Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania


Nakwambia wewe acha tu..... usanii wa hali ya juu hadi inatisha. Sasa hakuna ujanja tena. Usalama wa taifa wakishindwa kufanya kazi hapa basi wana JF tunaenda hadi kwenye vina vya habari kupata ukweli na kuuweka kwa hapa kwa niaba yao.
 

Kila kitu hapa kinatengenezwa kwa uangalifu mkubwa sana ila wanasahau kitu kimoja kuwa hawako peke yao katika hii dunia. Serikali ya Tanzania katika level ya juu kabisa inahusika na kila kitu hapa na ni swala la muda tu kabla kila kitu hakijaanza kuwageuka na kuwaaibisha.
 
Clue 3: Serikali ilipokuwa inalipia gharama za hospitali "Boston," hundi ilisema "pay to the order of...."?

hapa ndipo watu watakimbia nchi kwenye issue ya malipo ya gharama za hospitali... hii ya "Boston".....

Ninaomba tu wabunge wote wa upinzani na ccm wajiandae kwa mgongano mkubwa sana na serikali kuu katika hii issue.....

yanaendelea....
 
Kama balali hajafa basi huko kwetu huko tunaita uchuro! basi kajichuria na atakufa kiukweli sooner. Mafisadi wangekubali tu kufilisiwa na kwenda keko kuliko huu ufungwa wa kujisingizia kifo, ni kifungo zaidi ya kifungo cha gerezani.

Kweli mama,

Kuna wengi tu wanaoshangilia kwa kudhani kuwa wamempata Ballali katika hili swala kumbe na wao siku zao zinakuja karibuni ....... aibu kabisa. Afadhali kuishi maisha ya uadilifu kuliko kufikia kiwango hiki. Faida ya mapesa mengi ni nini sasa kama watu wanakuwa wanategemea kifo cha mwenzao au cha kwao binafsi ili kuishi kwa "amani, na raha mstarehe"....

grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Clue 2: Nani alisema ilikuwa inatumiwa "hundi" kufanya malipo?

balali hakuwa mfanyakazi wa siri-kali hadi 'umauti' ulipomfika, so sidhani kama kulikuwa na hundi ya malipo toka kwa siri-kali. Kama alifia hospitali, lazima kuwe na kumbukumbu za kifo, na kama kafia nyumbani, nani alithibitisha kifo chake? kama kifo hakijathibitishwa kuna uwezekano kuwa wamemzika akiwa hai?
 
.....tena wakasema mazishi yeke yalitumia masaa sita, mpaka watu wakachoka kufuatilia ibada.
Mwikimbi, Kubadili 'living organism' to 'non living organism' while leaving no trace in a single day is hard work!!
 

Mwafrika wa Kike,

Kwanza ninakuvulia kofia (sina kofia, ila naivua kama ishara) kwa kazi yako nzuri.

Mimi pia sikuamini kwamba Ballali amekufa, kama ambavyo sikuamini kwamba Osama Ben Laden ndiye aliyehusika na the "controlled demolition" (sio terrorist attack) ya World Trade Centre, Pentagon, etc. Kuna conspiracy kubwa sana, na hii si theory, it is practical. Lakini kama ulivyosema, kuna utata mkubwa.

Kwa upande mmoja wa shilingi (kwa kuwa mahesabu "yao" bado hayajakaa vizuri), ninaamini kwamba Ballali hajafa, ila, mbinu zinafanyika tuamini kwamba amefariki, hususan kwa kupitia "mainstream media" ya Bongo. Bahati mbaya hakuna "underground media" other than JF, kwa hiyo, hata hao wa "udaku" hawawezi kufanya tathmini ya kina na kubaini ukweli.

Kwa upande mwingine, ninaamini kwamba "kifo" cha Ballali kimeletwa ili kuzima kesi ya ufisadi uliokithiri hapa nchini. Ballali ndiye shahidi mkuu kwenye kesi hiyo.

Jambo moja kubwa la kutatanisha ni uvumi kwamba Ballali ni raia wa Marekani. Kama hili ni kweli, ninashindwa kuamini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliweza kumteua raia wa Marekani kuwa Gavana wa Benki Kuu, kazi ambayo ni nyeti mno?!!! Kulikoni?

Utata utata utata!

Bado kuna utata mwingine, maswali bado ni mengi... suala la Serikali kuhusishwa na maziko ya Ballali, suala la Serikali "kushauriwa" na familia ya "marehemu" kabla ya habari za kifo chake kutangazwa rasmi... Utata utata utata!

./Mwana wa Haki!
 

nani alisema balali hakuwa mfanya kazi wa serikali mpaka umauti unamfika?
 
nani alisema balali hakuwa mfanya kazi wa serikali mpaka umauti unamfika?

si alifukuzwa ajira yake ya udalali pale BOT, au nalo lilikuwa changa la macho. Maana siku hizi hakuna kuingia ndani au kukaa nje unaweza umbuka hivi hiiivi, ilobaki ni kukaa mguu mmoja ndani mwingine nje.
 
Narudia kauli yangu ya awali ktk threads nyengine kuhusu kifo cha balali.
"nilipokuwa mtoto ilikuwa ni rahisi kudanganywa, ila sasa nimekua na sidanganyiki kama mtoto"
Ilipita mwezi hapa since Mzee mwanakijiji aliposema kuwa anahisi Balali amefariki, baadae serikali kwa pupa ikaspeculate news kuwa kafa. Nikajisemea moyoni kuwa serikali imekurupukia hoja za JF. Na ukiangalia mwenendo wa mazishi na speculations zake inatia shaka.

Balali ana duel citizenship sasa mnataka niamini kuwa amekufaaaaa??? Serikali ya ki-secomedy
 
huu ni utata sana, unaweza kukuta hata MAREHEMU alihudhuria kwenye MSIBA/MAZISHI yake!
 
kwa kawaida Paka ni kiumbe mpole anayeishi na watu ndani ya nyumba.
Paka huyo huyo ukimfungia ndani ukaanza kumpiga akakosa pa kutokea utaona makucha yake.

Watanzania tumefungiwa ndani ya giza nene na siri-kali yetu.

Kwanza siri-kali kwa kutumia wizara ya fedha na BOT wametuibia fedha zetu nyingi sana.

Pili wanajitahidi kwa nguvu za fedha zetu kuficha wezi.

Tatu wanatumia fedha zetu kututukana na kutupa lugha za kebehi majibu ya kimatusi na kutuona hamnazo.

Umauti-plastic surgery wa Balali unaonyesha uuwaji wa siri-kali kwa raia wake. Haijawahi kutokea ktk historia mtu mwenye aliyekuwa na wadhifa kama ule kuzikwa na watu wasiojulikana. Kwani kila ambaye nimejaribu kuongea nae ama kwa simu ama kwa mdomo awe karibu ndugu, au balozi wa tz usa hakuna mwenye jibu huyu balali amefariki au la.

Balali yu hai anaishi sehemu isiyojulikana ama anasura nyingine.

Wakati umefika wa kurudisha siri-kali serikalini. Tugeuzi hiki chungu mpaka tuujue ukweli.

Kikwete alipokuja usa kwenye mkutano wa sullivan kati ya dec 11 to 13 alikutana na balali kwa sirikubwa sana. wakati huo Balali alikuwa akiishi kati ya dc na Maryland alikuwa mzima wa afya.

Paka anataka kujitetea.
Bila kwenda ikulu kwa hasira na kudai haki yetu sioni ushindi.
Amani haiji ila kwa ncha ya upanga.
Hakuna maendeleo yalifikiwa kwa kubembelezana.
 
Kweli Hiki Kifo Ni Utata Na Hata Mimi Sijaamini Kwamba Kilitokea, Kwa Sababu Kila Mtu (reliable Sources) Walikuwa Wanaleta Habari Tofauti Kwa Sababu Mpaka Leo Hii Sijui Balali Alifia State Gani? Ukiangalia Habari Za Kifo Chake Sijafahamu Alifia State Au City Gani Kwa Sababu Ndugu Zake Na Serikali Zilitoa Location Tofauti. Na Mpaka Sasa Sijamuona Fmes Na Wenzake Kuongelea Hii Thread, Hopeful Atakuja Na Habari. Na Nilishasema Kwamba Jinsi Jamaa Alivyo Controversial The Least Ambacho Ndugu Zake Wangefanya Ni Kuuonyesha Mwili Kwa Watanzania Woote Na Mwili Ungerudishwa Bongo Watu Waone, Lakini Jinsi Walivyofanya Ni Kuyeyushana Tuu Na Uongo Mtupu. Lakini Ipo Siku Ukweli Utajulikana Tuu
 
Kwenye thread moja niliuliza.... msimamo wa Anna Muganada kwenye hili swala zima uko wapi(Tangu tuhuma zimeanza mpaka kufukuzwa kazi kwa Ballali?
Lol, MwK ina maana Ballali alienda kwa wakwe wake wa zamani kufanyiwa plastic surgery?
 
Admin, pls sticky this thread so that whomever visit JF (including Mafisadi) iwe kifungua kinywa chao kwa mshangao!!
 
[QUOTE=MaMkwe;Aseme nini? Anatafuta umaarufu tu wa kisiasa. Wenzie tunamlilia ndugu yetu yeye anataka kuleta mzaha. Hivi hawa wanasiasa wa Bongo hawajui kifo?

HIVI UNAJUA KWAMBA MBOWE ANA DISTANCE RELATIONSHIP NA LATE GOV.MAANA GOV. MARRIED TO ANNA MUGANDA,WHO IS J.MUGANDA,FORMELY WITH VOA,WHO MARRIED TO FREEMAN SISTER...do a research utaona.just a lil bit of info.amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…