AAAiiiseeee!Kudai haki na kuvunja amani ni almost sawa na kumuua mdaiwa kama fidia ya deni.
Sijui kama umeyatafakari vizuri maneno ya mstari huu.
Kwa juu juu, utadhani ni maneno yenye maana kubwa, lakini ukiyaangalia kwa uhalisia ndani yake ni maneno ya kipuuzi sana.
Hivi unajuwa maana ya "HAKI" ni nini?
Mtu anayo HAKI ya kuishi, au siyo?
Unapodai HAKI ya kuishi; huyo anaye daiwa haki hiyo ni nani; mtu ambaye anaweza kukunyima HAKI hiyo ya kuishi, au siyo?
Hapo kwenye mazingira hayo bado unafikiri "AMANI" ipo?
Hizi lugha za kilaghai laghai hizi mnazo tumia kuwalaza akili nyinyi mmejifunzia wapi hizi?Ni halali kudai haki, lakini iwe katika njia isiyovunja amani
Samia anapenda sana kutoa mipasho ya aina hii kila mara, na katika mambo mengi.
Hatimae, sasa watu wamegundua ulaghai mwingi unaotumika kulaza akili za watu.
HAKI haiombwi. Ikidaiwa na mdaiwa akitumia ulaghai, HAKI inanyakuliwa kwa njia zozote zile.
Bakini na ulaghai wa kuwapumbaza wenyewe juu ya AMANI isiyokuwepo.