Kidato cha 6 wakamatwa wakitumia ChatGPT, NECTA yawafutia matokeo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya watahiniwa 58 baada ya kubainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani. Waliofutiwa matokeo ni watahiniwa 44 wa Mtihani wa Kidato cha Sita na 14 wa Mtihani wa Stashahada ya Ualimu wa Elimu ya Msingi (DPEE), baadhi wakitajwa kutumia AI (Chatgpt).

Tazma hapa matokeo ya kidato cha Sita 2026 > NECTA

Aidha, Baraza limekifungia kituo cha mitihani cha P5584 Excellency Open School kilichopo mkoani Manyara kutokana na kukiuka miongozo ya uendeshaji wa Mitihani ya Taifa. Kituo hicho kitaendelea kufungwa hadi NECTA itakapojiridhisha kuwa kinafaa kuendesha mitihani kwa usalama.

Your browser is not able to display this video.
Katibu Mtendaji Prof. Said A. Mohamed ameongeza kuwa ufaulu wa watahiniwa wa shule umefikia 99.92%, huku ukibaki juu ya 99% kwa miaka minne mfululizo. Amesema pia idadi ya waliopata Division One imeongezeka hadi 54.1% kutoka 48.6% mwaka 2025.

Your browser is not able to display this video.
 
Mwenye uelewa anisaidie ni vipi mtu anaweza baini kuwa hiki kitu kimeandikwa kwa AI au ni kwa kuwaza tu au Kuna vifaa vya kubaini AI generated contents
Tumia chatgpt iulize maswali utagundua utofauti katika namna inavyoandika, yani kiufupi AI zinajibu kiufundi sana na mpangilio sahihi wa maneno!. Chengine nafikiri waligundua mfanano wa majibu kwa watu kadhaa, yani mfano watu kumi muulize swali moja chatgpt itawajibu hivyohivyo so nawewe ukikopi hivyohivyo basi mfanano lazima uonekane tu!.
 
Mwenye uelewa anisaidie ni vipi mtu anaweza baini kuwa hiki kitu kimeandikwa kwa AI au ni kwa kuwaza tu au Kuna vifaa vya kubaini AI generated contents
Ukicopy na kupaste ni rahisi kujulikana

1. Msahihishaji anaweza weka swali kwenye AI na kuona ufanano wa jibu

2. Ai usipotumia prompt majibu yake yanaonesha kabisa hii ni AI the way inavyoelezea kwa maelezo mengi kupita kiasi yasiyo na ulazima

3. Zipo detectors sema ni kwa kudetect wa juu ambao ni layman

Kwa wazoefu ngumu mno kudetect
 
Nachojiuliza wametumiaje chatGpt kujibia maswali hali ya kwamba watu hawaruhusiwi kutumia simu kwenye chumba cha mtihani.
 
Ina maana waliingia na simu darasani, ama ilikuwaje?
 
mkuu inabidi nipate elimu kutoka kwako. hapo kutumia prompt imekaaje hapo?
 
Nachojiuliza wametumiaje chatGpt kujibia maswali hali ya kwamba watu hawaruhusiwi kutumia simu kwenye chumba cha mtihani.
Ina maana waliingia na simu darasani, ama ilikuwaje?
Nilipoona hii taarifa nilijiuliza hili swali pia!, labda waliingia na smart watch!, itabidi waje watupe majibu ya uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ