Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Waliofutiwa matokeo ni watahiniwa 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita na 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE), baadhi wakitajwa kutumia AI (Chatgpt).
Tazma hapa matokeo ya kidato cha Sita 2026 > NECTA
Aidha, Baraza limekifungia kituo cha mitihani cha P5584 Excellency Open School kilichopo mkoani Manyara kutokana na kukiuka miongozo ya uendeshaji wa Mitihani ya Taifa. Kituo hicho kitaendelea kufungwa hadi NECTA itakapojiridhisha kuwa kinafaa kuendesha mitihani kwa usalama.
Katibu Mtendaji Prof. Said A. Mohamed ameongeza kuwa ufaulu wa watahiniwa wa shule umefikia 99.92%, huku ukibaki juu ya 99% kwa miaka minne mfululizo. Amesema pia idadi ya waliopata Division One imeongezeka hadi 54.1% kutoka 48.6% mwaka 2025.