Mkuu MWK,
1. Nimeupata ujumbe wako na pia ninaheshimu msimamo wako, wa kutoamini kuwa Balali hajafariki, kwanza nitoe heshima kwa wajumbe wote waliochangia hii mada, ninaamini kuwa hii ni moja kati ya best ever ndani ya hii forum, kwa sababu huu ni mjadala ambao umetoa the best out of waananchi, yaani demokrasia at work, pia kuna mivutano imetokea lakini ya jana ni ya jana, leo ni siku mpya.
2. Binafsi bado ninasema kuwa msimamo wangu ni ule ule, kuwa Balali amefariki tena ninaamini kwa 100%, nafikiri sihitaji kurudia sababu, zote nimezitoa, ninajua kuwa msimamo katika maisha sio kitu cha mzaha kama ya kununua samaki sokoni, na ninajua pia kuwa msimamo siku zote ni lazima ujaribiwe kwa njia mbali mbali kuanzia za natural, mpaka un-natural, lakini binadamu imara kama mimi ni msimamo ndio unakupa usingizi safi, kujua kuwa hukuyumba pamoja na all the attacks, kwa sababu unaamini kuwa ulichokuwa unasimamia na kuamini ni ukweli wa Mungu, sio wa binadamu mwingine.
3. Nimetafuta mwenyewe facts za kifo, nimeishia kupata kama 90%, nilichoshindwa ni Tarehe na jina alilolitumia akiwa Hospitali, na ni lazima niwe mkweli kwenye hili kuwa hiki kifo sio your average au as usual one, lakini looking back nimewahi kuona vifo vingi vya aina hii, ingawa this one is different.
Nimeona Waziri Kibona, Gavana Rutihinda, Mzee Mwaikambo, na pia Amina Chifupa wakitangulia kwenye haki under very unusual ways, na pia wakiwa handled baada ya kufa under very same circumstances kama za Balali, lakini bado this one ni for the record kama sio history.
4. Kuna a very strong argument, kuwa marehemu was very bitter kwa kusingiziwa some crimes he did not commit, kama hii ni kweli basi yeye na familia yake wametuangusha sana sisi masikini, kwamba kusoma kote huko majuu na kuweza kufanya kazi kote huko majuuu, tena kwenye mashirika makubwa sana ya dunia, halafu kuja kuishia kuchezewa na wanasiasa wa bongo hawa wahuni wa kutupwa ambao mimi hata wakinipa soda ambayo haijafunguliwa siwezi kuikubali, na kuishia kutangulia kwenye haki bila ya kutufumbulia ukweli ulipo na hata kufanya mambo mengi kama ni ya kweli kwa siri, kwa sababu ya kuwaogopa hawa wahuni kwa kweli inasikitisha sana,
5. Ninaelewa kuwa ameacha ushahidi mzito sana, ninasema hivyo kwa sababu ninajua mengi yanayoendelea behind the scene na hii ishu, lakini nina wasi wasi sana kuwa huenda hata huo ushahidi aliouacha ukawa batili, kama wamefanya haya kwa the originator wa ushahidi. can you imagine watafanya nini kwa messenger wa kuleta huo ushahidi? This is a very sad story kuwaachia watoto wetu wa taifa la kesho, kwa sababu wote tumeona mazingara yaliyomtanguliza Amina, ambaye hakuwemo kwenye EPA wala BOT, sasa kwa nini tuliruhusu this one again? Kwenye hili taifa zima we are guilty sawa huenda tuna akili sana kama tunavyoonyesha humu JF, lakini ukweli ni kwamba bado tuko mbali sana na kwenye kujifunza na makosa, na believe me sasa hivi we are about to do the same na Mkapa, yaani ku-commit the same mistake kama ya Balali, halafu tutanza kutafutana uchawi.
Samahani kwa kuwachosha, lakini ninaomba kusema kuwa kwangu sina wasi wasi kuwa in due time, ukweli utatoka tena wazi na WHYs zote zitajibiwa, na ninaahidi kuwa iwapo itagundulika kuwa Balali hakufariki, basi nitajiuzulu rasmi kujihusiaha na siasa, au any kind of kutoa info kwa wananchi au mtu yoyote mwingine zaidi yangu, na nitajiondoa kabisa kwenye matayarisho yangu ya kuingia kwenye national politics ambako ni the matter of time kabla sijajikita hukona nitasema wazi hapa hapa JF,
Ninaheshimu sana wale wanaoamini kuwa Balali hajafariki, na hasa wale wenye hoja nzito, kwa haya machache ninaomba ku-retire unless ukitokea ushahidi mpya na mzito, lakini otherwise ninawpa heshima wajumbe wote kwa kazi nzito ya kuijadili hii topic, ya jana ya jana sasa tugange yajayo!
JF Mbele!