Kidato cha 6 wakamatwa wakitumia ChatGPT, NECTA yawafutia matokeo

Kidato cha 6 wakamatwa wakitumia ChatGPT, NECTA yawafutia matokeo

Tumia chatgpt iulize maswali utagundua utofauti katika namna inavyoandika, yani kiufupi AI zinajibu kiufundi sana na mpangilio sahihi wa maneno!. Chengine nafikiri waligundua mfanano wa majibu kwa watu kadhaa, yani mfano watu kumi muulize swali moja chatgpt itawajibu hivyohivyo so nawewe ukikopi hivyohivyo basi mfanano lazima uonekane tu!.
Katika sehem chatgot ana win ni utofauti wa majibu. Kwenye hiyo case ya necta wahusika walikamatwa na simu. Na siyo form six ila ni wanafunzi wa ualimu coz hao huruhusiwa kwenda na simu chuo.
 
Ilikuwaje wakaruhusiwa kuingia na devices zenye ku-access internet na wakafanikiwa ku-search kwenye AI? Wasimamizi wa mitihani kwa shule na vyuo husika wachukuliwe hatua.
 
Tumia chatgpt iulize maswali utagundua utofauti katika namna inavyoandika, yani kiufupi AI zinajibu kiufundi sana na mpangilio sahihi wa maneno!. Chengine nafikiri waligundua mfanano wa majibu kwa watu kadhaa, yani mfano watu kumi muulize swali moja chatgpt itawajibu hivyohivyo so nawewe ukikopi hivyohivyo basi mfanano lazima uonekane tu!.
Right! My son!
 
Simu zilipita wapi..?!
Hapo ni hongo tu zilitembea kwa wasimamizi,wakawaacha watahiniwa waingie na simu..
Chumba cha mtihani si huwa kuna /Polisi-CCM/Mlinzi-CCZm/Mgambo-CCM na Green Guard,wanafanya upekuzi?!!CCM mlishawazoesha hela kwenye usimamizi wa chaguzi ili waibe kura za CHADEMA..halafu mnalalama??!
Chanzo ni CCM tu..Ni hatari mno...
 
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Waliofutiwa matokeo ni watahiniwa 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita na 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE), baadhi wakitajwa kutumia AI (Chatgpt).

Tazma hapa matokeo ya kidato cha Sita 2026 > NECTA

Aidha, Baraza limekifungia kituo cha mitihani cha P5584 Excellency Open School kilichopo mkoani Manyara kutokana na kukiuka miongozo ya uendeshaji wa Mitihani ya Taifa. Kituo hicho kitaendelea kufungwa hadi NECTA itakapojiridhisha kuwa kinafaa kuendesha mitihani kwa usalama.

Katibu Mtendaji Prof. Said A. Mohamed ameongeza kuwa ufaulu wa watahiniwa wa shule umefikia 99.92%, huku ukibaki juu ya 99% kwa miaka minne mfululizo. Amesema pia idadi ya waliopata Division One imeongezeka hadi 54.1% kutoka 48.6% mwaka 2025.

Hakika ni hatari
 
Zipo mkuu

Zipo za chatgpt, DeepSeek na nyengine, black and white usipokua makini huwezi jua.

Huu mchezo haujaanza na Ai even before AI kuna calculator zina memory unasave formula na material kibao, msimamizi kama sio mzoefu hawezi jua.
YAH mkuu calculator zile mfano ,maswali Ya matrix ile
ya row tatu na colum tatu
au mbili kwa mbili
Ilikua inakuelekeza uanze kuweka vep data

Ukija kwenye function haswa inverse yake ukifanya kwakutumia ile calculator unaomba na graph na

Kimsingi ile calculator kwa anaejua kutumia anapiga balaa
 
NGOJA NIMALIZIE IBADA KWA MWAMPOSA
 DUHU
 
Uwe na adabu kijana wewe ni mdogo sana sanaaa kwangu!

Yaani mkijikusanya wewe na kaukoo kenu MJIJUMLISHE WOTEEEEEEE hakuna aspect in life yoyote mnayo nizidi Mimi.

NB. Elimu ya kweli ni kile kinacho bakia KICHWANI kwako baada ya ku graduate kikusaidie kupambana na maisha/ mazingira yako.. ukiona elimu haikusaidi basi hiyo elimu ni SCAM.
mkubwa huko unakoishi, humu jf tunapambana na ukubwa wa hoja mkuu! Kuhusu elimu nakuunga mkono.
 
hayo ni maoni yako binafsi gentleman,
ambayo ni imani yangu yanafaa kugeuzwa kua fursa muhimu sana ya kujipanga upya tena, kujirekebisha na kufanya vizuri zaidi mbeleni
we jamaa uwe muelewa, watoto 58 wamefutiwa matokeo ya mtihani kwa kosa la kutumia AI kujibu mitihani, hao 58 ni waliogundulika, je,unafahamu ni watoto wangapi ambao walitumia AI na hawajagundulika? huoni hao waliotumia udanganyifu huo na hawajagundulia maana yake tunapeleka watoto vilaza vyuo vikuu? matokeo yake mtu anakutishia na li cheti la digrii amemaliza chuo kumbe hata akili ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi hana? lazima hili swala la AI tulivalie njuga, vinginevyo tunazalisha akina tilatilaa vilaza watupu katika nchi hii. usiishie tu kusifia mkuu angalia na upande wa pili ndugu.
 
Hakika mkuu
 
Back
Top Bottom