Kifalsafa "kimantiki" Yesu hakutolewa Kafara. Dunia imedanganywa

Kafara ni kupoteza Jambo Fulani lenye thamani mazima. Yaani hutolipata tena. Una umefanya hivyo kwaajili ya Upendo ili upate Jambo zuri au uweka Hali ikae Sawa..
Unapaswa kuelewa vizuri alichofanya Yesu Kristo, na kwanini alifanya hivyo na kwasababu gani kafara au vizuri zaidi SADAKA ya Yesu inasemwa kuwa ilitolewa mara moja tu tofauti na kafara/sadaka nyingine.

Yesu alikufa msalabani ili kuukomboa ulimwengu. Kufa kwa ajili ya kusudio flani na sio kufa kwa uzee au ugonjwa. Manake ni kwamba aliweza kutoa kitu kikubwa zaidi ya kitu kingine, yaani uhai wake mwenyewe. Kwa vile Yesu ni Mwana wa Mungu na asiye na doa lolote, basi sadaka yake ilikuwa ya upeo wa juu kabisa na hakuna mwanadamu anaweza kufikia hata akijitolea kufa kwa ajili ya watu.

Nini kilitokea baada ya Yesu kufa msalabani. Alikwenda kuzimu (himaya ya giza na makao ya shetani). Kutokana na nguvu ya kafara alilolitoa kwa damu yake na uhai wake mwenyewe, aliweza kumnyang'anya shetani zile kamba au funguo alizokuwa anazitumia kuwatesa na kuwaangamiza wanadamu.

Kazi imekwisha au anavyosema mwenyewe; Yametimia au yamekwisha. Alipomaliza kazi hiyo kubwa na akiwa sasa na ameshanunua na kulipia haki zetu kwa damu yake, aliweza sasa kwa uwezo wa Kimungu kurudi na kuonekana katika ulimwengu wa kawaida, lakini sasa akiwa na mwili wa utukufu au hali ya kiroho. Ila kama ni kafara aliitoa na maisha yake hayakuwa tena yale yale ya kale, bali alibadilika kabisa na kwenda kwenye maisha mapya, hata baada ya kufufuka hakuishi tena maisha ya kawaida, ya kale yalikwisha kabisa sio tu kwake bali hata kwa wale aliowatolea maisha yake.
 
kujitoa kafara ni kubeba mzigo wa wengi, ili wao wawe salama, wanaume wamejitoa kafara hata kuingia sehemu hatarishi ili familia zao ziwe salama, Askari wamejitoa kafara kulinda mipakani ili taifa libaki salama

Askari wapo tayari Kujitoa Kafara kwaajili ya kulinda watu na sio kwamba wamejitoa Kafara.

Hujasikia wanajeshi wa Congo huko wanajisalimisha?

Kujitoa Kafara na kuwa tayari Kujitoa Kafara ni mambo mawili tofauti.

Mtu anaweza akawa tayari Kujitoa Kafara lakini siku ya Kafara akakimbia
 

Sasa Mkuu unatoa Kafara kitu Fulani alafu unauhakika utakipata kitu kilekile alichotoa Kafara. Hiyo ni KAFARA kweli?
 

Pongezi kwa maoni yako. Lakini haimaanishi kwamba yako sahihi. Ingawa binafsi nayaheshimu
 
Nimekuelewa ila Kwa mujibu wa biblia na yohana 1---,yesu(huyo tunayemuongelea) ni muunganiko wa vitu vitatu=Mungu,Roho na Binadamu,Kwa kuwa lengo ni kumkomboa binadamu basi kilichokufa hapo ni huo ubinadamu,kilichobaki Kwa huyo yesu ni Mungu na Roho ndo vilivyofufuka basi.
 
Sijadoma yote ila kati ya uongo mkubwa wazungu wamefanikiwa kutuhadaa, na wanapiga hela ndefu sana bila hustle ni dini. Dini zote duniani zimeanzishwa na wao na makao makuu yapo kwenye nchi husika. Na sadaka na zaka zote zinaenda kwao, yesu manabii sijui kina nani nikama kina mkandamizaji wanavyotufanyia leo, miaka 500 mbele utasikia kina zumaridi wanasomwa kweny bibilia ya wakati huo
 
Qyesu aliuawa kwa sababu alienda kinyume na mafundisho ya kiyahudi, wala hakufia mtu yeyote
 
Leta hoja acha taarabu kama za ccm
Siwezi kukupa hoja yoyote wewe ambaye umekaririshwa ujinga wa Madrassa na ukanielewa.. Umefundishwa kupinga ufufuko wa Yesu na ndio msingi wa Imani yako.. Sasa hivi mimi ntakupa hoja gani unielewe.. Ila narudia Tena.. Habari za Yesu ni bora mkaachana nazo tu kwa sababu hamumuwezi huyo.. Na hata mkileta mawazo yenu na mafundisho yenu hayatabadili ukweli kuwa Yesu ndio njia Ukweli na Uzima.. Na kwake Kila goti litapigwa..
 

Umefafanua vizuri sana.
Robert Heriel Mtibeli una la kujifunza hapa.
 
kwani unafikiri kafara ya Yesu ilitakiwa kufanyika vipi? je unaamini kafara inafanyika juu ya mwili na sio roho?
 
Ubarikiwe sana
 
Afadhali wavaa kobazi wao wanajua mtu wao alikufa wala hakufufuka na hatakaa afufuke wala hakupaa mbinguni amezikwa kama wengine na kaburi lake lipo hadi leo linaitwa alkaaba ila wanaamini siku ya kiama watakutana naye huko atakusanya umati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…