wanavushwa?

Tuwe makini sana
 
MKIRU sasa hivi ni tulivu, kenge hao wakijitokeza tena huko mama awapeleke kuzimu wakatulie huko. Ni washenzi sana
 
Wishful thinking.

Ni miaka mingapi tangu mafunzo ya JKT kwa vijana yaanze? Ni wangapi waliopitia hayo mafunzo walipata ajira? Wangapi hawakupata?

Ukiijua JKT (JWTZ) vizuri, utaacha hizi ndoto za mchana.
 
Thank you very much
 
Dini inasingiziwa si hapo juzi tulisikia Gari lenye Bendera ya chama fulani ikisafirisha Wahamiaji haramu? Kweli wale ni Wahamiaji haramu au ndio hawa hawa Magaidi washenzi?
 

Dini inafuga ugaidi. Dunia nzima Waislamu ni asilimia 90 ya Ugaidi.
 
UKIWA MAKINI BILA KUFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE UTAGUNDUA MUANDISHI NDIO ANATENGEZENEZA PICHA YA KUHUSISHA UISLAMU NA UGAIDI ETI KISA TU ANAANDIKA ANSAR SUNNA. HIZO NDIO PROPAGANDA TUNAZOZIKATAA KWA NGUVU ZOTE.! SEHEMU TAYARI UNAONA INA RASIMALI ZA KUTOSHA KAMA GESI SASA WW UNADHANI WAZUNGU WATAWAACHA KWA AMANI.

LAZIMA WATUMIE UISLAMU KAMA KIKI KUFANIKISHA MAMBO YAO NA TAYAR WA AFRICA AKILI ZA KUFIKIRIA NI FINYU BASI WAO WANABEBA KILA AINA YA NENO WANALOLISIKIA.

SASA HAO WAISALAMU HAPO WANAUA WATU ALAFU WAO WANAPATA FAIDA GANI.?? KISHA HIYO GESI WAIPELEKE WAPI ?? ALAFU KWANN WANAOKUFA NI HAO HAO WAISLAMU WAKAZI WA MAENEO HAYO.?? HUJIULIZI PIA
???????

KUNA VITU SENSITIVES HATUWEZI KUVIANDIKA HAPA MANA MSHAZOEA KUBISHANA MTAONA PIA NI UONGO MANA NYIE MKISHA AMINI KITU NDIO HICHO HICHO HAMBADILIKI MNA VICHWA VIGUMU VYA KUKUBALI UKWELI
???
 
Wishful thinking.

Ni miaka mingapi tangu mafunzo ya JKT kwa vijana yaanze? Ni wangapi waliopitia hayo mafunzo walipata ajira? Wangapi hawakupata?

Ukiijua JKT (JWTZ) vizuri, utaacha hizi ndoto za mchana.
Ni kweli ni ndoto😀

Kwamba wao JWTZ na JKT ni special sana hapa duniani😀

Hao hao JWTZ unao wasifia ndio mambo ya panya road yametokea hapa hapa nchini tena chini ya vitoto vidogo tu na watu wazima kulazwa ndani mapema kama kuku.

Hili hili taifa ndilo yale ya kibiti yalitokea na JWTZ ikiwepo.

Rais wa nchi mchonga alinusurika kupinduliwa na hao hao JWTZ wengine kwa zaidi ya mara moja.

Wewe unafikiri hao vijana wa JKT wataendelea kuwa humble miaka yao yote huku umasikini ukiwatandika vilivyo na wanaona wakubwa wao wakitumbua tu mali na kufanya ufisadi na viongozi wa serikali huku wao wakiimbiwa uzalendo.

Unafikiri watu wanakula uzalendo etii ehhhh nakusisitiza hawa vijana sio kwamba hawawezi kufanya ila wanakosa supplier wa silaha tu maana kila sababu ya ku go against serikali wanayo hawahitaji kuambiwa na yoyote.

Ubaya au uzuri mtaani maisha kila siku yanazidi kuwa tight kwa sababu ya uongozi na hakuna mabadiliko yoyote yale.

Hata huko Msumbiji naamini kabisa walikuwepo wananchi na viongozi waliokuwa wana ongea kama wewe awali ila leo hii kiko wapi ?

Tanzania leo hii tu kuna vijana wamepotea na hawaeleweki walipoenda.

Ogopa sana mtu aliyechoka umasikini na akapata silaha huyu maana ya maisha kwake inakuwa haina uzito tena.
 
Alipohojiwa, alisema kauli hii; "Mungu, wasaidie watu wale."

Kipi kilichompelekea azungumze haya,?Alikwenda kuwasaidia,halafu anaondoka anajua fika anawaacha matatani.

Nirudie unielewe,Alikwenda kutatua tatizo,tatizo halijesha anaondoka na anawaombea Kwa Mungu.Aligundua Nini?
SteveMollel
 
Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba yale maeneo karibia yote yenye vurugu kule Msumbiji yana historia kongwe sana kuhusiana na suala la vurugu za kisiasa, hata kabla ya Taifa hilo la Msumbiji halijapata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wao Ureno. Kambi nyingi sana za Makundi ya kisiasa ya Wapigania Uhuru wa nchi hiyo ya Msumbiji ziliwekwa katika ukanda huo wa Kaskazini mwa nchi hiyo, maeneo ambayo hadi leo hii bado yanaendelea kukumbwa na vurugu. Makundi ya Wapigania Uhuru ya vyama vya Siasa vya FRELIMO na RENAMO vilikuwa na Kambi zao nyingi za wazi na za siri kubwa ktk maeneo hayo yenye vurugu kwa sasa. Baada ya kufanikisha suala la kuuangusha utawala wa mkoloni wao Ureno, maeneo hayo tayari yalikuwa yamevurugwa vibaya sana na vita vya ukombozi, miundombinu yote ya kujenga uchumi kama vile viwanda viliharabiwa kabisa na mapigano ya vita.
Mbaya zaidi, hata chama cha Siasa cha FRELIMO kilipofanikiwa kushika madaraka ktk nchi hiyo ya Msumbiji, haikukishirikisha Chama cha RENAMO ktk kuitawala nchi hiyo ya Msumbiji, badala yake vyama hivyo viligawanyika na kuwa vyama vinavyohasimiana, vikapigana vita tena wao kwa wao ili kugombea kupata udhibiti wa madaraka ktk nchi hiyo, hatimaye Chama cha RENAMO kilizidiwa nguvu na kushindwa vita. Chama cha FRELIMO kutokana na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwl. J. K. Nyerere na CCM yake, walifanikiwa kuhodhi na kudhibiti mamlaka na madaraka yote ya nchi hiyo ya Msumbiji, na RENAMO kikawa Chama kikuu cha Upinzani dhidi ya FRELIMO.
Mbaya zaidi tena, utawala wa FRELIMO ulikichukulia Chama cha RENAMO kama Kundi la Waasi wala siyo Chama cha Siasa, Matokeo yake Wanachama na Wapiganaji wa RENAMO wakakimbilia msituni na kuweka Kambi zao nyingi za Siri kwenye huo Upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Serikali ya Msumbiji Kama ililitelekeza kabisa kwa muda mrefu eneo hilo lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo kwa sababu ililiona kama eneo lenye maficho ya Waasi wa RENAMO, hata huduma za kijamii zilikuwa duni sana kwenye maeneo hayo. Wananchi wengi wa upande huo wa Kaskazini mwa nchi waliona kama Serikali ya Msumbiji imewatenga na haikuwa inawajali. Serikali ilijichimbia mizizi kwenye eneo la Kusini mwa nchi hiyo ya Msumbiji na kuigawa nchi ktk mapande mawili ya Kaskazini na Kusini. Serikali hiyo ya Msumbiji ilirudi tena kwa kasi upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya Ugunduzi wa Nishati ya Gesi kwenye maeneo hayo ya Kaskazini, hapo ndipo ukawa mwanzo mpya wa kuibuka kwa Vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa ktk eneo hilo la Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Suala la Dini au Udini ktk vurugu hizo za huko Msumbiji linatumika tu na wahusika kama "SCAPEGOAT" ili kuweza kupata msaada wa kijeshi na wa silaha za kupigania vita dhidi ya maadui zao.
 
Alikwenda kutatua tatizo gani hasa huko Msumbiji??
Shida kubwa Sana tuliyonayo sisi Watu weusi ni kwamba huwa hatupendi kabisa kufanya tafiti za kina ili kubaini kiini hasa cha Migogoro ya kibinadamu inayoliandama bara hili la Afrika. Ni lazima tuwe tunafanya utafiti wa kina ili tujue viini au vyanzo halisi vinavyosababisha Migogoro (root cause) ili tuweze kutatua Migogoro hiyo inayotuandama ktk nchi zetu hizi miaka nenda rudi.

Je, Unajua ni kwa Nini huyo mzungu (mkaburu) pamoja na wenzake walikuwepo kwenye eneo hilo lenye machimbo ya gesi huko Jimboni Cabo Delgado nchini Msumbiji wakiwa na silaha za kijeshi ikiwamo na hiyo helikopta ya kijeshi aliyotumia katikà kufanya uokoaji wa hao Watu??? Unazijua sababu???
 
Ok 👍
 
Tusaidie kw faida ya wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…