Kidini Israel na Trump wapo sahihi, kisheria Wapalestina wapo sahihi

Kidini Israel na Trump wapo sahihi, kisheria Wapalestina wapo sahihi

All in all, huyo YESU WA BIBLIA NI TOFAUTI NA ISA WA QURAN

Unanukuu vifungu , hujui hata maana yake
lakin kaka hata kama kuna utata wa maandko kwenye maneno hayo utata uko WAP hayo maneno hamyasom ndo maana hata mkinikuliwa munashangaa na kuishia kusema hamjui maana ya maandko hayo,na ndo majibu hayo hayo munayopewa na wataalam eenu bila kutafar
Kuna watu wengi, wengine ni wasomi kabisa lkn naona bado hawajui kuwa wayahudi sio wa kristo, kuna watu humu wana toa comments zao kama kishabiki hivi wakifurahia wayahudi kuitwaa Jerusalem wakidhani wayahudi ni wa kristo.
 
Umeona shetani ni mbaya sana jamaa kafungiwa kwenye kibuyu kangangana kunukuu mistari kibao eti anajenga hoja.

Cha ajabu sasa kahepa ule mstari maarufu. "Mimi ndimi njia kweli na uzima mtu haji kwa baba yangu ila kwa njia yangu" Hakuna njia nyingine ya kufika kwa Mungu ni kujidanganya na upotevu mkuu eti kuna mbadala wa Bwana Yesu kama wataka ukifa uuone ufalme wa Mungu, ndio hakuna mbadala.
kila mjumbe anapotumwa kulingania watu in lazima atamuhusisha mungu aliyemtuma na mwenyewe aliyetumwa hali hiyo IPO kwa mitume wot na kwa nyakat zote za ibrahima(a.s) musa(a.s) ISSA(s.s) na Muhammad(a.s)
 
Wewe unazidi kutoa ushahidi Kuwait waliopita ni waislamu,na uislamu ulianza kabla ya Mtume Muhammad,ndio wakavaa kanzu.Wasiokuwa wafuata hao mitume iliyopita,ndio hawavai kanzu, kwa sababu wanajuwa wazi na ndivyo ilivyo ,hilo ni vazi la waislamu.Hutkuta Trump,hata siku moja avyae kanzu, wala Netanyau avyae kanzu..
Umenisaidia sana kutoa ndani ya biblia,kutzidi kutujulisha kama manabii waliyopita walikuwa waislamu,na uislamu ulikuwako kabla ya Mtume Muhammad.
acha pumba zako na wewe
 
Kuna vitu pia sivielewi vizuri sana kuhusu hizi Dini. Kwa mfano marufuku ya trump ilivyotoka ya kuzuia baadhi ya mataifa ya kiislam. Mataifa mengi ya kiislam yalipinga sana. Ss unajiuliza kwn pale maka kuna u lazima gani kwenda ktk nchi ya unayemuita kafiri? Tena unasema anakugombanisha kwa makusudi ili akuuzie silaha ...si kheri usiende na ww mpge marufuku asije kwako
US ni ya wahindi wekundu mkuu, kwa hiyo yy trump hana uhalali wa kuwazuia watu wengine kwani naye pale US sio kwao/kwake
 
Umeishiwa hoja,hoja inapingwa kwa hoja,sio maneno matupu.
uislam ulikuwepo kivipi wakati mnasema uislam aliuanzisha mohammed bin abdullah
na mohamed alizaliwa karne ya sita baada ya anayeitwa yesu kuzaliwa!!!!
 
GHAFLA UMEKUWA KIPOFU ?????

ILE POST YA [HASHTAG]#184[/HASHTAG] HUKUIONA ???




Mwislamu wa kwanza duniani si Muhammad (SAW), bali ni Ibrahimu, aliyejisalimisha kikamilifu kwa Allah.

Lakini Uislamu ukiwa ni njia ya maisha umefunuliwa kwa Mitume mingine iliyomtangulia Ibrahimu, kama vile Adamu na Nuhu. Kwa hiyo, Uislamu ndiyo njia ya maisha ya wanadamu wote.

Swali :

Vipi Ibrahimu atakuwa Mwislamu?

Majibu:

Soma Mwanzo 11:31

. "Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko."

Kwa hiyo, Ibrahimu alizaliwa Uru wa Wakaldayo na hawezi kuwa Myahudi. Kwanza kwa sababu Uru wa Wakaldayo ilikuwa Mesopotamia, ambako kwa sasa ni sehemu ya Iraq.

Kwa hiyo, Yeye alikuwa ni Mwarabu zaidi kuliko Myahudi.

Pili neno “Uyahudi” limekuja baada ya kuishi kwa Yudah, mjukuu mkubwa wa Ibrahimu.

Soma zaidi, Mwanzo 12:4-5 Naye Abramu alikuwa ni mtu wa miaka sabini na mitano alipotoka Harani... nao wakaingia katika nchi ya Kanaani."

Kwa hiyo Ibrahimu alihamia Kanaani akiwa na miaka sabini na mitano na Biblia kwa uwazi inataja kuwa, Ibrahimu alikuwa huko akiwa ni mgeni. Mwanzo 17:8

"Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kanaani, kuwa milki ya milele, nami nitakuwa Mungu wao."

Sasa soma Mwanzo 14:13.

“Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania;...”

Vipi unamwita Ibrahimu Myahudi kama Biblia yenyewe inamwita Mwebrania jina ambalo maana yake ni mtu kutokea upande mwingine wa mto Euphrates.

Pia linamaanisha kufungamana na Eber, mjukuu wa Shem.

Sasa soma katika Mwanzo 32:28 kile kilichotokea kwa jina Yakobo baada ya mieleka na Malaika.

"Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe ukashinda."

Kwa hiyo Ibrahimu alikuwa ni Mwebrania. Na wajukuu wa yakobo walikuwa ni Waisraeli yakiwemo makabila kumi na mawili.

Yuda alipewa jina la utani la "Yahudi" kwa hiyo, wajukuu wa Yuda peke yao ndiyo waliokuwa Wayahudi kwa asili.

Na ili kumjua ni nani hasa ndiyo alikuwa Musa, soma Kutoka 6:16-20.

"Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, sawasawa na vizazi vyao; Gershoni, na Kohath, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia na thelathini na saba. Wana wa Gershoni; ni Lbni, na Shimei, sawasawa na jamaa zao. Na wana wa kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia na thelathini na mitatu. Na wana wa Merari; ni Mali, na Mushi. Hizi ni jamaa za hao Walawi sawasawa na vizazi vyao. Huyo Amramu akamwona Yokebedi ndugu ya baba yake; naye akamzalia Haruni, na Musa..."

Kwa hiyo, Musa hakuwa Myahudi kwa sababu hakuwa mjukuu wa Yuda lakini ni wa Lawi.

Musa alipewa Torati (sheria) kwa wana wa Israeli.

Swali : Unalifasiri vipi jambo hilo?

Majibu:

Kwa kuwa sisi tunatumia Qurani kama ni kipimo. Unaweza kuifafanua Biblia na kusahihisha maoni ya Kiyahudi na Kikristo kwa Muktadha wa Qurani.

Qurani ni kitabu kilichofunuliwa mwisho, hakijaharibiwa wala kughushiwa. Yaliyo ndani yake Allah ameyadhamini, katika Sura 2:2: "Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake;....." pia katika Sura ya 15:9 "Hakika Sisi ndio tulioteremsha mauidha haya (hii Qurani); na hakika Sisi ndio tutakayoyalinda."

Aya hii ni changamoto kwa wanadamu.

Ni ukweli wa wazi kuwa zaidi ya miaka elfu moja na mia nne imeshapita hakuna hata herufi moja ya Qurani hii iliyobadilishwa ingawa makafiri wamejaribu kwa kila liwezekanalo kuibadilisha, lakini wameshindwa kwa unyonge katika juhudi zao hizo. Kama ilivyotajwa katika aya hii tukufu:

"Hakika Sisi ndio tutakayoyalinda" na Allah, ameshailinda. Kinyume chake, vitabu vitakatifu vingine vyote (Torati, Zaburi, Injili, nk) vimeshaghushiwa kwa njia ya kuongeza, kufuta au kubadilisha asili yake.

Swali : Qurani inasema nini juu ya Ibrahimu na Musa linalothibitishwa na Biblia?

Katika Sura 3:65: “Enyi watu mliopewa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahimu, na hali Taurati na Injili havikuteremshwa ila baada yake? Basi je, hamfahamu?”

Na katika Sura 3:67: “Ibrahimu hakuwa Myahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu, mtii; wala hakuwa katika washirikina.”

Katika Sura 2:140: “Mnasema (nyinyi Mayahudi na Manasara) kuwa Ibrahimu na Ismaili na Is-haqa na Yaaqubu na kizazi (chake) walikuwa Mayahudi (kama nyinyi)? Sema: “Je, nyinyi mnajua zaidi au Mwenyezi Mungu? Na ni nina dhalimu mkubwa kuliko yule afichae ushahidi alionao utokao kwa Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na hayo mnayoyafanya.”

Shukrani mkuu!
 
Naam, bila shaka, jina “Allah” linaonekana ni geni kwa wasiokuwa Waislamu, lakini jina hili limeshatumiwa na Mitume yote tangu Adamu mpaka Muhammad (AS).

Nalo ni ufupisho wa maneno mawili ya Kiarabu; Al – Ilah, yaani Mwenyezi Mungu.

Kwa kuiondosha herufi "I" utapata neno Allah.

Kwa mujibu wa nafasi yake katika tungo (sentesi) ya Kiarabu jina hilo linaweza kuwa na umbo la "Allaha" ambalo ni karibu na jina la Muumba kwa Kiebrania yaani “Eloha.”

Lakini Wayahudi wanatumia kimakosa umbo la wingi “Elohim,” linaloashiria zaidi ya Mungu Mmoja.

Neno "Allaha" lina matamshi yanayokaribiana na neno la Kiarama linalojulisha Mungu lugha iliyotumiwa na Yesu, kwa kulitaja "Alaha" (Tazama Insaiklopidia Britannica 1980 chini ya neno “Allah” na “Elohim”).

Kwa hiyo, wakati jina “Allah” ni geni kwa wasio Waislamu, lakini si geni kwa Mitume yote tangu Adamu mpaka Muhammad, (AS) kama walivyotangaza misingi ile ile ya Uislamu (utiifu kamilifu) na neno “Allah” linamaanisha jina la Mungu Aliye Hai.

Jina hilo halina wingi au ujinsia, kwa hiyo hakuna kitu kama “Allahs-Miungu,” au “Allah,” wa kiume au wa kike, kama ilivyo, katika lugha ya Kingereza yenye miungu ya kiume na kike (Gods or Goddess).

Pia ni jambo la kuchanganya kutumia neno God, kwa vile Wakristo wengi wanaozungumza Kingereza wanamzingatia Yesu kuwa ni Mungu.


Hata neno “Muumba” pia linachanganya, kwa kuwa Wakristo wanashikilia kuwa Yesu ameumba dunia.



Si tu jina “Allah”, ndilo geni, lakini pia njia wanazozitumia Waislamu kumwabudu Allah wakiwa na udhu, unyenyekevu, kurukuu, kusujudu na kufunga, nazo ni ngeni kwa wasio Waislamu, lakini si ngeni kwa mitume yote. Wakati udhu (kuosha uso, mikono, miguu, na kupaka maji kicwani), kabla ya kusali, haufanywi na Wakristo wa leo lakini jambo hilo lilifanywa na Waislamu na mitume iliyotangulia, kama inavyoonekana katika vifungu vya Biblia vifuatavyo:

Kutoka 40:31-32 "Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake; hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu, walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa".

Ingawa Paulo amefanya mabadiliko mengi katika mafundisho ya Yesu (AS), lakini alikuwa mwaminifu katika kuuheshimu udhu, kama inavyoonekana katika Matendo 21:26.

"Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu...."

Na 1 Wakorinto 11:5-6, 13: "Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa. Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au konyolewa, na afunikwe."

Wanawake wa Kiislamu wanatekeleza swala zao huku wamefunika vichwa vyao. Amua wewe mwenyewe; Je, ni vizuri kwa mwanamke aswali mbele ya Mungu huku kichwa chake kimefunikwa au hakijafunikwa?

Waislamu wanaabudu kwa unyenyekevu, kurukuu, kusujudu na bila ya viatu kama ilivyofanywa na Mitume iliyotanguli. Zaburi 95:6


"Njoni, tuabudu, tusujudu, tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.” Yoshua 5:14

"Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la BWANA. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake?"

1 Wafalme 18:42

"Basi Ahabu akainuka ili ale na kunywa, Naye Eliya akapanda juu mpaka kilele cha Karmeli; akasujudu kifudifudi, akainama uso mpaka magotini."

Hesabu 20:6 "Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa BWANA ukawatokea."

Mwanzo 17: 3 "Abramu akaanguka kifudifudi Mungu akamwambia akasema."

Kutoka 3:5 "Naye akasema, Usikarabie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu."

Na Matendo 7:33 "Bwana akamwambia, vua viatu miguuni mwako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu.
Mbona unaandika utumbo mtupu
 
Maandiko ya Qur-an yanaonesha wazi kuwa kabla ya hapo hata Muhammad mwenyewe alikuwa akifuata kawaida za ibada alizofundishwa na Wayahudi.
-Wayahudi walikuwa na desturi ya kusali kwa kuangalia Yerusalemu, kawaida hii ndiyo iliyotawala maisha ya Muhammad kwa takriban zaidi ya mwaka mmoja na nusu naye alikuwa akiabudu kwa kuangalia Yerusalemu.
(Qur-an 2:144 fafanuzi uk 34)

Tukio la mwaka 610 BK ndilo lililoleta mabadiliko makubwa kwa Muhammad, mwaka huo ndio ambao Muhammad
alipokea mafunuo yake mapya katika mapango ya Jabal hilaa tofauti za kimafundisho, mwenendo, n.k zilianza
kuonekana katika maisha ya
Muhammad mara tu baada ya kuanza kupokea mafunuo hayo. (maisha ya Muhamadi uk 16 shekhe Farsy).


-Hilo lilimfanya Muhammad
kuanza kupingwa na wayahudi hao, Haswa sababu kuu ni pale Muhammad alipoanza kupinga mafundisho waliyompa kama vile., Kutotia mkazo wa Kiibada katika jengo lenye asili ya upagani Al-Kaaba. Qur-an 22:29 [27:9], na Kuanza tabia ya kutangaza imani mpya ya uislam na kuwa na mafundisho yaliyo onekana
kutofautiana na yale ya kibiblia(TANAKH).
Kutokana na mafunuo hayo mapya hoja kuu ya Wayahudi ilikuwa ni juu ya mashaka waliyonayo, kuwa mafunuo haya ya Muhammadihayakuwa ya kweli, Aya ifuatayo ya Qur-an inonyesha hilo.

Qur-an Al-Baarah 2:97 Ufafanuzi uk 24 aya 97 hapa wayahudi wanampinga Malaika Jibril amhaye ndiye aliyeleta mafunuo hayo kwa Muhammad.
Na Ibada ya ijumaa inatokana na ugomvi wa Wayahudi na Muhammad.


-Kutokana na hali hiyo mahusiano baina ya Muhammad na Wayahudi
yaliharibika, Fuatilia katika aya
zifuatazo:

Qur-an 5_:82 Maadui wa Uislam ni Wayahudi
Qur-an 2:I04 [Ufafanuzi] Wayuhudi. ,walihitirafiana na Muhammad na kurushiana maneno.

Tangu hapo Muhammad hakupenda kamwe kuwiana na kile wanachofanya wayahudi katika mifumo ya kidini, na
ndipo anaitangaza rasmi siku ya ljumaa kama siku ya sala katika Ummah wa Kiislam wakati huo akiwa
Yathrib (madina),ili apingane na WAYAHUDI, kumbuka awali alifata mila zao na alisali nao siku ya sabato(JUMAMOSI).

KUANZIA HAPO MUHAMMAD AKAPANDIKIZA CHUKI KWA WAFUASI WAKE DHIDI YA MYAHUDI, Quran imejaa Aya lukuki za kuwachukia wayahudi hasa.

Mungu ibariki ISRAEL ,Mungu wabariki Wayahudi


BIBLIA TAKATIFU INASEMA SIKU ZA MWISHO,WAYAHUDI WATAUTAMBUA UKRISTO NA KUUFATA,
 
UISLAMU UMEKUJA NA MUDY, LKN KUNA WATU WANADANGANYWA NA KUDANGANYIKA, WHY?

Quran 39: 12 Suratul Zumar (Makundi / Vikosi)
"Na pia nimeamrishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha (kwa mwenyezi Mungu)"

Quran 6: 14 Suratul Al- An'am (Wanyama)
Sema "je nifanye mola (wangu) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, (Ambaye ndiye) muumba wa mbingu na ardhi" naye hulisha wala halishwi" sema hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu na (nikaambiwa). usiwe miongoni mwa wanaomshirikisha (Mwenyezi Mungu).

Katika ufafanuzi wa aya ya 19-20, katika Suratul Yusuf 12:20 kuna maneno haya--
Unaona kuuzana kulikuwako zaidi yamiaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo nabii Muhammad. Kisha wakausingizia uislamu kuwa ndio uliokuja na kuuza watu.

Kadiri ya aya hizi zote tunaona ya kuwa dini ya kiislamu ilianzishwa rasmi hapa duniani Ramadhan siku ya Jumatatu mwezi 17 sawasawa na Tarehe 27 December mwaka 610 Baada ya Kristo (B.K), na mtu aitwae Muhammad Bin Abdalah Bin Abd-Muttalib Bin Hashim Bin Abd Manafu Bin Kusay. Mama yake aliitwa Amina Bint Wahab.
 
UISLAMU UMEKUJA NA MUDY, LKN KUNA WATU WANADANGANYWA NA KUDANGANYIKA, WHY?

Quran 39: 12 Suratul Zumar (Makundi / Vikosi)
"Na pia nimeamrishwa niwe wa kwanza wa (viumbe) wanaojisalimisha (kwa mwenyezi Mungu)"

Quran 6: 14 Suratul Al- An'am (Wanyama)
Sema "je nifanye mola (wangu) asiyekuwa Mwenyezi Mungu, (Ambaye ndiye) muumba wa mbingu na ardhi" naye hulisha wala halishwi" sema hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu na (nikaambiwa). usiwe miongoni mwa wanaomshirikisha (Mwenyezi Mungu).

Katika ufafanuzi wa aya ya 19-20, katika Suratul Yusuf 12:20 kuna maneno haya--
Unaona kuuzana kulikuwako zaidi yamiaka 4000 kabla ya kuja dini ya kiislamu aliyokuja nayo nabii Muhammad. Kisha wakausingizia uislamu kuwa ndio uliokuja na kuuza watu.

Kadiri ya aya hizi zote tunaona ya kuwa dini ya kiislamu ilianzishwa rasmi hapa duniani Ramadhan siku ya Jumatatu mwezi 17 sawasawa na Tarehe 27 December mwaka 610 Baada ya Kristo (B.K), na mtu aitwae Muhammad Bin Abdalah Bin Abd-Muttalib Bin Hashim Bin Abd Manafu Bin Kusay. Mama yake aliitwa Amina Bint Wahab.

Ndiyo mafundisho ya Padri wako baada ya kumpa minofu
 
Maandiko ya Qur-an yanaonesha wazi kuwa kabla ya hapo hata Muhammad mwenyewe alikuwa akifuata kawaida za ibada alizofundishwa na Wayahudi.
-Wayahudi walikuwa na desturi ya kusali kwa kuangalia Yerusalemu, kawaida hii ndiyo iliyotawala maisha ya Muhammad kwa takriban zaidi ya mwaka mmoja na nusu naye alikuwa akiabudu kwa kuangalia Yerusalemu.
(Qur-an 2:144 fafanuzi uk 34)

Tukio la mwaka 610 BK ndilo lililoleta mabadiliko makubwa kwa Muhammad, mwaka huo ndio ambao Muhammad
alipokea mafunuo yake mapya katika mapango ya Jabal hilaa tofauti za kimafundisho, mwenendo, n.k zilianza
kuonekana katika maisha ya
Muhammad mara tu baada ya kuanza kupokea mafunuo hayo. (maisha ya Muhamadi uk 16 shekhe Farsy).


-Hilo lilimfanya Muhammad
kuanza kupingwa na wayahudi hao, Haswa sababu kuu ni pale Muhammad alipoanza kupinga mafundisho waliyompa kama vile., Kutotia mkazo wa Kiibada katika jengo lenye asili ya upagani Al-Kaaba. Qur-an 22:29 [27:9], na Kuanza tabia ya kutangaza imani mpya ya uislam na kuwa na mafundisho yaliyo onekana
kutofautiana na yale ya kibiblia(TANAKH).
Kutokana na mafunuo hayo mapya hoja kuu ya Wayahudi ilikuwa ni juu ya mashaka waliyonayo, kuwa mafunuo haya ya Muhammadihayakuwa ya kweli, Aya ifuatayo ya Qur-an inonyesha hilo.

Qur-an Al-Baarah 2:97 Ufafanuzi uk 24 aya 97 hapa wayahudi wanampinga Malaika Jibril amhaye ndiye aliyeleta mafunuo hayo kwa Muhammad.
Na Ibada ya ijumaa inatokana na ugomvi wa Wayahudi na Muhammad.


-Kutokana na hali hiyo mahusiano baina ya Muhammad na Wayahudi
yaliharibika, Fuatilia katika aya
zifuatazo:

Qur-an 5_:82 Maadui wa Uislam ni Wayahudi
Qur-an 2:I04 [Ufafanuzi] Wayuhudi. ,walihitirafiana na Muhammad na kurushiana maneno.

Tangu hapo Muhammad hakupenda kamwe kuwiana na kile wanachofanya wayahudi katika mifumo ya kidini, na
ndipo anaitangaza rasmi siku ya ljumaa kama siku ya sala katika Ummah wa Kiislam wakati huo akiwa
Yathrib (madina),ili apingane na WAYAHUDI, kumbuka awali alifata mila zao na alisali nao siku ya sabato(JUMAMOSI).

KUANZIA HAPO MUHAMMAD AKAPANDIKIZA CHUKI KWA WAFUASI WAKE DHIDI YA MYAHUDI, Quran imejaa Aya lukuki za kuwachukia wayahudi hasa.

Mungu ibariki ISRAEL ,Mungu wabariki Wayahudi


BIBLIA TAKATIFU INASEMA SIKU ZA MWISHO,WAYAHUDI WATAUTAMBUA UKRISTO NA KUUFATA,

Ndiyo mafundisho ya Padri wako hayo?? Hivi hata huelewi wayahudi wakifuata dini gani??unaleta uharo wa Padri wako
 
Unatumia references gani kuipa nguvu argument yako.Kama hujuwi basi kaa kimya au uliza utaambiwa.Qur'an haijaacha kitu kuhusu habari za Israel na habari za Nabii Ibrahim(a.s) kuwa alikuwa ni muislam hata nabii yakobo(a.s).
Nabii Ibrahim(a.s) ndiye aliyejenga msikiti wa alsqa na mwanaye Ismail.Quran imeeleza hoja zote haijaacha kitu.
Bible sio history,Ni fiction, nyi vipi????
 
Usiandike mistari mingi haisidii lolote andika na ile kuhusu Bwana Yesu na mwanamke msamaria pale kisimani ilikuwaje wakachangamana. Uko mujiza wa Bwana Yesu wa Kulisha maelfu kadhaa mikate na samaki Aliufanya mara mbili wajua ilikuwa wapi na wapi? Akimaanisha nini?
Miujiza gani,ngano and fairly tells!!!!! Then unaambiwa mtu akaruka akenda mbinguni, unaamini.....na namsubiri arudi imepita miaka 2000...
 
Wewe wa ajabu kweli maneno mengi na nukuu nyingi hujui hata kuwa Yakobo/Israel ni mjukuu wa Ibrahimu. Israel ni jina alilopewa na Mungu.

Bado tuko twasuburi ulete familiy tree ya kumuunganisha Mtume Muhamad SAW na Ismail wa Ibrahim acha hizi longolongo.
Ibrahim who never existed???? Ndio ujinga ulipoanzia
 
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).

Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.

Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.

Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.

Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu.

Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.


Makala hii ni kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya 1, Uk 10.

0715865544/0755865544

View attachment 649590
Asante kwa mada mzuri, yet uongo huu ndio unaoitawala dunia
 
Back
Top Bottom