Kibonde afariki na mamilioni ya pesa za watu

Kibonde afariki na mamilioni ya pesa za watu

Poleni sana na msiba wa Kibonde.

Najaribu kuwaza, Kibonde ni MC wa masherehe mbali mbali. Kuna wakati tulitaka kumbook tukakuta imekuwa full booked kwa jumamosi za takribani miezi minne mbele.

Sasa najaribu kujiuliza, endapo marehemu alikuwa amepokea advance (kishika uchumba) kwaajili ya kuwa MC kwenye harusi za watu, je pesa hizo ndugu zake watarudisha? Waliolipa kwa Mpesa Tigo Pesa au bank atleast wapo salama. Je, vipi kwa waliolipa cash? Yani walionana na marehemu kisha wakalipa na hawakuandikishiana popote pale

Kwa uhodari na jina alilokuwa nalo Kibonde kwenye ushehereshaji basi yawezekana kabisa kuwa atakuwa amefariki na pesa nyingi za watu waliotoa advance.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app

Mezea basi, hizo ni sehemu ya rambirambi. Hazilipiki.
 
Ndio hapo watanzania tujifunze kusaini kwenye makaratasi hata pesa kidogo tunayolipa au kupokea. Makubaliano yanayohusu pesa bila kusaini mkataba iko siku utakula hasara.
Hapo pia hoja ya ma-Mc kusajiliwa na kulipa kodi inapokuja yaani wanakuwa na ofisi kabisa kama anavyofanya yule mgogo Mc Pilipili kwa kuwa na kampuni yake na hata kama likitokea lolote basi wanaweza kumpa Mc mwingine. Ila navyojua wengi wa ma-MC huwa na umoja wao na inapotokea dharula huwa wanamleta MC mwingine
 
Ndio muwe na utaratibu wa kuweka bima, kama wanavyofanya kwenye mikopo.
 
Ni Mara chache sana wanaodai wanatokea!
Kuna jamaa yangu mmoja kauzu kweli kuna msiba mmoja watu Wako makaburini pale waliposema Je kuna mtu mtu yoyote anayemdai marehemu jamaa aliibuka [emoji23]

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ya kuitana hadharani haiko sawa, mwingine anaweza akawa anamdai marehem lakini ile nguvu ya kujitokeza mbele ya watu ili apewe haki yake anaikosa na kuamua kuipotezea kishingo upande

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BABA TUPAC leo umeongea jambo la muhimu mno, niliwahi kumuuliza mchungaji mmoja kuhusu hii sheria ambayo inatumika na waislamu baada ya kifo waislamu sharia ni kuwa hakuna kuzika mpaka marehemu asafishwe madeni yake yote, ndio maana kabla ya kumsalia inatangazwa `waumini sasa tunaenda kumsalia ndugu yetu na kumuombea dua, lakini kabla ya hapo kama kuna mtu yoyote anamdai marehemu aje hapa amalizane na ndugu zake` siku moja pale ilala msikitini alijitokeza jamaa anamdai marehemu milioni 30 ikawa kimbembe. Jirani yangu mchungaji aliniambia hata kwao pia ipo hio ila sema huwa inamezwa na uombolezaji na hakuna anaekumbushia. Kama ndugu wa kibonge ama msiba mwengine wowote mlipieni marehemu madeni yake au mkubali kuyabeba kwenye shingo zenu ili ndugu aende kwa bwana akiwa msafi.
Alizikwa huyooo?aliyedaiwa 30m

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa haina ndungu wala hisia...

Watanzania wengi sijui darasani na maishani tunafaulu vipi. Aliyetoa mada Sio Mdai hata useme pesa aina hisia. Na angekuwa Mdai hapa Sio Mahali pake, so hoja yako kuwa pesa haina hisia Au undugu hapa ni misplaced. Ni dalili ya Watu walio frustrated, wivu, kupenda na kuombea mabaya wengine. Kilicho moyoni ndo humtoka mtu. It’s very sad
 
Ni mapenzi ya Mungu , kuna jamaa alimkopesha rafiki yake 2000000 kwa faida ya asilimia 20 kwa mwezi na haikuwa na maandishi kwani walishibana . Alifariki ghafla na pesa ikapotea ghafla . Ni kujipanga tena upya .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom