Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Acheni unafiki wenu hapa Mbowe ameongea kama mwenyekiti wa CHADEMA na aliyosema ni sahihi, kama nyie mna jipya wekeni hapa tusome sio kuwa vibaraka na makuwadi wa MAFISADI tu.
Mlitaka amsifu Kikwete kwa kwenda Japan?
Unajua huwezi kusema kama unavyosema ikiwa unajua nini kinahitajika,sio watu wanachukia ya akina Mbowe na Zitto na wenzao lakini ,kilicho muhimu ni mhimili wa hayo wanayoyasema huwa haupo ,wameyasema ya Richmond ,EPA,Buzwagi na kila siku wanakuja na jipya ,sasa nini faida ya haya kwani yanaonekana yako mengi kuliko yaliokuwa tayari yameibuliwa ,naweza kusema hizi walizonazo na walizowahi kuziibua ni silaha nzito lakini wakizitumia vibaya haziotawasaidia kitu mfano hai ni wa majeshi ya Saddam Husein walikuwa na silaha nyingi na za kisasa lakini hazikuwafaa kitu walibaki kujisifu kwenye vyombo vya habari piga tajame ,wamepigwa na silaha zao,hivyo wapinzani wataendelea kushindwa mbali ya masiri makubwa makubwa waliyonayo kuhusiana na CCM.
Huyo Balai Lama walimuibua wao na mascandali kibao ,angalia sasa maneno kutoka kwa watu wa Balali yanazidi kusema kuwa Balali hakutafuna kitu wala hahusiki na kasheshe za wizi inamaana wapinzani wanaaza kupelekwa kkwenye kona itawabidi wamtafute tena nani anahusika na mwisho itaonekana hawana msimamo kwani wanabadilika badilika kila wanaemkamata wanaambiwa sie.
Akina Lowasa wote na wenzake wamesema wameonewa inamaana kamati za kina Zitto zitatoka na majina ya watu wengine ambao wanajulikana kama kafara na ambao huishia kwenye kujiuzulu tu ,ili kuwasafisha CCM na walio ndani ya Inner circle .
Nini faida ya kumkamata fisadi ,badala ya wakwasi hawa kuibuka kwenye majukwaa kwa nini hawaendi na vielelezo vyao mahakamani na kuwashitaki mafisadi na badala yake kungojea CCM iwawajibishe hamuoni kama CCM wana hiari yao na huu ni woga wa Kikwete tu moja kwa moja angelisema mwenye ushaidi aende nao mahakamani akafungue jalada ,sio kutushutumia viongozi wetu.Tumewachagua kwa kutumia vigezo vya utendaji wao wa kazi kama mnawaona ni mafisadi na muna ushahidi wa kutosha basi elekeeni kwenye vyombo vya sheria na washitakini kama wahujumu uchumi.
Kikwete wacha kuwawajibisha viongozi na wenzako ,usiwe wewe kuwa mwenye kuwashauri waachie ngazi kwani kwa kufanya hivyo utawamaliza wote na kila siku watakuzushiya mwengine.
Akina Kabwela ,Slaa ,Kabwe wote hawa wanafahamu sheria kwa kiasi chao ikiwa wamekuwa mabingwa wa kupeleleza na kupata ushahidi basi waelekee mahakamni huko ndiko watakakokwenda kutetea ,sio kutuchafulia nchi na kutufanya tupoteze muelekeo.