Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Watu walitaka mpaka Hashimu Thabiti ajue Balali kafa ndiyo wamini eeeh!

Pundit wananchi wako desparate kutafuta balozi wao mpya kwasababu wa sasa ameshindwa kazi yake
 
Mbona hakuna mwenye kusema Tanzania Daima ni ya nani?
 
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu peponi hayo masuala ya ufisadi yana muhusu yeye na mola wake

Wewe unataka mungu ampeleke fisadi peponi ili aende kuwaibia akina Nyerere? Kwi kwi kwi!!!
 
Mbona hakuna mwenye kusema Tanzania Daima ni ya nani?

Unauliza swali wakati jibu unalo? Utafiri ni mtihani wa GCSE hapa UK mwaka huu ambapo nyuma ya maswali waliweka majibu? Ingelikuwa Afrika wangetucheka sana. Inakuwaje board nzima ikafanya makosa kama hayo?
 
Kwahiyo mume wa dada yake Freeman ana dada ambaye ndio mke wa Ballali?
Kama ni hivyo kaaazi kweli kweli!
No wonder kuna unaoitwa mgogoro mzito ndani ya CHADEMA makao makuu!
Ndio haya?
 
Wewe unataka mungu ampeleke fisadi peponi ili aende kuwaibia akina Nyerere? Kwi kwi kwi!!!

kwi kwi kwi,

labda anataka aende peponi ili akachapwe viboko na Nyerere asubuhi na jioni kwa siku hamsini na sita (dont ask me why 56 days).
 
Unauliza swali wakati jibu unalo? Utafiri ni mtihani wa GCSE hapa UK mwaka huu ambapo nyuma ya maswali waliweka majibu? Ingelikuwa Afrika wangetucheka sana. Inakuwaje board nzima ikafanya makosa kama hayo?

No mambo huwa yanabadilika sometimes hata umiliki wa kampuni na usijue hadi ufanye uchunguzi!
Najua ilikuwa ya Freeman ila iyo connection ni wasiwasi tu kwasababu kutakuwa na conflict of interests hapo!
 
Sina La Kusema Huwa Nasikia Wakatoliki Wanaimba Mazikoni Ave Ave Maria Jamaa Walikuwa Wanamonita Safi Ndugu Kufika Tu Usa Jamaa Kafa What A Coinsidance?
 
Jmushi umekuwa na tabia ya kubadili sana mada hapa .Sasa hoja iliyoko si hii ambayo wewe unaulizia maswali yako .Hoja ni Yona Maro na mauza uza yake ndiyo issue hapa .TD unataka iwe issue kwa sababu ipi ? Mume ama shemeji pia havina nafasi hapa ika nafasi iko kwa hawa wanaotaka ku twist issues .
 

Dont worry Lunyungu,

Nimekuelewa mkuu wangu!
 
Unauliza swali wakati jibu unalo? Utafiri ni mtihani wa GCSE hapa UK mwaka huu ambapo nyuma ya maswali waliweka majibu? Ingelikuwa Afrika wangetucheka sana. Inakuwaje board nzima ikafanya makosa kama hayo?

Mimi bado nasoma threads na posts zake taratibu sasa ili nijue nia ya maswali yake ambayo mengi ana majibu mwenyewe ni nini hasa!
 


Zote hapo juu ni comment zako!
We umeleta habari halafu unapanga itakavyojadiliwa!
Kwa hiyo si ungeifuta kabisa hiyo kauli ya Maro yenye ku suggest TD ina uhusiano na Ballali?
We na Mtanzania ndio mnanichanganya!
Sasa kinachojadiliwa hapa ni nini haswa?
Maana madai yako kuwa hoja ni ya Maro haijamaanisha kuwa hoja hizo ambazo ni contents za mjadala huu zisijadiliwe!
Ndio maana sipendi siasa na siwapendi wanasiasa!
 

NINA UHAKIKA ASILIMIA 100 BALALI HAJAFA.NAANGALIA TU USANII UNAVYOFANYIKA NA WATU WANARUKIA STORI TU KWA SABABU MTU FLANI KATANGAZA JAMBO,JAMANI AMKENI NDUGU ZANGU
 
usimsahau na Lunyungu aliyekuja na bandiko la FMES kwa sahihi ya shy..

Si umeona vitu? Ameshakuja kutoa maelezo kuwa hii ni email amepokea toka kwa SHY na kumbe Shy alikopi maandishi ya FMES hapa JF.

Asante Kamanda kwenye hili!
 
kwi kwi kwi,

labda anataka aende peponi ili akachapwe viboko na Nyerere asubuhi na jioni kwa siku hamsini na sita (dont ask me why 56 days).

Mie naomba aende AHERA na huko amkute Dito na wavalishwe gauni kama la Adolf Hitler. Kila siku asubuhu wanachora saba na kutumbukiziwamo nanasi...
Huko wamsubiri Mugabe na wale viongozi wa Burma (Mynmar).
 
•
Mwili wa Balali kuchomwa moto leo

*Heshima kutolewa Kanisa la Mtakatifu Stephen
*Ratiba yaonesha ndugu wa karibu tu kuhudhuria

Na Joseph Lugendo

ALIYEKUWA Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Daudi Ballali anazikwa leo mjini Washington DC, Marekani na huenda mwili wake ukachomwa moto kwa mujibu wa taratibu za makaburi anakozikwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika kutoka nchini humo, mwili wa marehemu uliohifadhiwa kwenye nyumba ya maziko ya De-Vol iliyoko mjini humo unatarajiwa kuagwa leo saa 4 asubuhi kwa saa za Marekani katika Kanisa Kuu la St.Stephen Martyr 2436 Pennsylvania Ave,NW Washington, DC 20037.

Heshima za mwisho zitatolewa kanisani hapo baada ya misa na zitahusisha ndugu jamaa na marafiki wa karibu tu na sio hadhara ya mtu yeyote anayetaka kushiriki.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Bw.Ombeni Sefue ataongoza waombolezaji kutoa heshima hizo akifuatiwa na watumishi wa Idara mbalimbali alizowahi kutumikia marehemu Ballali alipokuwa akifanyakazi kwenye Shirika la Fedha Duniani (IMF), ndugu zake waliowasili Marekani siku chache zilizopita na Watanzania wachache wanaoishi Washington DC.

Baada heshima za mwisho mwili huo utapelekwa katika makaburi ya Wakatoliki ya Get of Heaven eneo la Silver Spring, MD. Hata hivyo haijajulikana kama mwili huo utachomwa moto ama utazikwa kiafrika kwa kuteremshwa kaburini kwasababu huduma zote mbili zinakubalika katika makaburi hayo.

Ikiwa atachomwa moto, majivu yake hayataruhusiwa kugawanywa bali yatateremshwa kaburini kwa mujibu wa taratibu za kikatoliki.

Wakati huo huo chanzo chetu kingine kilichokarubu na familia hiyo hapa nchini kilidokeza kwamba mazishi hayo yamesababisha mgawanyiko na mvutano mkubwa ndani ya familia yake.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mvutano huo sasa umeigawa familia hiyo katika makundi makuu mawili yanayopingana.

Mvutano huo umesababishwa na kutokubaliana kulikojitokeza baina ya makundi hayo ya familia juu ya mahali anapopaswa kuzikwa Dkt. Ballali.

Mtoa habari wetu alisema upande unaoongozwa na mke wa marehemu Bi Anna Muganda ulitaka Dkt. Ballali azikwe nchini Marekani alikofia wakati upande wa ndugu zake walitaka mwili wa marehemu urejeshwe nchini kwa maziko.

Akizungumza kwa simu na Majira jana jioni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Patrick Mombo, alisema amezungumza na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani lakini nao haukuwa na habari zozote juu ya mazishi ya Dkt. Ballali.

"Nimezungumza na Balozi, alikuwa akielekea ofisini lakini hakuwa na taarifa zozote za mazishi, sasa hivi kule ni asubuhi, nikipata taarifa yoyote nitakueleza," alisema Balozi Mombo.

Juzi Serikali katika nyakati tofauti ilitoa taarifa rasmi za kifo cha Dkt. Ballali kilichotokea Ijumaa ya wiki iliyopita Mei 16, mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa na Ikulu, Rais Jakaya Kikwete alielezea masikitiko yake juu ya kifo hicho na kuelekeza kuwa taarifa zaidi juu ya mazishi yake zitatokana na uamuzi wa familia yake.

Kwa upande wa BoT, Ofisa Uhusiano Mwandamizi, Bw. Emmanueli Mwero naye alitoa taarifa ya kuthibitisha kifo hicho na kuahidi kutoa taarifa za mara kwa mara juu ya kitakachokuwa kikiendelea.

Watu mbalimbali waliotoa maoni juu ya kifo hicho, licha ya kuitaka Serikali kufanya uchunguzi ili kupata taarifa zaidi pia walipendekeza mwili wake uletwe nchini kwa ajili ya mazishi.

Hata hivyo, kinyume na mtazamo huo wa wananchi, taarifa nyingine zisizo rasmi zilidai kuwa, Dkt. Ballali, enzi za uhai wake alipendekeza kama akifa, mwili wake usiletwe nchini.

Taarifa hizo zilidai kwamba mazishi rasmi ya Dkt. Balali yanatarajiwa kufanyika leo nchini Marekani.

Wakati huo huo serikali imelaumiwa kwa kupiga chenga msiba wa gavana huyo hasa ambaye ndani ya moyo wake alikuwa na taarifa muhimu kuhusu yaliyojiri katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

"Huyu alikuwa ni mtu muhimu hivyo serikali haikupswa kukaa kimya...kwa kweli hili limetusikitisha sana," alisema Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa CUF, Bw. Hamad Rashid Mohamed, alipozungumza na gazeti hili.

Alisema walitegemea serikali ingetoa tamko hasa kwa kuzingatia kuwa gavana anateuliwa na Rais, hivyo hilo ni jukumu la serikali kuueleza umma kuhusu yaliyotokea badala ya kuiachia taasisi.

Bw. Rashid alisema hata kama serikali haikuona umuhimu wa kuwapatia taarifa wananchi basi ilistahili kuwaeleza jinsi ilivyosikitishwa na kifo chake hasa kwa kuzingatia kuwa kimetokea katika kipindi muhimu na uchunguzi ya 'madudu' yaliyotokea ndani ya akaunti ya EPA ukiwa unaendelea.

Alisisitiza kuwa Dkt. Ballali alikuwa na taarifa muhimu kuhusu EPA, hivyo serikali ilipaswa kutolea taarifa kifo hicho. "Watanzania walipaswa kuambiwa tangu kuugua kwake hadi kufariki," alisisitiza.

Alisema inawezekana ameacha wosia na nyaraka mbalimbali hivyo ameitaka serikali kuunda tume ya kuchunguza kifo chake. Ameshauri tume itakayoundwa itoke miongoni mwa wabunge.
 
Slaa: Tume ichunguze kifo cha Daudi Ballali




na Mwandishi Wetu



KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amependekeza kuundwa kwa tume huru ya kimataifa itakayochunguza mazingira ya kifo cha Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa ambaye ni Mbunge wa Karatu, alisema umuhimu wa kuundwa kwa tume hiyo unatokana na utata uliozingira habari zote zinazomhusu Ballali tangu alipoondoka hapa nchini Agosti mwaka jana.

Dk. Slaa, mwanasiasa aliyeibua tuhuma kadhaa dhidi ya Ballali, na mmoja wa wanasiasa waliokuwa mstari wa mbele kutaka kurejeshwa nchini, ili aje kujibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili, ikiwa ni pamoja na kusaidia uchunguzi wa wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT, alisema kifo chake kabla ya kukamilika kwa suala hilo, ni pigo kubwa.

'‘Tunaiomba serikali iunde tume ya kimataifa ili ukweli ujulikane. Huyu ni mtu mkubwa, ana siri nyingi za taifa. Anahusishwa na ufisadi. Hatuwezi tukaliacha suala hili likaachwa hivi hivi tu.

'‘Kama serikali imeficha ugonjwa, hospitali na hata hicho kifo ambacho taarifa zake zimepatikana baada ya siku nne, tunataka tume huru iundwe ihusishe majaji na watu wenye heshima katika jamii ya kimataifa," alisema Slaa.

Mwanasiasa huyo ambaye ndiye aliyesoma orodha ya mafisadi mwaka jana na kuibua mwamko wa kipekee katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi, alirejea kauli aliyopata kuisema siku zilizopita kuhusu Ballali na umuhimu wake wa kumrejesha hapa nchini wakati akiwa hai.

'‘Nilipata kusema huko nyuma, na leo narejea tena kulisema hili kwamba, iwapo Ballali atakufa kabla ya hajarejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi ndani ya BoT na hata kabla hajahojiwa na Kamati ya Mwanasheria Mkuu inayochunguza kashfa ya EPA, basi damu yake itakuwa juu ya serikali," alisema Slaa.

Alisema mwenendo mzima wa namna serikali na Rais Jakaya Kikwete walivyolishughulikia suala zima la Ballali, kuanzia kuondoka kwake kwenda nje kwa matibabu, kulazwa na baadaye kufa, ni jambo linalotia shaka na kuibua maswali mengi.

Mwanasiasa huyo alisema anaamini haiwezekani Ballali, ambaye ugavana wake ulitenguliwa na si kufukuzwa, aende nje kwa matibabu na alazwe pasipo serikali kupitia Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Marekani, kujua mahali aliko.

Alisema anaamini kwamba gharama zote za matibabu ya Ballali zilibebwa na serikali, kwani hata baada ya uteuzi wake wa ugavana kutenguliwa, aliendelea kubakia kuwa mtumishi wa serikali.

'‘Hiki kiini macho cha serikali kudai eti hawajui alikokuwa amelazwa na anakoishi Ballali, ni ushahidi wa wazi kwamba serikali ilikuwa inaficha jambo.

'‘Walikuwa wakijua aliko, na walifanya hivyo wakijua kwamba iwapo angerejea angeweza kutoa siri kwa kuwataja wahusika wengi, na hivyo kuleta mtikisiko mkubwa serikalini," alisema Dk. Slaa.

Aliilaumu serikali kwa kutoa taarifa nyingi zinazokinzana kila mara waandishi wa habari walipokuwa wakifanya juhudi kubwa katika kufuatilia alikokuwa gavana huyo wa zamani wa BoT.

Alisema uamuzi wa serikali kukaa kimya kwa muda mrefu pasipo kutoa taarifa hata baada ya Ballali kufa, ni ushahidi mwingine wa namna ilivyokuwa ikishikwa na kigugumizi kuhusu suala hilo.

'‘Ninachosema hapa ni kwamba, wakati serikali inapotoa majibu yenye utata na yenye kupingana, haijawahi kusimama na kusema aliyeondoka ni mtu wetu, Mtanzania mwenzetu. Ni kwa nini serikali ilikuwa haifuatilii? Kwa nini ubalozi haukufuatilia? Unaweza kuona namna serikali inavyojaribu kuficha jambo," alisema Dk. Slaa.

Alisema ni jambo la ajabu kwamba, maofisa wa ubalozi wamekuwa wakifuatilia kwa karibu kila mara Watanzania wanapokwenda India kwa matibabu ya moyo, tena kwa watu wa kawaida kabisa na hivyo kuzua maswali ni kwa nini kwa Ballali hali ilikuwa ni tofauti.

Kama hiyo haitoshi, Dk. Slaa alieleza kushangazwa na kifo cha Ballali ambacho kimetokea siku chache tu baada ya kuwapo kwa taarifa za makachero kutumwa kumfuatilia nchini Marekani.

'‘Ni jambo lisiloeleweka sawa sawa na linalopaswa kutolewa maelezo. Haiwezekani tunasikia makachero wamekwenda kumfuata na siku chache baadaye kupitia katika mtandao tunaambiwa amefariki na kisha siku chache baadaye inatangazwa rasmi amekufa. Nini kimemuua? Serikali itujibu," alisema.

Alisema huko nyuma na hata katika mtandao kulikuwa na taarifa za mtu huyo kuwekewa sumu, jambo ambalo serikali pamoja na kutakiwa kulitolea ufafanuzi ilikaa kimya.

Alieleza kushangazwa kwake pia na hatua ya Kamati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayochunguza Kashfa ya EPA, kuwahoji watuhumiwa wengine na wamiliki wa kampuni 22, huku ikimuacha shahidi muhimu Ballali, katika muda wote wa miezi karibu mitano ya kazi yao.

'‘Ni kwa nini wanahojiwa akina Jeetu Patel na wengine wa makampuni 22, na hawa watu hawakuteremka BoT kama Roho Mtakatifu. Ninaamini Ballali angekuwapo angeeleza siri hizo," alisema Dk. Slaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…