Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Haya Gavana/mwl hapo post 171:
Umetaja/Nukuu Kumbukumbu la taurati 18.
Hebu anzia mstari wa 16-22. (The Promise to Send a Prophet).
Mussa alikuwa anaongea na Wana wa Israel akiwaeleza kuhusu kuchukua tahadhari juu ya nchi ya ahadi wanayo iendea ni maagizo ya Musa aliyopewa na Mungu hapo mlima Sanai, pamoja na mambo mengine ya jinsi ya kumjua nabii/prophet aliyetumwa na Mungu kwao. Ismail si kati ya wana wa uzao wa Yakobo/Israel. Uongo mwengine huu mweupe pee.
Kwa muktadha huu labda mwl Gavana tusaidie kuweka family tree ya Ismael inayo muunganisha na Bwana Mtume SAW.
Bishara yenye nguvu imo katika Mathayo 21:33- 40.
Hii ni mojawapo ya methali za Yesu ambamo ndani yake mna utabiri wa kufika Mtume Mtukufu. Bishara yenyewe ni hii:-
“Kulikuwa na mtu mwenye nyumba naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara akapangisha wakulima akasafiri.
Wakati wa matunda ulipokuwa karibu akawatuma watumishi wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake. Wale wakulima wakawakamata watumishi wake, huyu wakampiga na huyu wakamwua, na huyu wakampiga kwa mawe.
Akawatuma tena watumishi wengi kuliko wa kwanza, ikawa tena vile vile. Mwisho akamtuma mwanawe kwao, akisema watamsitahi mwanangu. “
Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi haya na tumwue, tuutwae urithi wake, Wakamkamata wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamwua.
Basi atakapokuja yule bwana wa shamba la mizabibu atawatendaje wale wakulima? Wakamwambia, Atawaangamiza vibaya wale wabaya, na shamba la mizabibu atawapangisha wakulima wengine, watakaomlipa matunda kwa wakati wake.
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.
Kwa sababu hiyo nawambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake. naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika, na yeyote ambaye litamwangukia litamsaga tikitiki.
Wakuu wa makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano yake, walitambua ya kuwa anawanenea wao. Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii,”
Katika methali hii iliyo nzuri Yesu ameeleza historia ya mfululizo wa kuja kwa Mitume.
Ni wazi hapa kwamba shamba la mizabibu ndiyo ulimwengu, wakulima maana yake ni walimwengu kwa jumla, matukio ambayo bwana wa shamba alitaka kuvuna ndiyo wema, uaminifu na ucha-Mungu, watumishi ndiyo manabii wa Mungu waliokuja duniani mmoja baada ya mwingine; mwana ndiye Yesu aliyekuja baada ya mfululizo wa manabii wengi. Mwana huyu aliadhibiwa na wakulima. Baada ya kusema mambo haya, Yesu ameendelea kunena juu ya “Jiwe” walilolikataa waashi, hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.”
Jiwe lililokataliwa ndiyo wazao wa Ismaili, waliodharauliwa na wana wa Isihaka.
Kulingana na bishara hii ya Yesu, mtu mmoja angekuwa jiwe kuu la pembeni - “Muhuri wa Manabii,” katika lugha mashuhuri ya Qur'an tukufu - hangekuwa nabii wa cheo cha chini, bali mfano wa manabii atakayeleta Sheria ya mwisho na kamili toka kwa Mwenyezi Mungu.
Kuinuliwa kwa Nabii toka katika nyumba ya Ismaili lilionekana jambo geni, kwani wengi katika mfululizo wa manabii wa hapo mbele walitoka katika nyumba ya Isihaka (Israel).
Lakini Yesu anasisitiza ya kuwa Mwenyezi Mungu ataondoa ufalme wake kutoka nyumba ya Israeli na kuwapa wana wa Ismaili, watakaotoa matunda yake; yaani wana wa Ismaili ndiyo watakaokuwa taifa litakalodumisha uchaMungu na ibada ya Mwenyezi Mungu duniani.
Kila mtu anaweza kuona hapa ya kuwa hapana mtu yeyote aliyedai utume baada ya Yesu, na akafanikiwa, isipokuwa Mtume mtukufu Muhammad s.a.w.
Ni yeye ambaye mafundisho yake yalihitilafiana na dini ya Mayahudi na akavunja kabisa nguvu za dini hiyo. Ni yeye ambaye taifa lake lilidharauliwa na kuchukiwa.
Nabii Muhammad s.a.w. ndiye mjumbe wa Mungu wa pekee aliyejaaliwa kushinda maadui zake wote katika uhai wake, hivyo ni yeye tu ambaye ndiye lile jiwe ambalo yeyote aliyeanguka juu yake alivunjika-vunjika na yeyote liliyemwangukia likamsaga tikitiki.
Wakristo wamekosea sana kwa kudhani Yesu ndiye “Jiwe” linalotajwa hapa. Lakini wanasahau ya kuwa Yesu alikuwa Mwisraeli, hali yeye amesema “Ufalme wa Mungu utaondolewa kutoka kwa Waisraeli na kupewa taifa jingine,” yaani Waismaili. Isitoshe, ikiwa jiwe ni Yesu, basi ingefaa kufahamishwa aliwasaga akina nani tikitiki