Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Kua vizuri kupambana na uhalifu ni kuhakikisha vitendo vya uhalifu havitokei kiholela kwa kuimalisha ulinzi na upelelezi mnene kabla ya matukio yenyewe, sio kumalizia watu Jera wengine wakishapoteza maisha, Alaaah.

Yani tangu May moaka June mtu kapotea mnasema mpo vizuri, Shwain.
 
Polisi wakiamua jambo lao, huwa wanalifanikisha ndani ya muda mfupi tu. Na kwa hili tukio la kikatili alilofanyiwa huyu malaika; hakika wanastahili pongezi!

Ila wakiamua sasa kuzingua; huwa wanazingua kweli! Na mfano mzuri wa kuzingua wa hawa jamaa, ni ule wa kipindi kile wa kumtaka Lissu na dereva wake eti warudi kwanza nchini ili wawape ushahidi wa kushambuliwa kwao kule Dodoma!!

Unajiuliza hivi tukio kama lile angefanyiwa PM, au VP; wangetoa kisingizio dhaifu kama hiki kweli 😁
 
downloadfile.jpg


Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imewataja watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Maidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.

Paroko huyo pia anatuhumiwa kuwa ndiye allyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.

Pia soma:
 
Watu tunaowaamini kwenye jamii ndo wanatenda ukatiri wa hivi kumuua malaika Mtoto Asimwe ili wakafanye ushirikina.

-----
Asimwe.jpg
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama baada ya msako mkali kuanzia May 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia leo June 19, 2024 wamefanikisha kukamatwa kwa Watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya Mtoto Albino Asimwe Novart (aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera) wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta Mteja Mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema Watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa Mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa Mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza Mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman Mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine Mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada Mkazi wa Kamachumu.

“Jeshi la Polisi linatoa kutoa onyo kali kwa Watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo”

Pia soma:
 
Binadamu utu umetuisha, wanadai na baba mzazi wa mtoto kahusika na kakamatwa, hawa jamaa wanahitaji adhabu nzito sana iwe fundisho kwa wengine
 
Hawa kama ni wao kweli wapelekwe kwenye uwanja wa shule tukatoe hukumu mamaae hao ni kuwapiga chainsaw.Maana nikiangalia picha ya marehem inaniumiza sana maana na binti anamiaka miwili yy ni kufurahi tu km marehem pichani anafuraha tele harafu wajinga wanaenda kumkata dah .... .😭😭😭😭Pumzika kwa amani mtoto mzuri.
 
Paroko wa Kanisa la Roman Catholic huko Misenyi Kagera ametiwa mbaroni na Polisi pamoja na wenzake wanna akiwemo Baba mzazi wa mtoto albino aliyeuwawa.

Inadaiwa Bwana Paroko Kwa jina la Epidius Rwegishora alimfuata Baba mzazi wa mtoto albino aliyeuwawa na kumshawishi eti wafanye biashara ya viungo.

View: https://www.instagram.com/p/C8Zj-FcNzue/?igsh=MWFjZmdxcHZ2ZHh5MQ==

My Take
Hayo ndio Makanisa yenu na hao ndio Viongozi wenu mnaodai wanawawekea mikono ya Baraka.

Hakuna watu Wana kashfa za uhayawani na unyama ikiwemo uchawi kama Viongozi wa dini mlizoletewa na Wazungu na Waarabu kuanzia usenge(Ushoga) Hadi kulawiti Watoto.Very sad.

R.I.P mtoto.

View: https://www.instagram.com/p/C8ZmayFoN5v/?igsh=MXZneTRuOTdvOHpzdQ==
 
Back
Top Bottom