Kifaa rahisi cha kupukuchua mahindi kutoka kwenye gunzi

Kifaa rahisi cha kupukuchua mahindi kutoka kwenye gunzi

Siwezi poteza muda wangu kumchukia mtu asiejielwa wa kuelewa nini anata. PROF. Chawa
kulikoni pasipo husika unaamsha mihemko dhidi ya maoni yangu ikiwa sio chuki hiyo gentleman?

hakuna haja ya kuharibu mjadala wenye hoja mahususi sasa, ni muhimu kujitengenezea kifaa hicho cha kubangua mahindi na kuona ugumu au urahisi wake katika kupukucha 🐒
 
Ni ubunifu mzuri ila naona kuna changamoto zifuatazo:
1. Hivyo visoda vitakuwa butu mapema kabla ya kazi kuisha. Kuna haja ya kuweka vifuniko vingi akiba kwa ajili ya replacement ya vile vilivyo chakaa.
2. Hiyo mashine inafaa kwa mkulima mdogo kabisa mwenye shamba labda nusu eka hadi eka moja tena liwe ni shamba lisilotoa mazao mengi na lipo karibu na nyumbani. Sio rahisi kuitumia hiyo mashine kupukuchua gunia 12+. Hiyo mashine haitofaa kwa wale wenye mashamba ya mahindi huko maporini i.e. mbali na nyumbani au wale wenye mashamba makubwa. Huku Umasaini shamba la kawaida ni 20-50 Acres. Shamba kubwa ni hadi ekari 200 au zaidi. Hiyo mashine haitamudu au itakuwa gharama kubwa kwani inatakiwa mashine hizo ziwepo nyingi na wahudumu pia wawe ni wengi hapo shambani siku ya kuvuna. Ukivuna nusu-nusu shamba lako, ujue ukiondoka tu na wezi watakuja kumalizia palipo baki.
3. Hiyo mashine haitoi ushindani kwa mashine zile zinazoendeshwa kwa Injini za moto.
Nimewalenga hawa wachini wanaotumia mikono sio hao wenye kumudu kununua au kukodi mashine za kupukuchua mahindi.
Gunia hadi kumi unaweza tumia kifaa hiki kama familia kila mmoja akiwa na chake,kwa msimu mmoja tu hakiwezi chakaa
 
Utapukuchua mahindi mangapi na kifaa hicho,, wakati tunataka kifaa ambacho utapukuchua mahindi 30 kwa wakati mmoja,, siyo mhindi 1
Zipo mashine ni mfuko wako tu au ukiweza ubunifu tu unatumia mota au pikipiki kuendeshea kinu
 
Kila mmoja naomba apeleke ubunifu huu wa kijijini kwake ikawasaidie watu wasiumize mikono kupukuchua mahindi toka kwenye magunzi.
Kifaa hiki kimetengenezwa na vizibo vya soda misumari na ubao.
Huu ni ubunifu toka China kwa gharama nafuu kabisa.

View attachment 3284201
Tukiwa wabunifu umasikini unakimbia
joseph1989 umeona matumizi ya akili,mimi na wewe tumebishana sana kwenye ule uzi wa Mchango wa special schools kwenye Innovation, Ona hapa unahitaji shilingi ngapi kugonga hivo visude hapo,Hii ndio innovation mkuu,
 
Ila iliwekwa mada ya wowowo hapa inachangiwa mwezi mzina non stop
Unaujua muziki wa wowowo lakini mkuu? Ongelea vitu vingine please 😂😂

343064463.jpg
 
joseph1989 umeona matumizi ya akili,mimi na wewe tumebishana sana kwenye ule uzi wa Mchango wa special schools kwenye Innovation, Ona hapa unahitaji shilingi ngapi kugonga hivo visude hapo,Hii ndio innovation mkuu,
Ungekuwa unajua matumizi ya akili ungelijibu hili swali ila umekimbia.
Screenshot_20250327_075611_Chrome.jpg

Mwaka 2007 nishamshuhudia bro wa Mechanical Engineering akitengeneza hiyo machine ya kupukuchua mahindi.Halafu hizo mashine ndogo ndogo zipo kibao ukienda COET, DIT nk.Tatizo lenu linarudi pale pale hamna hela ya kufund hizo projects na kuzigeuza kuwa biashara.
 
Mada nzuri kama hizi zina uchangiaji mdogo😭
Inatia aibu kubwa na kudumaza akili zetu na maendeleo yetu pale ambapo wengi wanashabikia zaidi mambo ya kutubomoa kuliko ya kutujenga. Mabadiliko na ukombozi mkubwa wenye tija kimtazamo na kimaendeleo inabidi uanzie kwenye fikra (mindset liberation).
 
Back
Top Bottom