Kidini Israel na Trump wapo sahihi, kisheria Wapalestina wapo sahihi

Kidini Israel na Trump wapo sahihi, kisheria Wapalestina wapo sahihi

Suggestion yangu hawa watu waachwe tu, mmoja achukue ardhi au wakubaliane wachukue wote.
Kwa sababu ni ujinga kutumia dini ku-justify kugombania ardhi.
Kuna sehemu nyingi ina migogoro ya maeneo kwa kila mtu kuwa na hoja zake.
Wengine wanakubaliana na matokeo, wengine hutafuta suluhu, na wengine huendelea kupigana mpaka the last ones standing.
Huwezi ukadai walipewa na Mungu tu. Hiyo haitoshi, maana throughout history watu wamekuwa wakipinduana kuchukua ardhi.
Em tutafute a common ground ku-solve hili suala.
Kila mtu ana makazi pale, sasa kwa nini tunaona ni bora mmoja aondoke... Illogical.
Kuondoka kwa hao watu MUNGU alikusema zaman kuwa waondosheni msiwaache hata mmoja kwa hao watakuwa mwiba kwenu(mbigiri)lkn waliwaacha na wengine kuwaoa kama kina delira matokeo yake ndo haya,wapalestina si mahala pao pale
 
Wote kidini ni Waongo sababu trump sio bloodline ya yacob na hao akina netanyau pia sio bloodline ya yacob. Bali ni masinagogi ya shetani.
 
Kilete hapa hicho kitabu cha taurati na injili ,unaonesha mnacho ,

Ukileta ni tag
Biblia nilikuletea mimi.Tafuta vitabu usome,na kama hukipati wakati kimetwaja kipo, jiulize kuna nini mbona viongozi wangu ,Wa kikiristo hao walioko makao makuu,hawatupi vitabu hivi,kumefichwa nini?
 
Wanasema israel ni kitovu cha dini tatu uyahudi, ukristo na uislam, kwani uislam ulianzia israel?
ukitaja dini basis kila eneo ktk dunia hii itakua no milki ya din husika coz dunia yote inamilikiwa na mungu hvyo sehem zote za dunia tulitakiwa kuish kutokana na mfumo alioutaka mungu kwa hyo uislaam kutoanzia huko haimaanish kuwa uislaam hauhusiki hapo uislaam umehusika kutokana na histolia iliyotangulia ya minabii ya mungu kupitia Quran ambayo imewataja akina mnabii mussa ibaraha issa-yesu na wengne weng pamoja na vitabu vyao
Madai ya Waisraeli yanaanzia katika misingi ya kidini ambapo katika Biblia (kitabu kitakatifu wa Wakristu na Wayahudi), Kitabu cha Kwanza cha Nabii Musa kiitwacho Mwanzo (sura ya 12), kinaonesha jinsi Ibrahim alivyoitwa na Mwenyezi Mungu ili kumtumikia. Eneo hilo la Palestina ambalo zamani lilijulikana kama Kaanani, ndipo chimbuko la dini tatu kuu zenye msingi wa Ibrahim zilibuka. Dini hizo ni Uyahudi, Ukristu na baadaye Uislamu. Dini ya Wayahudi yenye misingi ya Biblia ya Agano la Kale, likianza na vitabu vitano vya Musa: Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi na Kumbukumbu la Torati. Ukristu ukianzia misingi kwenye Agano la Kale hadi Agano Jipya na Uislamu ukishika vitabu vinne vya Tourat ya Nabii Musa (a.s), Zabur ya Nabii Dawood (a.s), Injili ya Issa bin Mariam (a.s.) au Yesu na Kurani ya Muhamad (s.a.w).

Ibrahim, mwenyeji wa Uru wa Ulkadayo (Mesopotamia), leo Iraq, wa kabila la Waebrania anahama kutoka Iraq na kwenda Haran, Syria, na baadaye kuingia Kaanani (Uyahudi), ambapo Mwenyezi Mungu anamtokea katika njozi na kumwapia Ibrahimu kuwa, ardhi yote hiyo amepewa yeye na uzao wake na kuahidiwa Baraka. Yaani, kubarikiwa kwa kila atakaye mbariki na kwamba jamaa zote za dunia zitajibarikia. Pamoja na ahadi hiyo, Mungu anamwambia nabii Ibrahimu kuwa uzao wake utakwenda utumwani, Misri, kwa miaka mia nne (400) hadi kizazi cha nne, ndipo watakapookolewa na kupandishwa Kaanani.

Mizizi ya ugomvi huo inaanzia mnamo Karne ya Kumi na Tisa (19), wakati wa vuguvugu la utaifa la Uzayuni na Uarabu. Vuguvugu la Wayahudi lilianzishwa kuwa la kisiasa, mwaka 1892, dhidi ya Urusi na Ulaya. Mkakati ulianza kwa Wayahudi wote, popote walipo, kurejea katika nchi ya Palestina ambapo walipachukulia kuwa ndipo nchi yao ya asili. Katika kutimiza azma yao, Muungano wa Kizayuni na Taasisi za Fedha za Kiyahudi walihimiza uhamiaji na kufadhili ununuzi wa ardhi Palestina, chini ya utawala wa Ottoman na Uingereza. Mgongano huo ukianzishwa na Uingereza, kupitia Mikataba mitatu: Mkataba wa McMahon (chini ya Sir Henry McMhaon-Hussein); Azimio la Balfour la Novemba 2, mwaka 1917; na Mkataba wa Sykes-Picot, chini ya mwanadiplomasia wa Uingereza, Mark Sykes na Mfaransa, Frncois George-Picot.

Aidha, tangu hapo kulifuatiwa na milipuko ya mapigano ya mara kwa mara, kati ya Wayahudi na Waarabu, katika eneo la Palestina. Hakuna asiyekumbuka jinsi kiongozi wa Chama cha Nazi, Adolf Hiltler alivyowafanyia Wayahudi maangamizi makuu ya kupitia angamizo la Holocaust, ikiwa ni jitihada ya kulifuta taifa hilo. Azimio la Umoja wa Mataifa la mwaka 1947, liliridhia kugawanywa kwa nchi ya Palestina kwa Wayahudi na Wapalestina, ambapo Wayahudi walikubali na Wapalestina wakiungwa mkono na Umoja wa Nchi za Kiarabu, wakikataa na kusababisha kuzuka vita baina yao. Vita hivyo viliwafanya Wapalestina kuhama na kukimbilia nchi jirani za Kiarabu wakiwa wakimbizi yaani Al-Naqba. Makundi kwa makundi ya Wazayuni kutoka Ulaya Magharibi na Marekani walihamia Israeli. Zikabuniwa propaganda kuwa Wazayuni walikuwa katika mateso makali, chini ya utawala wa Adolf Hitler.

Miongoni mwa vitengo vilivyoundwa kuilinda Israeli, kilikuwa ni kikundi cha ulinzi na ujasusi, maarufu kikijulikana kama Shay ambacho wakati wa utawala wa Waingereza, wanachama wake walikuwa mkono muhimu wa harakati za chinichini za Mazayuni dhidi ya maeneo ya wenyeji wa asili ya Palestina. Wakazi asilia wa maeneo hayo ni Wafilisti na Wayahudi. Kitengo hiki kilipata msaada mkubwa, kutoka kwa wakala mkubwa wa Mazayuni, Zionist Congress, idara iliyoanzishwa mjini Zurich mwaka 1929.

Mara baada ya kuundwa taifa la Israeli, wahamiaji kutoka Ulaya na Marekani (Wazayuni) wakiongozwa na Shay walisuka mipango na kuendesha shughuli za kijasusi sehemu mbalimbali ulimwenguni. Kabla ya hapo, tokea mwaka 1923 hadi ilipofanikisha mpango wake, mwaka 1948, Shay ililenga kuanzisha taifa huru la Kizayuni katika maeneo ya Waarabu.

Na, mbinu iliyotumika wakati ule, ilikuwa kupandikiza watawala wa Kizayuni kimya kimya, ambao kwa taswira ya nje walionekana kama watumishi wa utawala wa Kiingereza, ambapo, wakati huo huo, walitumia fursa ya utawala kuandaa programu na kupanga mikakati dhidi ya Waarabu hasa wakazi wa maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, taarifu za kijasusi zilikusanywa ili kutumika katika udanganyifu au propaganda na mipango ya utekaji nyara maeneo hayo.

Makala hii ni kutoka katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi Sura ya 1, Uk 10.

0715865544/0755865544

View attachment 649590
 
Uislamu umekuja miaka ya 600 AD , sasa wakajipendekeza kwa wayahudi na kudai ibrahimu alikuwa muislamu, kitu ambacho sio kweli, before 600AD hakuna historia,wala mabaki ya chembe ya historia yanayoonesha paliwahi kuwepo din inaitwa uislamu,

Waarabu walikuwa. Wanaabudu jiwe jeusi na kufanya ibada kwa mungu allah,
Ndio tamadun alizokuja kuzichukua muhamad na kuziboresha kisha kusema huu utakuwa UISLAMU

lakin uislamu hauhusiani hata kidogo na MANABII WAYAHUDI ,

HATA QURAN inataja neno ISRAEL lakini haijui nini maana ya israeli, lkn BIBLIA inakuambia mwanzo na chimbuko la neno ISRAEL,

Quran haitaji neno YERUSALEM , Lakin biblia imelitaja mara 5000 ,

Waislamu wanaongopewa kuwa YERUSALEMU NI YAO , wakati hapo Yerusalemu palijengwa HEKALU NA MFALME SULEMAN, hilo hekalu muundo wake , na vitu vilivyokuwepo ndani haviendan na UISLAMU hata kidogo,

Leo pamejengwa msikit wa Al aqsa, miaka ya karibuni, lakin bado kuna waislamu wanadanganywa HUO MSIKITI ALIJENGA SULEMAN
ckiriza ndg ifi unatambua wayahud ambao mnabii wao n mussa hawakupenda kusikia kuna mtume atakaekuja kuwa in yesu na hats baada ya kuja kwake wakampinga lakin haimaanish kuwa mtume yesu hamtambui mussa na histolia take coz aliletwa na mungu Huyo huyo aliemleta musa hali kadhalika kwa watu wa yesu hawakupenda kusikia kuwa kuna mtume mungine atakuja baada yak na ndo maana hats baada ya kuja kwake hajayasahau sehemu zote za msing ambazo waliotangulia kabla yake yalikua maeneo matakatifu mbele za mungu in short angalia chain hapo chin halafu tafakar
 
Suggestion yangu hawa watu waachwe tu, mmoja achukue ardhi au wakubaliane wachukue wote.
Kwa sababu ni ujinga kutumia dini ku-justify kugombania ardhi.
Kuna sehemu nyingi ina migogoro ya maeneo kwa kila mtu kuwa na hoja zake.
Wengine wanakubaliana na matokeo, wengine hutafuta suluhu, na wengine huendelea kupigana mpaka the last ones standing.
Huwezi ukadai walipewa na Mungu tu. Hiyo haitoshi, maana throughout history watu wamekuwa wakipinduana kuchukua ardhi.
Em tutafute a common ground ku-solve hili suala.
Kila mtu ana makazi pale, sasa kwa nini tunaona ni bora mmoja aondoke... Illogical.
Ni kweli mkuu hii mambo nilipewa tu na Mungu ina ukakasi kidogo

Kwanza kujiuliza kipindi anapewa ilo eneo lilikuwa tupu kwa maana halikaliwi na watu au? Na alie wapa tuseme Mungu hakuzingatia watu waliokuwa wanaishi hapo kabla kama sikosei kuna andiko linasema waue watu wote utakao wakuta mji huo,hapa kuna kama upendeleo ni kwanini nasi wote tunasema ni mfano wa mungu/watoto/waja wake lkn wengine ndo waonekane wana haki kuliko wenza wao tena mbaya upendeleo unao ratibiwa na baba muumba

Tuje ktk dhana ya baraka, kwanini eti tukiwabariki watu/jamii fulani nasi ndo tunabarikiwa, je hili tabaka la ubora nini chanzo chake nasi kama binaadam tulio huru kufikiri na kutenda ni sawa kweli mungu atupe hizi daraja za ubora na bila hata kufikiria na kujiuliza tunaona sawa tu hapa kuna ukakasi wa dhana ya ubora na unyonge na mbaya umetolewa na muumba juu ya viumbe wake ( Nina mashaka hapa haya madaraja ya ubora isije ikawa binaadam kajipa kwa sababu zake za kibinaadam tu kwa kutumia eti vitabu vitakatifu) maana haielezeki eti Mungu ndo atoe upendeleo huo why?

Sipingi maandiko yoyote ya imani zetu lakini hainizuii kutafakari kama mtu huru na ambae hafungwi na myororo wa historia na hasa ulioegemea ktk eti kitabu kitakatifu tu kuliko hali halisi ya nyakati hizi (pia hapa si wote wanaoamini hicho kitabu kama msingi wake ni kitabu tu) kwa ufupi na kwa mtizamo wangu dhana ya ubora kwa jamii fulani na mbaya imetolewa na muumba wa vyote huwa siielewi kabisa
 
Katab
Hakuna mwarabu nabii wa Mungu. Mohammad ni Anti-Christ aliyetabiriwa miaka 600 kabla ya hajaanzisha dini yake. Mohammad ni mtumishi wa Baali (habal) ambaye nyie mnamwita Allah. Baali ni Shetani ndo maana hata majini na mapepo huko kwenu ni viumbe wazuri.
katabiriwa kwenye kitabu kipi?
 
Ni kweli mkuu hii mambo nilipewa tu na Mungu ina ukakasi kidogo

Kwanza kujiuliza kipindi anapewa ilo eneo lilikuwa tupu kwa maana halikaliwi na watu au? Na alie wapa tuseme Mungu hakuzingatia watu waliokuwa wanaishi hapo kabla kama sikosei kuna andiko linasema waue watu wote utakao wakuta mji huo,hapa kuna kama upendeleo ni kwanini nasi wote tunasema ni mfano wa mungu/watoto/waja wake lkn wengine ndo waonekane wana haki kuliko wenza wao tena mbaya upendeleo unao ratibiwa na baba muumba

Tuje ktk dhana ya baraka, kwanini eti tukiwabariki watu/jamii fulani nasi ndo tunabarikiwa, je hili tabaka la ubora nini chanzo chake nasi kama binaadam tulio huru kufikiri na kutenda ni sawa kweli mungu atupe hizi daraja za ubora na bila hata kufikiria na kujiuliza tunaona sawa tu hapa kuna ukakasi wa dhana ya ubora na unyonge na mbaya umetolewa na muumba juu ya viumbe wake ( Nina mashaka hapa haya madaraja ya ubora isije ikawa binaadam kajipa kwa sababu zake za kibinaadam tu kwa kutumia vitabu vitakatifu) maana haielezeki eti Mungu ndo atoe upendeleo huo why?

Sipingi maandiko yoyote ya imani zetu lakini hainizuii kutafakari kama mtu huru na ambae hafungwi na myororo wa historia, kwa ufupi dhana ya ubora kwa jamii fulani na mbaya imetolewa na muumba wa vyote huwa siielewi kabisa
Kwanza fanya utafiti, hichi kinachoitwa biblia ni maneno ya mungu au ni ya watu.

Ukiisoma Quran, inasema hakuna aliembora mbele ya Allah isipokuwa MCHA MUNGU. Kwaio uwe muarabu, mzungu au mwafrika kama si mcha mungu huna ubora kwake.
 
Walio kuwa wanaishi katika hilo eneo walikuwa wakiabudu na kuitukuza miungu, mabaali na maashera hivyo Mungu ndio akamua kuwapokonya nchi yao na waangamizwe pengine wakawe fundisho kwa wale wa aina hiyo. Kwa nini wao mulize Mungu.

Kuhusu Israel uzao wa Yakobo kuwa taifa teule pia muulize Mungu ilikuwa vipi akaamua manabii kupitia katika uzao huo. Hata yeye Mungu/Bwana Yesu kuja duniani alizaliwa katika uzao wa Daudi myahudi? Maana kama Bwana Yesu angezaliwa katika uzao wa wagunya kwa mfano penginepo wagunya ndio wangekuwa taifa teule.

Ni wazi shetani naye ana watu ambao ni taifa teule lake na kwa hila zake akataka kujinasibisha na hilo taifa teule la Mungu.

Muhimu ni kujitahidi kuzishirikisha na kutumia akili zetu hizi za uwanadamu maana tutawajua kwa matendo yao ila hapo sasa unafiki na ugumu wa nyoyo za binadamu kuukubali huu ukweli mchungu ndio inakuwa kimbembe.

Ni kweli mkuu hii mambo nilipewa tu na Mungu ina ukakasi kidogo

Kwanza kujiuliza kipindi anapewa ilo eneo lilikuwa tupu kwa maana halikaliwi na watu au? Na alie wapa tuseme Mungu hakuzingatia watu waliokuwa wanaishi hapo kabla kama sikosei kuna andiko linasema waue watu wote utakao wakuta mji huo,hapa kuna kama upendeleo ni kwanini nasi wote tunasema ni mfano wa mungu/watoto/waja wake lkn wengine ndo waonekane wana haki kuliko wenza wao tena mbaya upendeleo unao ratibiwa na baba muumba

Tuje ktk dhana ya baraka, kwanini eti tukiwabariki watu/jamii fulani nasi ndo tunabarikiwa, je hili tabaka la ubora nini chanzo chake nasi kama binaadam tulio huru kufikiri na kutenda ni sawa kweli mungu atupe hizi daraja za ubora na bila hata kufikiria na kujiuliza tunaona sawa tu hapa kuna ukakasi wa dhana ya ubora na unyonge na mbaya umetolewa na muumba juu ya viumbe wake ( Nina mashaka hapa haya madaraja ya ubora isije ikawa binaadam kajipa kwa sababu zake za kibinaadam tu kwa kutumia eti vitabu vitakatifu) maana haielezeki eti Mungu ndo atoe upendeleo huo why?

Sipingi maandiko yoyote ya imani zetu lakini hainizuii kutafakari kama mtu huru na ambae hafungwi na myororo wa historia na hasa ulioegemea ktk eti kitabu kitakatifu tu kuliko hali halisi ya nyakati hizi (pia hapa si wote wanaoamini hicho kitabu kama msingi wake ni kitabu tu) kwa ufupi na kwa mtizamo wangu dhana ya ubora kwa jamii fulani na mbaya imetolewa na muumba wa vyote huwa siielewi kabisa
 
Uislamu umekuja miaka ya 600 AD , sasa wakajipendekeza kwa wayahudi na kudai ibrahimu alikuwa muislamu, kitu ambacho sio kweli, before 600AD hakuna historia,wala mabaki ya chembe ya historia yanayoonesha paliwahi kuwepo din inaitwa uislamu,

Waarabu walikuwa. Wanaabudu jiwe jeusi na kufanya ibada kwa mungu allah,
Ndio tamadun alizokuja kuzichukua muhamad na kuziboresha kisha kusema huu utakuwa UISLAMU

lakin uislamu hauhusiani hata kidogo na MANABII WAYAHUDI ,

HATA QURAN inataja neno ISRAEL lakini haijui nini maana ya israeli, lkn BIBLIA inakuambia mwanzo na chimbuko la neno ISRAEL,

Quran haitaji neno YERUSALEM , Lakin biblia imelitaja mara 5000 ,

Waislamu wanaongopewa kuwa YERUSALEMU NI YAO , wakati hapo Yerusalemu palijengwa HEKALU NA MFALME SULEMAN, hilo hekalu muundo wake , na vitu vilivyokuwepo ndani haviendan na UISLAMU hata kidogo,

Leo pamejengwa msikit wa Al aqsa, miaka ya karibuni, lakin bado kuna waislamu wanadanganywa HUO MSIKITI ALIJENGA SULEMAN
mtume muhamad na waislam kiujumla wanawafahamu yesu,musa,Ibrahim, zakaria ISIHAKA yakub na kadharka kupitia quran

mtume ISSA(yesu) anamtambua muhamad lakin watu wake wanamkana muhamad na watu wake muhamad lakin Huyo2 yesu anawafaham akina musa,ibrahima na chain yote.

njoo sasa kwa musa,mwenyewe anamtambua yesu na Muhammad kwa mujibu was Qur'an lakin watu wake hawawatambui yesu na watu wake wala muhamad na watu wake wao wanawafahamu tu kuanzia mtume wao na waliokafuata kabla yake

NB:makundi hayo mawil ya chin sio wote ndo ndo wanapinga kwa maana wapo wayahud walimkubar yesu na wamemkubal muhamad na wapo wakiristo wanakubal uislaam na uislaam unatambua mitume wake wote waliokuja kabla ya Muhammad na unaamin wote hao walitumwa kufundisha iman moja mfumo mmoja was maisha ya unyenyekevu mbele za mungu ndo tofaut za majina ya din ilipotokea
 
Uislam ulianzia Saud Arabia na akina Mohamad
Mohamad anazaliwa, anatambaa, ana anza kuongea na kutembea Wayahudi na Wakristo wana muangalia
Uislam ulianzia toka enzi za Adam na Hawa. Soma Quran ujuwe ukweli Acha kukamatiwa akili.
 
Asante kwa kutufungua macho mkuu ila nadhani, kwa wakati huu, msingi wa kisiasa ni muhimu zaidi kutukiwa maana kuliko mrengo wa kidini.
 
Achen kuzaa wtt nje ya ndoa Ishmael Alitangulia Kaanan lkn ulikuwa nje ya Agano Hvyo nchi si yake Yakobo mbalikiwa ndiye mmiliki halali hao wengine watafute pa kwenda angalizo usinchukie Mimi muulize MUNGU aliye juu
Kwa hiyo baba Abraham alikuwa malaya ?? Hadi kuzaa nje ya ndoa ???
 
Kwa hiyo baba Abraham alikuwa malaya ?? Hadi kuzaa nje ya ndoa ???

Unachotakiwa ujue ni kuconnect dots. Shetani alimdanganya Hawa kwa hila na Hawa akamshawishi Adamu wakamuasi Mungu. Sarai/Sara akamshawishi Ibrahimu akamzaa mtoto nje ya agano lake na Mungu.
 
Uislamu umekuja miaka ya 600 AD , sasa wakajipendekeza kwa wayahudi na kudai ibrahimu alikuwa muislamu, kitu ambacho sio kweli, before 600AD hakuna historia,wala mabaki ya chembe ya historia yanayoonesha paliwahi kuwepo din inaitwa uislamu,

Waarabu walikuwa. Wanaabudu jiwe jeusi na kufanya ibada kwa mungu allah,
Ndio tamadun alizokuja kuzichukua muhamad na kuziboresha kisha kusema huu utakuwa UISLAMU

lakin uislamu hauhusiani hata kidogo na MANABII WAYAHUDI ,

HATA QURAN inataja neno ISRAEL lakini haijui nini maana ya israeli, lkn BIBLIA inakuambia mwanzo na chimbuko la neno ISRAEL,

Quran haitaji neno YERUSALEM , Lakin biblia imelitaja mara 5000 ,

Waislamu wanaongopewa kuwa YERUSALEMU NI YAO , wakati hapo Yerusalemu palijengwa HEKALU NA MFALME SULEMAN, hilo hekalu muundo wake , na vitu vilivyokuwepo ndani haviendan na UISLAMU hata kidogo,

Leo pamejengwa msikit wa Al aqsa, miaka ya karibuni, lakin bado kuna waislamu wanadanganywa HUO MSIKITI ALIJENGA SULEMAN
Hapa umeandika ukweli mtupu, inaonekana umebobea kwenye maswala haya.
 
Tatizo huu mgogoro wanatajwa waislam na wayahudi tu ila wakristo hawatajwi sijui ni kimkakati au bahati mbaya, nataka kujua wakristu walioa maeneo hayo ya Jerusalem wapo upande upi, wa Israeli au Palestinia?
mkuu wakristo wapo asilimia 2% tu za raia wote (kati ya hao 80% ni waarabu iliyobaki ni wahamiaji wasio pata uraia),wayahudi wapo 74.9% na muslim 20.8%.wayahudi hawautambui ukristo.
 
Kwa hiyo baba Abraham alikuwa malaya ?? Hadi kuzaa nje ya ndoa ???
Kosa kubwa alilofanya Abraham ni kuufanyia kazi ushauri wa mkewe kutembea na kijakazi wake ndo yakapelekea hadi leo uzawa wake kutopatana.
Tukiambiwa hakunaga balance sheet kati ya mke na mume tunakuwa wabishi mwishoni yanatukuta mabalaa.
 
Yaani kama leo 21st Century ustaarabu wa wanadamu wanatumia "dini"/"fiction" kama msingi wa kuamua mambo nyeti ya ustaarabu mzima wa humanity basi tutakua na matatizo makubwa sana na yameshatushinda kuyakabili.

"Dini" ni concept moja ya uongo na kitapeli na ya kizandiki mno which can never hold any water....Hao waisrael na mungu wao wanamtambua wao waendelee nae wao kama wao.....wasilete upuuzi wao kwa jamii ingine isiyo-subscribe kwenye huo ujinga wao wanaouamini wao...

Ni ujinga wa hali ya juu kwenda mahali na hoja ya kidini ku-claim something
 
Kosa kubwa alilofanya Abraham ni kuufanyia kazi ushauri wa mkewe kutembea na kijakazi wake ndo yakapelekea hadi leo uzawa wake kutopatana.
Tukiambiwa hakunaga balance sheet kati ya mke na mume tunakuwa wabishi mwishoni yanatukuta mabalaa.
Ugomvi haukuanza hapo.Mhayudi alipokataa kumtambuwa Yesu,na kumuita mtoto wa nje ya ndoa ndio tatizo limeanzia hapo.Kama myahudi angemtambua Yesu,tatizo lisingekuwako.Laana ya kutomtambua Yesu,ndio inawatafuna waisral,itawatesa daima.
 
Back
Top Bottom