Kichaka cha 'TUILINDE AMANI YA NCHI' kinapaswa kufyekwa ili tuweze kuendelea kama nchi

Kudai haki na kuvunja amani ni almost sawa na kumuua mdaiwa kama fidia ya deni.
AAAiiiseeee!
Sijui kama umeyatafakari vizuri maneno ya mstari huu.

Kwa juu juu, utadhani ni maneno yenye maana kubwa, lakini ukiyaangalia kwa uhalisia ndani yake ni maneno ya kipuuzi sana.

Hivi unajuwa maana ya "HAKI" ni nini?
Mtu anayo HAKI ya kuishi, au siyo?
Unapodai HAKI ya kuishi; huyo anaye daiwa haki hiyo ni nani; mtu ambaye anaweza kukunyima HAKI hiyo ya kuishi, au siyo?
Hapo kwenye mazingira hayo bado unafikiri "AMANI" ipo?
Ni halali kudai haki, lakini iwe katika njia isiyovunja amani
Hizi lugha za kilaghai laghai hizi mnazo tumia kuwalaza akili nyinyi mmejifunzia wapi hizi?
Samia anapenda sana kutoa mipasho ya aina hii kila mara, na katika mambo mengi.

Hatimae, sasa watu wamegundua ulaghai mwingi unaotumika kulaza akili za watu.

HAKI haiombwi. Ikidaiwa na mdaiwa akitumia ulaghai, HAKI inanyakuliwa kwa njia zozote zile.

Bakini na ulaghai wa kuwapumbaza wenyewe juu ya AMANI isiyokuwepo.
 
🤣🤣🤣🤣. Watu ni wajanja Sana wanataka wakiibia nchi basi wale na familia zao bila kwere wala kelele🤣🤣🤣🤣
 
Kifyekwe kabisa na mizizi ing'olewe, bunge butu halina meno, bunge lina wajibu wa kuisimamia serikali, lakin kila mbunge akisimama mama mama mama kuna kusimamiana hapo?
 
Hawa mashetani ni wabaya kuliko hata shetani mwenyewe!!
 
Ni ukweli.
Mtu asiibe pesa zetu kwa kisingizio chochote.
Lakini mtu akihatarisha amani yetu pia ashughulikiwe kwa mujibu wa katiba yetu na si kisiasa.
Viongozi wezi wa mali zetu, muache huu ujinga.
 
Kwa hiyo amani haipaswi kulindwa? Kweli demokrasia ni mavi kabisa.
 
Kwa hiyo amani haipaswi kulindwa? Kweli demokrasia ni mavi kabisa.
Amani na haki vinapaswa kulindwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa demokrasia. Amani na haki ya kweli ni pamoja na ile iliyopo moyoni, si amani ya unyonge, si amani bila haki! Hiyo si amani!.Amani ya kweli ni pamoja na kuhoji na kufahamu ukweli juu ya mapato na matumizi ya serikali, amani ya kweli ni pamoja na kupata uchumi imara tuepuke umasikini.
 
Mkuu tuingie porini vinginevyo tutakuwa keyboard warriors tu na hamna kitakachobadilika
 
Tatizo lenu mmekaririshwa. Nchi ina miaka 64 je hatujapiga hatua yoyote? Iyo haki unayosema iachwe hata kama inahatarisha uhai wa Taifa? Ripoti ya CAG haikagui Mapato na matumizi ya serikali? Je ni sahihi kushirikiana na wanaharakati wa nje kumdhihaki na kumtuna Rais na nchi yako?
 
Angalia hii ropokaji imevimbiwa amani.
 
Yaliyotokea Kenya, hatujajifunza bado? South Sudan, DRC?

Ni halali kudai haki, lakini iwe katika njia isiyovunja amani.

Kudai haki na kuvunja amani ni almost sawa na kumuua mdaiwa kama fidia ya deni.
Ni nani huwa anavunja amani, kama sio hao walinda amani chini ya CCM.?
 
Amani ya nchi huku wanatuibia kila siku!!
 
Umeachiwa Shamba kubwa lenye rutuba na miti ya matunda, Mgodi wa tanzanite, ng'ombe wa maziwa elfu moja na eneo kubwa la kufanyia biashara, Kisha baada ya miaka 64 maendeleo pekee yanayoonekana kwako ni kutembelea baiskeli ya phoenix! Hayo ndiyo maendeleo unayotaka? Miaka 64 nchi ina kila aina ya rasilimali ila mwaka huu 2025 kuna wanafunzi wanaketi chini kwa kukosa madawati!, Hiyo ndiyo amani unayoitaka? Hiyo ndiyo amani ya moyoni? Nadhani ulipaswa kuungana na hao wanaharakati wa nje kwa nguvu zote kukemea na kuvunja huu mnyororo wa umasikini na unyonge
 
Umeandika kiharakati sana. Umeacha ukweli wa kihistoria na hali halisi. Bahati mbaya una argue kama mtoto wa darasa la pili.
 
Hii nchi shida sio mapato!
Ni matumizi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…