Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Kama Mbowe alisema haijamchukulia hatua?
Membe kasema eti serikali haihusiki je?hilo linatosha kuwa jibu juu ya kifo cha Balali?
Serikali hii ina wakati mgumu sana hadi sasa na tunasubiria Bunge la bajeti ......kuhakikisha kuwa hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe, na ripoti ya EPA itawekwa hadharani waziwazi..
Mwafrika wa Kike,
Nilipokuona umepotea last weekend bila ya kuonekana humu JF, nilijiamimisha kwamba you are somewhere working hard.... Kumbe machale yangu yalikua positive.
Mwaga issues mama.
Clue 1: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali ameondoka kwa matibabu kwenda "Boston"?
Clue 1: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali ameondoka kwa matibabu kwenda "Boston"?
Mwafrika wa Kike,
Mimi nimeandika mara nyingi hapa na kuudhi baadhi ya watu lakini msimamo wangu bado ni ule ule, nakubaliana na wewe kabisa na bado naendelea kuamini Ballali hajafa.
Watanzania tunaingizwa kwenye udanganyifu mkubwa sana. Tumeibiwa pesa zetu na sasa tunafanywa wajinga na kuanza kudanganywa.
Mimi kuna watu ambao nafahamiana nao kwa muda mrefu ambao ni wahusika wakuu kwenye hili jambo, ningeweza kukaa kimya ili kulinda urafiki. Ila imani yangu na moyo wangu unakataa maana kila nikifikiria napata sababu nyingi za kuamini Ballali hajafa kuliko za kunifanya niamini.
Inaelekea nchi yetu haina serikali, usalama wa taifa ni watupu na wanachojua ni kuiba na kutishia wananchi maskini badala ya kukabiliana na mafia wa kimataifa kama akina Ballali pamoja na watu wake ndani ya serikali yetu.
Tuendelee kupiga kelele mpaka kieleweke.
Kama vile ambavyo nilisisitiza kutolazimisha wasomaji hapa na watanzania walio nyumbani kuamini habari za kifo cha Ballali, sitafanya kinyume chake na kulazimisha watu kutokuamini kifo chake. Ninachosema hapa ni kuwa, safari zote nilizofanya kwenda Boston na baadaye DC kwenye ibada ya mazishi hazikunipa uthibitisho wowote wa kutosha kuwa Ballali yuko hai au amekufa. Nitaacha hili kwa wasomaji na watanzania kuamua waamini lipi kuhusu kifo cha Ballali. Ninachosema hapa ni kuwa, kuna juhudi kubwa sana zinafanywa na watu wakubwa kabisa katika serikali ya Tanzania na ya hapa Marekani ili habari nzima ya Ballali ibakie kuwa utata.
Clue 1: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali ameondoka kwa matibabu kwenda "Boston"?
Nakubaliana na wewe kabisa Mwafrika wa kike kutokana na ugunduzi wako,ndiyo maana nilisema siku habari za kifo cha Ballali zilipotolewa kwamba giza limetanda sana katika tukio hili zima na nilisema kuwa nitakuwa Tomaso katika hili! lakini FMES alipoleta uthibitisho nikaanza kubadili upepo lakini sasa hata mimi narudi kwenye msimamo wangu wa awali.
Kazi nzuri dada Mwafrika wa Kike!
Hili ndilo swali ambalo muhimu kabisa la kuanzia kwenye hii habari ya "kifo cha Ballali". Swali sasa sio tu kama Ballali amekufa au alikuwa mgonjwa, maswali ni kuwa, je alianza kuugua lini, aliondoka lini Tanzania, na serikali ilijua lini na vipi kuhusu kuondoka kwa Ballali......
Clue 1: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali ameondoka kwa matibabu kwenda "Boston"?
Clue 2: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali amefariki "Boston"?
Taarifa za kifo hapa marekani ni public info!
Na si familia inayotoa habari hizo kama wanavyodai kina Kishoka!
Habari hizo hutolewa na coroner kwenda kwenye magazet and so forth!
Na hao wenye hiyo funeral home nao wasiwasi sana kwasababu hata wao walitakiwa wawe na database yao ili tuweze kusearch watu waliokufa kama vile funeral home nyingine zinavyofanya!
Habari hizi tayari zingeshakuwa public hadi sasa!
Kwanini zinazuiliwa isivyo kawaida?
Hiyo funeral home nayo tutaichunguza tu!