Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kama Mbowe alisema haijamchukulia hatua?

Membe kasema eti serikali haihusiki je?hilo linatosha kuwa jibu juu ya kifo cha Balali?

Serikali hii ina wakati mgumu sana hadi sasa na tunasubiria Bunge la bajeti ......kuhakikisha kuwa hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe, na ripoti ya EPA itawekwa hadharani waziwazi..

MK,

Unadhani kuna mtu wa kumchukulia Mbowe hatua kwa chochote kile.... kuna usanii huko na uoga uliokithiri. Mimi nawachallenge ccm wamchukulie hatua Mbowe kwa kile alichosema ili mengine yote ya sirini yaje nje na yajulikane.
 
Wana JF,

Imefikia wakati ambapo maamuzi machungu inabidi yafanyike hapa JF na kama itawezekana kwenye media za nyumbani. Kwa zaidi ya wiki moja sasa mimi na baadhi ya wana JF hapa tumekuwa tunafanya uchunguzi kuhusu uhakika wa habari za kifo cha aliyekuwa Gavana wa benki kuu - Dr Ballali. Wakati haya yakiendelea, mimi nilizikubali na kuziamini (msisitizo zaidi kwenye imani) habari za kifo cha Ballali ambazo ziliwekwa hapa na Invisible.

Kulingana na taarifa, vyanzo vya habari, mipango ya mazishi, sala na maombi kwa marehemu ambavyo vyote viliwekwa hapa JF, imani yangu ilizidi kukua na kupelekea uamuzi wa kukubali kuwa Ballali amekufa. Hata hivyo, uchunguzi wa siri unaonyesha utata na usiri mkubwa sana kwenye ugonjwa na hatimaye kifo cha Ballali. Kila nafasi na gharama iliyotumika kupata hii habari imefikia kwenye mwisho mfu (dead end) na mchanganyo ambao haustahili kuwepo hapa.

Binafsi niliahidi kuwa nitaomba msamaha hapa JF kama itathibitishwa kwangu kuwa Ballali yuko hai. Naomba sasa niseme kuwa sina sababu ya kuthibitishiwa kuwa Ballali yuko hai ili niombe msamaha kwa kuamini kifo cha Ballali. Pamoja na kuwa sina hakika kwa sasa kuwa Ballali yuko hai, lakini pia ni vyema ikiwa wazi hapa kuwa sina hakika (na sikufanikiwa kupata uhakika kwa asilimia mia moja) kuwa Ballali amekufa. Juhudi zote za kutafuta hili na lile kuhusu kifo cha Ballali zinafikia mwisho na mlango mzito sana wa kufungua ili kujua ukweli. Na kwa hili, naomba msamaha kwa wana JF na watanzania.

Nimekuwa natumia sana neno imani (kuwa na hakika na yasioonekana) katika hii issue ya Ballali. Niliamini kifo cha Ballali na imeshindikana kupata uhakika wa kutosha kufikia hitimisho la kifo chake. Kwa hili, naomba msamaha na kusema hapa kuwa sina imani tena kuwa Ballali amekufa. Nafasi nyingi sana zilijaribu kutolewa kwa Ballali kutoa story yake kuhusu yote yaliyotokea BoT. Kwa sasa kuna mengi yamepatikana na yatawekwa hapa JF kama ilivyo kawaida ya kila miziki inayopatikana hapa JF. Ila katika hili la kifo cha Ballali, naomba niseme wazi kuwa sina imani tena kama amekufa na kwa sasa ninapinga habari zote za kifo cha Ballali.

Kama vile ambavyo nilisisitiza kutolazimisha wasomaji hapa na watanzania walio nyumbani kuamini habari za kifo cha Ballali, sitafanya kinyume chake na kulazimisha watu kutokuamini kifo chake. Ninachosema hapa ni kuwa, safari zote nilizofanya kwenda Boston na baadaye DC kwenye ibada ya mazishi hazikunipa uthibitisho wowote wa kutosha kuwa Ballali yuko hai au amekufa. Nitaacha hili kwa wasomaji na watanzania kuamua waamini lipi kuhusu kifo cha Ballali. Ninachosema hapa ni kuwa, kuna juhudi kubwa sana zinafanywa na watu wakubwa kabisa katika serikali ya Tanzania na ya hapa Marekani ili habari nzima ya Ballali ibakie kuwa utata.

Hata hivyo, ningependa kuwakumbusha wale wanaodhani kuwa kifo au kupotea kwa Ballali kutapelekea hii case kuisha wajiandae kwa safari nyingine. Inajulikana kabisa kuwa Mramba, Mgonja na viongozi wakubwa serikalini kwa pamoja au kwa nyakati tofauti waliiidhinisha malipo toka benki kuu. Iko wazi kuwa auditing ya Deloitte ilisitishwa baada ya kugundua mambo mengi ambayo serikali haikutaka yajulikane. Inafahamika kabisa kuwa wahusika wa wizi wa BoT ni wengi sana na Ballali ni kipisi tu cha mkuyu mzima. Inafahamika pia wizi wa BoT sio wa EPA peke yake, kuna mengine mengi ambayo hayajafanyiwa uchunguzi.

Kupotea au kufa kwa Ballali sio mwisho wa huu mchezo na hii movie. Kwa sasa ndio mwanzo sehemu ya pili ya hii series inaandaliwa na wengine wote kwa kuanzia na mzee wa kula nyasi (Mramba), Mgonja na wenzake wajiandae kwa sehemu ya pili ambayo ndio kwa sasa wametia mafuta kwenye moto.

Huu ni mwanzo tu.....
 
Last edited by a moderator:
Clue 1: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali ameondoka kwa matibabu kwenda "Boston"?
 
Mwafrika wa Kike,

Nilipokuona umepotea last weekend bila ya kuonekana humu JF, nilijiamimisha kwamba you are somewhere working hard.... Kumbe machale yangu yalikua positive.

Mwaga issues mama.
 
Mwafrika wa Kike,

Mimi nimeandika mara nyingi hapa na kuudhi baadhi ya watu lakini msimamo wangu bado ni ule ule, nakubaliana na wewe kabisa na bado naendelea kuamini Ballali hajafa.

Watanzania tunaingizwa kwenye udanganyifu mkubwa sana. Tumeibiwa pesa zetu na sasa tunafanywa wajinga na kuanza kudanganywa.

Mimi kuna watu ambao nafahamiana nao kwa muda mrefu ambao ni wahusika wakuu kwenye hili jambo, ningeweza kukaa kimya ili kulinda urafiki. Ila imani yangu na moyo wangu unakataa maana kila nikifikiria napata sababu nyingi za kuamini Ballali hajafa kuliko za kunifanya niamini.

Inaelekea nchi yetu haina serikali, usalama wa taifa ni watupu na wanachojua ni kuiba na kutishia wananchi maskini badala ya kukabiliana na mafia wa kimataifa kama akina Ballali pamoja na watu wake ndani ya serikali yetu.

Tuendelee kupiga kelele mpaka kieleweke.
 
Mwafrika wa Kike,

Nilipokuona umepotea last weekend bila ya kuonekana humu JF, nilijiamimisha kwamba you are somewhere working hard.... Kumbe machale yangu yalikua positive.

Mwaga issues mama.

Wewe acha tu mwenzangu...

Mwanzoni niliamini kwa sababu sikuamini kabisa kama kuna familia Tanzania inaweza kusema kuwa mwanafamilia mwenzao amekufa wakati si kweli au ni vinginevyo. Chanzo cha hii habari ni mtu wa ndani kabisa kwenye familia ya Ballali. Niliendelea kutumia neno imani kwenye maneno yangu kwa vile nilikuwa sina uthibitisho katika hili.

Baada ya uchunguzi wa karibu wiki nzima, kwa asilimia 95 ninapinga habari za kifo cha Ballali. Sina imani tena na habari za kifo cha Ballali.

Yataendelea.......
 
Mwafrika wa Kike,

Mimi nimeandika mara nyingi hapa na kuudhi baadhi ya watu lakini msimamo wangu bado ni ule ule, nakubaliana na wewe kabisa na bado naendelea kuamini Ballali hajafa.

Watanzania tunaingizwa kwenye udanganyifu mkubwa sana. Tumeibiwa pesa zetu na sasa tunafanywa wajinga na kuanza kudanganywa.

Mimi kuna watu ambao nafahamiana nao kwa muda mrefu ambao ni wahusika wakuu kwenye hili jambo, ningeweza kukaa kimya ili kulinda urafiki. Ila imani yangu na moyo wangu unakataa maana kila nikifikiria napata sababu nyingi za kuamini Ballali hajafa kuliko za kunifanya niamini.

Inaelekea nchi yetu haina serikali, usalama wa taifa ni watupu na wanachojua ni kuiba na kutishia wananchi maskini badala ya kukabiliana na mafia wa kimataifa kama akina Ballali pamoja na watu wake ndani ya serikali yetu.

Tuendelee kupiga kelele mpaka kieleweke.

Mtanzania,

Chanzo cha habari hii ni toka kabisa ndani ya familia ya Ballali. Hata mimi sina nia ya kuweka machungu kwenye familia ambayo kama kweli Ballali amekufa wako kwenye maombolezo. Mambo yote yaliyofanyika ikiwemo sala na ibada maalumu ya mazishi havitoshi kabisa kuthibitisha habari hii. Nimetumia muda wa kutosha kabisa kusafiri na kufuatilia hili na ukweli unaelekea kwingine kabisa tofauti na kile kinachoripotiwa.

Uchunguzi wa habari hii unakutana na utata mkubwa kabisa kiasi cha kuifanya hii habari nzima kutokuwa ya kweli.
 
Kama vile ambavyo nilisisitiza kutolazimisha wasomaji hapa na watanzania walio nyumbani kuamini habari za kifo cha Ballali, sitafanya kinyume chake na kulazimisha watu kutokuamini kifo chake. Ninachosema hapa ni kuwa, safari zote nilizofanya kwenda Boston na baadaye DC kwenye ibada ya mazishi hazikunipa uthibitisho wowote wa kutosha kuwa Ballali yuko hai au amekufa. Nitaacha hili kwa wasomaji na watanzania kuamua waamini lipi kuhusu kifo cha Ballali. Ninachosema hapa ni kuwa, kuna juhudi kubwa sana zinafanywa na watu wakubwa kabisa katika serikali ya Tanzania na ya hapa Marekani ili habari nzima ya Ballali ibakie kuwa utata.

I love you Mwafrika wa Kike....! Mapigo yangu ya moyo yanaongezeka, naongezea beti la tatu (lile beti la kwanza ni la Afrika, la pili ni la Tanzania, na La tatu ni la mwafrika wa kike) kwenye mwimbo wetu wa Taifa, na ninaliataja jina lako hapo... MUngu mbariki mwafrika wa kike!
 
Clue 1: Serikali iliambiwa lini na nani kuwa Ballali ameondoka kwa matibabu kwenda "Boston"?

Hili ndilo swali ambalo muhimu kabisa la kuanzia kwenye hii habari ya "kifo cha Ballali". Swali sasa sio tu kama Ballali amekufa au alikuwa mgonjwa, maswali ni kuwa, je alianza kuugua lini, aliondoka lini Tanzania, na serikali ilijua lini na vipi kuhusu kuondoka kwa Ballali......
 
Nakubaliana na wewe kabisa Mwafrika wa kike kutokana na ugunduzi wako,ndiyo maana nilisema siku habari za kifo cha Ballali zilipotolewa kwamba giza limetanda sana katika tukio hili zima na nilisema kuwa nitakuwa Tomaso katika hili! lakini FMES alipoleta uthibitisho nikaanza kubadili upepo lakini sasa hata mimi narudi kwenye msimamo wangu wa awali.

Kazi nzuri dada Mwafrika wa Kike!
 
Kinyamana,

Ukisoma postings za FMES jana utagundua na yeye hana uhakika tena. Anajiuliza maswali kama ya kwetu.

Ukiona mttu kama Mwafrika wa Kike ambay kuna wakati hawakuwa critical sana kwa Ballali ukilinganisha na mafisadi wengine. Ukiona na yeye anaanza kutilia mashaka kifo chake, jua hapo kuna tatizo kubwa sana.

Kama Ballali angelikufa naamini watu kama Mwafrika wa Kike wangealikwa kuuaga mwili wa marehemu.

Usalama wa taifa wako wapi? Balozi wetu anaenda kuimba kanisani akiliimbia gogo? Kweli nchi ya JK imefilisika kwenye kila idara.
 
Kama balali hajafa basi huko kwetu huo tunaita uchuro! basi kajichuria na atakufa kiukweli sooner. Mafisadi wangekubali tu kufilisiwa na kwenda keko kuliko huu ufungwa wa kujisingizia kifo, ni kifungo zaidi ya kifungo cha gerezani.
 
Hili ndilo swali ambalo muhimu kabisa la kuanzia kwenye hii habari ya "kifo cha Ballali". Swali sasa sio tu kama Ballali amekufa au alikuwa mgonjwa, maswali ni kuwa, je alianza kuugua lini, aliondoka lini Tanzania, na serikali ilijua lini na vipi kuhusu kuondoka kwa Ballali......

jamani mnatutisha! kuna gazeti moja la udaku nadhani ni risasi au sani sina uhakika niliiona mtaani leo, mbele kabisa kuna picha inayoonyesha jeneza lenye mwili wa bilali ukiwa altareni kwenye kanisa kuu la st stephen the matyrs, washington dc. tena wakasema mazishi yeke yalitumia masaa sita, mpaka watu wakachoka kufuatilia ibada.

sasa mwafrika wa kike tueleze kama nalo hili ni bonge la move.

siwezi kukataa kwa hili la mwafrika mwanamke, kwa kuwa mafisadi wa tz wanaishi mwezini, wakati sisi tunaishi hapa ardhini. mtu kuwa na 50bilioni kwenye akaunti yake, anaweza kutengeneza move moja nzuri kuliko zile za hollywood.

mh, mbesaaa
 
Angalau sasa tunaanza kuona mwanga, maana wengine tulikuwa tunajiuliza maswali mazito mazito na tunakosa majibu yake.

Kulikoni msiba ukahitaji kadi kuudhuria? Je tangu lini ktk mila za kiafrica Msiba ukawa sherehe?, Sina uhakika kama balali ni Mzee sana kusababisha watu kumfanyia sherehe wakati amefariki.
 
Mimi pia nafikiri kuomba tena msaada pale jangwa la Namib kule Namibia. Balali ni lazima ijulikane ameishia wapi.

View attachment 1603
Hawa wamefunzwa kunusanusa wakiwasaidia mbwa.

mierkat.jpg
Huyu kafunzwa kupiga picha adimu.

Balali ni lazima ijulikane alilazwa wapi tujue jina, alifia wapi pia tujue jina la mahali alipofia na halikadhalika amezikwa wapi tupajue.

Nchi zilizoendelea zinaweka kumbukumbu ya mambo yote na sasa umefika wakati wana JF walio karibu na huko kwenye utata wakachunguza kwa wakati wao.

Ni mpaka kieleweke.
 
Taarifa za kifo hapa marekani ni public info!
Na si familia inayotoa habari hizo kama wanavyodai kina Kishoka!
Habari hizo hutolewa na coroner kwenda kwenye magazet and so forth!
Na hao wenye hiyo funeral home nao wasiwasi sana kwasababu hata wao walitakiwa wawe na database yao ili tuweze kusearch watu waliokufa kama vile funeral home nyingine zinavyofanya!
Habari hizi tayari zingeshakuwa public hadi sasa!
Kwanini zinazuiliwa isivyo kawaida?
Hiyo funeral home nayo tutaichunguza tu!
progress.gif

Kwa nini mtu enlightened kama jmushi1 usiamue kuchukua some concrete course of action na kutuma petition kwa District Coroner (na ikiwezekana hata mahakamani) wa mji aliofia Ballali ili Coroner a-release to the public scrutiny the complete Death Certificate of Mr. Daudi Ballali ikionyesha sababu ya kifo chake (among other details)? Au labda tatizo ni kwamba bado haifahamiki ni mji gani haswa Ballali alipatwa na umauti? Au pengine hata official Death Certificate won't be enough to convince someone like you? Kwa nchi kama Marekani hicho ni kitu ambacho kinawezekana kabisa. Has anyone ever brought up this idea anyway?
 
Back
Top Bottom