Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Paroko wa Kanisa la Roman Catholic huko Misenyi Kagera ametiwa mbaroni na Polisi pamoja na wenzake wanna akiwemo Baba mzazi wa mtoto albino aliyeuwawa.

Inadaiwa Bwana Paroko Kwa jina la Epidius Rwegishora alimfuata Baba mzazi wa mtoto albino aliyeuwawa na kumshawishi eti wafanye biashara ya viungo.

View: https://www.instagram.com/p/C8Zj-FcNzue/?igsh=MWFjZmdxcHZ2ZHh5MQ==

My Take
Hayo ndio Makanisa yenu na hao ndio Viongozi wenu mnaodai wanawawekea mikono ya Baraka.

Hakuna watu Wana kashfa za uhayawani na unyama ikiwemo uchawi kama Viongozi wa dini mlizoletewa na Wazungu na Waarabu kuanzia usenge(Ushoga) Hadi kulawiti Watoto.Very sad.

R.I.P mtoto.

View: https://www.instagram.com/p/C8ZmayFoN5v/?igsh=MXZneTRuOTdvOHpzdQ==

Na wewe acha kuandika kama unatumia matako kufikiri
Tupo under the same umbrella
About izo religion..na ni mtu mmoja ndo kafanya ivo sio kanisa...mpuuzi wewe
 
Ila inaweza ikawa kweli ni padre..huwezi kuwa paroko msaidizi kama sio padre..na mm nimeumia ila hii ni dhambi yake binafsi na sio kanisa...
Nadhani ni vyema ikathibitishwa, kwa sababu wanaume wengine tunahangaika kutafuta fedha ili maisha ya familia yaende,
mapadre wa kanisa katoliki hawana familia inakuwaje ashiriki dhambi hii ili apate pesa,
 
View attachment 3020852

Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imewataja watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Maidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.

Paroko huyo pia anatuhumiwa kuwa ndiye allyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.

Pia soma:
Akina Shomile vipi tena?
 
Baba paroko siyo padre,wamesema ni kijana alikua mlevi akachukuliwa na kanisa kulelewa ili aache pombe,siyo Kwamba na yeye ni paroko

ACHENI kulichafua kanisa, before hamjafanya utafiti
Hii comment nimeikuta sehemu nyingi sana, lakini inafikirisha. Taarifa ya polisi imetaja "Paroko msaidizi" na ili awe Paroko msaidizi lazima awe padri tena mwandamizi. Nyie mnaosema "ni kijana aliyekuwa nalelewa tu" mnataka kusema polisi wamekurupuka?? Kwasababu wao ndio waliomtaja kwenye taarifa yao.

Kama wamekurupuka maana yake tusubiri waje kuomba radhi na kusahihisha makosa yao lakini kwasasa kinachosomeka ni paroko msaidizi
 
Jipe muda soma habari.
Huyo bwana ni paroko msaidizi.
Kama katenda kosa, ametenda yeye kama yeye hajatumwa na kabisa.
Dini isikupe upofu, mahakama itachunguza ukweli wote
Madhehebu ya dini sawa na club za mpira kimifano, wachezaji wakifanya fujo uwajan, au kupewa kadi nyekudu, watakayoighalimu, ni club yao. Hivyo hivyo hata madhehebu yenu, msijitoe, yameshakua njia ya kujitafutia uchumi tu kwa watu??
 
Watu tunaowaamini kwenye jamii ndo wanatenda ukatiri wa hivi kumuua malaika Mtoto Asimwe ili wakafanye ushirikina.

-----
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama baada ya msako mkali kuanzia May 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia leo June 19, 2024 wamefanikisha kukamatwa kwa Watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya Mtoto Albino Asimwe Novart (aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera) wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta Mteja Mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema Watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa Mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa Mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza Mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman Mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine Mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada Mkazi wa Kamachumu.

“Jeshi la Polisi linatoa kutoa onyo kali kwa Watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo”

Pia soma:
Watu wanacomment ooh sijui kanisa Thihaka kama zote..
Do you really think kuna dini ambayo ni proven au ni ivi ivi tunaenda kiimani.. Anyway kama ni kiimanii acheni dhihaka za kikuma viongozi wetu kwenye izo dini ni binadamu kama sisi wana mapufungufu yao vile vile.. Ishu imefanywa na mmoja basii ndo mafollower ya dini gani sijuii yanapata point KUENI NA AKILI KMMK
 
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama baada ya msako mkali kuanzia May 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia leo June 19, 2024 wamefanikisha kukamatwa kwa Watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya Mtoto Albino Asimwe Novart (aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera) wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta Mteja Mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema Watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa Mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa Mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza Mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman Mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine Mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada Mkazi wa Kamachumu.

“Jeshi la Polisi linatoa kutoa onyo kali kwa Watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo”
#MillardAyoUPDATES
Picha zao Tafadhali
 
Na hawa ndo baba zetu wasio na uchungu hata chembe na damu zao.
Mama hata angeahidiwa kupewa dunia katu asingeweza kuuza damu yake. Wa mama wapokee maua Yao kwenye swala LA kupambania watoto wao
 
Inaniijia picha watoto wa Kipalestina namna gani wanavyouawa na madhaalim, kiumbe kama huyo hajui lolote, maumivu aliyoyapata wakati anakatwa viungo ama kuchinjwa, Sub haanallah! Wauawe haraka, hakuna kuchelewa
 
Back
Top Bottom