Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Kifo cha Asimwe Novath (Albino); Baba mzazi na Paroko msaidizi washikiliwa kwa tuhuma za mauaji

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama baada ya msako mkali kuanzia May 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia leo June 19, 2024 wamefanikisha kukamatwa kwa Watu tisa wakiwa na viungo vinavyodhaniwa ni vya Mtoto Albino Asimwe Novart (aliyeuawa Wilayani Muleba Mkoani Kagera) wakiwa wamehifadhi katika vifungashio vya plastiki wakitafuta Mteja Mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Polisi, David Misime imesema Watuhumiwa waliokamatwa ambao wameeleza jinsi walivyoshiriki katika tukio hili ni pamoja Baba mzazi wa Mtoto huyo aitwaye Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni Mganga wa jadi Mkazi wa Nyakahama, Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa Mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu na pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga.

Watuhumiwa wengine ni Dastan Kaiza Mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman Mkazi wa Nyakahama, Gozibert Alkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Rwenyagira Burkadi Mkazi wa Nyakahama Kamachumu, Ramadhani Selestine Mkazi wa Kamachumu na Nurduni Hamada Mkazi wa Kamachumu.

“Jeshi la Polisi linatoa kutoa onyo kali kwa Watu wanaoendekeza imani za kishirikina ikiwemo kupiga ramli chonganishi wakiaminishana kwamba wanaweza kupata utajiri kwa njia za kishirikina kuacha tabia hizo”
#MillardAyoUPDATES
Screenshot_20240619-192822_WhatsApp.jpg
 
Polisi wakiamua jambo lao, huwa wanalifanikisha ndani ya muda mfupi tu. Na kwa hili tukio la kikatili alilofanyiwa huyu malaika; hakika wanastahili pongezi!

Ila wakiamua sasa kuzingua; huwa wanazingua kweli! Na mfano mzuri wa kuzingua wa hawa jamaa, ni ule wa kipindi kile wa kumtaka Lissu na dereva wake eti warudi kwanza nchini ili wawape ushahidi wa kushambuliwa kwao kule Dodoma!!

Unajiuliza hivi tukio kama lile angefanyiwa PM, au VP; wangetoa kisingizio dhaifu kama hiki kweli
 
Dizasta katika ile ngoma yake...!!

"Kanisa nilikuja uniongoze

Nimpende mungu wewe unaifunza nimwogope

Jua kali lilinifunza kukaba nikakupa maisha

Na cha ajabu haujanifunza chochote

Nasikia una pande mbili za sarafu
Upande mzuri na upande unaoingia dili mpaka na wafu

Na unanifundisha baya haliwi na thawabu
Nilikuwa mjinga na sasa nayabashiri majawabu"
 
Polisi wakiamua jambo lao, huwa wanalifanikisha ndani ya muda mfupi tu. Na kwa hili tukio la kikatili alilofanyiwa huyu malaika; hakika wanastahili pongezi!

Ila wakiamua sasa kuzingua; huwa wanazingua kweli! Na mfano mzuri wa kuzingua wa hawa jamaa, ni ule wa kipindi kile wa kumtaka Lissu na dereva wake eti warudi kwanza nchini ili wawape ushahidi wa kushambuliwa kwao kule Dodoma!!

Unajiuliza hivi tukio kama lile angefanyiwa PM, au VP; wangetoa kisingizio dhaifu kama hiki kweli
 
Tanzania ni nchi inayofuata Utawala wa Sheria, ni Nchi ya kidemokrasia, Viongozi wetu wana amini katika haki na usawa.

Kuna matukio yanatokea, yanaumiza saana, yanasikitisha saana, tukio la kuuwawa kikatili kwa mtoto Asimwe Novart tena mhusika akiwa ni baba mzazi ambaye alipaswa kuwa mlinzi wa huyu Malaika, kea kweli kuna muda unatamani Sheria ziwekwe pembeni na maumivu aliyopitia huyu mtoto wapitie hao wote waliohusika kukatisha uhai wa huyu Malaika.

Fikiria wakati Asimwe Novart akiwa anahitaji msaada mbele ya Wanaume katili, hakuweza hata kujitetea zaidi ya macho ya huruma alionyesha kuomba huruma kwa Wanaume hawa katili, Alihitaji upendo wa baba, lakini baba alimuangamiza.

Inauma, inaumiza kuona hawa watu waliotenda unyama huu, kwa sababu ya Tanzania kuwa nchi ya Utawala wa Sheria wanapelekwa mahakamani tena kwa gari, Kuna muda unatamani ungekuwa na whisk ushudie ule ukatili waliotenda wakitendewa wao waexperience maumivu aliyopitia Asimwe Novart.

Pumzika kwa Amani Asimwe Novart

Mwenyezi Mungu ibariki Tanzania

Mwenyezi Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom