Mimi ni wa MASIHI tayari. Hiyo dini ya Allah Baki nayo wewe.
Kama wewe unataka kuifuata Dini ya Masih, jisalimishe kwa Mola Mlezi wa Viumbe vyote. Mola Mlezi wa kila kitu. Masih (Amani iwe juu yake) alijisalimisha kwa Allah Peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote na alikuwa ni Muislam, alimuabudu Allah Peke Yake bila ya kumshirikisha na chochote, fuata njia yake Masih, kuwa Muislam, usifuate njia ya Paulo.
Masih sio Allah wala sio Mwana wa Allah, Ametakasika Allah na mnayomshirikisha nayo. Mama yake sio Mama wa Mungu, Ametakasika Allah na mnayomshirikisha nayo na Ametukuka Allah na kuwa Juu Kutukuka Kukubwa Kabisa.
Mama yake Masih, Bibi Maryam alikuwa ni mwanamke mwema, msafi aliyekuwa mbali mno na machafu, sio Mama wa Mungu kama mnavyodai, Ametakasika Allah na mnayomshirikisha nayo, na wala Bibi Maryam hakuwa mchafu hakuwa mzinifu kama wanavyomtukana mayahudi waliolaaniwa.
Na mwanae Bibi Maryam, Masih, alikuwa ni Mtume wa Allah na Mtumwa wake.
ayat 64 from Surah Al Imran
﴿قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ﴾
[ آل عمران: 64]
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu.