Kidato cha 6 wakamatwa wakitumia ChatGPT, NECTA yawafutia matokeo

Kidato cha 6 wakamatwa wakitumia ChatGPT, NECTA yawafutia matokeo

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Waliofutiwa matokeo ni watahiniwa 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita na 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE), baadhi wakitajwa kutumia AI (Chatgpt).

Tazma hapa matokeo ya kidato cha Sita 2025 > NECTA

Aidha, Baraza limekifungia kituo cha mitihani cha P5584 Excellency Open School kilichopo mkoani Manyara kutokana na kukiuka miongozo ya uendeshaji wa Mitihani ya Taifa. Kituo hicho kitaendelea kufungwa hadi NECTA itakapojiridhisha kuwa kinafaa kuendesha mitihani kwa usalama.

Katibu Mtendaji Prof. Said A. Mohamed ameongeza kuwa ufaulu wa watahiniwa wa shule umefikia 99.92%, huku ukibaki juu ya 99% kwa miaka minne mfululizo. Amesema pia idadi ya waliopata Division One imeongezeka hadi 54.1% kutoka 48.6% mwaka 2025.

Haya matokeo ya kidato cha sita mwaka huu yameakisi matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka jana—99% vs 98%.
Ufaulu wa kishindo vs uchaguzi wa kishindo.
Waliopata division 1 wapelekwe Havard au MIT wote.
Kuwapeleka jalalani university ni kuwashusha hadhi
 
mkuu inabidi nipate elimu kutoka kwako. hapo kutumia prompt imekaaje hapo?
Prompt ni kama unaiambia/unaiamrisha Ai ijibu kwa mpangilio unaotaka wewe,

Mfano wa prompt

"Answer this in 50 words or less. No filler, no explanations, just the facts."

Unaweza ukauweka prompt hio kwenye swali, so inakupa jibu fupi Tu halafu wewe kwa kutumia Akili yako toka kwenye jibu ndio unaweka maelezo
 
Itakua ni simu ,now wanafunzi wengi wanaingia na simu hao ni kikundi kidogo kilichoshitukiwa.
Kuna Dogo mmoja tunafanya nae kazi ni injinia wa umeme anasema toka kidato cha sita hadi anamaliza chuo hawezi ingia kwenye pepa bila simu.
Duh, itakuwa usimamizi wa mtihani wa siku hizi si kama zamani...

Zamani hadi chooni unasindikizwa na askari.. sijui kama hizi taratibu bado zipo..
 
Mwenye uelewa anisaidie ni vipi mtu anaweza baini kuwa hiki kitu kimeandikwa kwa AI au ni kwa kuwaza tu au Kuna vifaa vya kubaini AI generated contents
Kwa muktadha wa NECTA hao watahiniwa walikutwa na simu, na walikua wanatumia chatgpt kuuliza maswali.

Ila kuhusu kuhusu kujua chat gpt imetumika unaingiza ile document our maandishi yale kwenye software za plagiarism check kama Turnitin au grammarly.
 
Ukicopy na kupaste ni rahisi kujulikana

1. Msahihishaji anaweza weka swali kwenye AI na kuona ufanano wa jibu

2. Ai usipotumia prompt majibu yake yanaonesha kabisa hii ni AI the way inavyoelezea kwa maelezo mengi kupita kiasi yasiyo na ulazima

3. Zipo detectors sema ni kwa kudetect wa juu ambao ni layman

Kwa wazoefu ngumu mno kudetect
Kwa sisi ambao tumeandaa ma proposal mengi mengi

Huwa tunaweza ku edit.. idea noma mtu asigundue
 
Duh, itakuwa usimamizi wa mtihani wa siku hizi si kama zamani...

Zamani hadi chooni unasindikizwa na askari.. sijui kama hizi taratibu bado zipo..
Inategemeana tena mitihani hii maswali sijui 10 pepa inapigwa picha yote Ai anajibu ndani ya sekunde, Unakuta wajanja wanaandika key points. Hayo mabogus ndio yanacopy kila kitu ndio maana yamedakwa kama kuku.
Tena hizi scientific calculator ndio wanatumia kuweka simu kwenye mfuniko ule wa nyuma.
 
Hawa wanafunzi WA siku hizi wahuni Sana kama hiyo Chatgpt ukibahatika kupiga picha mtihani inakusolvia wote, ila kuna namna ya kumkamata mwanafunzi,zipo namna nyingi mno,
1.unaweza kuuliza huo mtihani Chatgpt ukiona kuna mfanano mkubwa ujue ilitumika
2.pia the way mtu alivyojibu Kwa ufasaha na bila kukosea hata nukta, maana Chatgpt iko very smart
3.lakini pia unaweza kuona Lugha ni ya kitaalamu sana kuliko kiwango cha kawaida cha mwanafunzi.
4.Na vinginevyo
 
Back
Top Bottom