View attachment 3020803
Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imewataja watuhumiwa waliokamatwa ambao walieleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hilo ni pamoja Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Maidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu.
Paroko huyo pia anatuhumiwa kuwa ndiye allyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.
Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada mkazi wa Kamachumu.
Credit - HabariMtandaoni