Acha kudanganya watu mkuu, Yesu wa biblia ni tofauti kabisa na Isa wa quran. ,
Wa biblia alitabiriwa na manabii kama kina isaya, ezekiel ,daud kuwa ataitwa Mungu mkuu,
Ila wa quran kwanza hata hakusurubiwa, yaan in short ni watu wawil tofauti kabisa.
Kuhusu muhamad , huyu ana historia yake ,awali alikuwa anasali kuelekea yerusalemu, akifata din ya wayahud, baadae aliposema amepewa utume, wayahud walitaka athibitishe, hapo ndipo ugomvi ulianza ,na mpaka quran ina aya za kuwachukia wayahudi
KWA UFUPI , UISLAMU KAJA NAO MUHAMAD ,
HIVI Wewe unaelewa zaidi HALI MBILI NDANI YA HUYO YESU, KULIKO YESU MWENYEWE ???
TUKUSIKILIZE WEWE AU YESU ??
Kile anachokisema Yesu (AS) juu yake na Mungu
Yesu Kristo (AS) kamwe hajataja juu ya Utatu wala hakuwa macho kuwa kuna Mungu wa Utatu.
Ufahamu wake ulikuwa ni ule ule kama wa wale mitume Waisraeli wa mwanzo, waliohubiri Upweke wa Mungu.
"Yesu akamjibu, Ya kwanza ndiyo hii, Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja; nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote." Marko 12:29-30
"...Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake." Mathayo 4:10 na Luka 4:8. Yesu (AS) anasema kuwa ni Mungu peke yake ndio wa kuabudiwa.
"...Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja.." Marko 12:29 Yesu (AS) anathibitisha upweke wa Mungu.
"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliyembinguni." (Mathayo 7:21)
Ni wazi kuwa Mungu alikuwa Mbinguni na Yesu (AS) alikuwepo ardhini.
Kwa hiyo vipi watakuwa wameungana katika mwili mmoja?
Imani ya Kikristo inaeleza kuwa 'Nafsi Tatu' zimeungana katika mwili mmoja (watatu ndani ya mmoja).
Itawezekana vipi kwa waunda Utatu wote wawe Miungu kamili wakati kila mmoja wao anaunda moja ya tatu ya Uungu?
"Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma."
Yohana 17:3.
Hapa, Yesu (AS) anachora mstari kati ya Mungu na yeye mwenyewe.
Ili ufikie uzima wa milele ni kujua Mungu wa kweli na Yesu (AS) kuwa ametumwa akiwa ni Mjumbe wa Mungu tu.
Yesu (AS) anasema:
"Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu." Marko 10:18.
Yesu (AS) anatetea kuwa hakuna mwema isipokuwa Mungu, na hilo linamtenga Mungu na Yesu.
"Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake." Mathayo 24:36
na "Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba." Marko 13:32
Yesu (AS) anakiri kuwa elimu yake ina mipaka finyu kinyume na Mungu, ambaye ni mjuzi wa kila kitu. Pia, hukumu ni ya Mungu peke yake anayetunza siri zote Yeye mwenyewe.
"Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile." Yohana 5:19
Hapa, Yesu (AS) anakiri kumtegemea Mungu.
"Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama niskiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka." Yohana 5:30
"Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka." Yohana 6:38
"Basi Yesu akawajibu, akasema, Mafunzo yangu si yangu mimi, ila ni yake yeye aliyenipeleka." Yohana 7:16
"...na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu, ila kama Baba alivyonifundisha ndivyo ninenavyo." Yohana 8:28
Yesu (AS) anaweka wazi sana kuwa Yeye ana upungufu wa nguvu takatifu. Yeye mwenyewe hawezi kufanya lolote kwa kuwa Mungu pekee ndiye chanzo cha nguvu na mamlaka.
"Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu ambaye nimewaambia iliyo kweli, niliyoisikia kwa Mungu..." Yohana 8:40
Yesu (AS) ameungama kuwa Yeye alikuwa ni Mjumbe anayetimiza kazi aliyoamrishwa na Mkuu.
Ziada, Mtume Yesu (AS) anasema: "Yesu akamwambia, usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Yohana 20:17
Aya hii inatia nanga (inaumaliza) UTATU na IMANI YA MUNGU KUWA NA MWILI.
Inaonesha mahusianao ya Yesu (AS) na Mungu kuwa ni kama ya binadamu yoyote yule yaani kusali na kuomba msaada toka Kwake.