Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Mkuu MWK,

1. Nimeupata ujumbe wako na pia ninaheshimu msimamo wako, wa kutoamini kuwa Balali hajafariki, kwanza nitoe heshima kwa wajumbe wote waliochangia hii mada, ninaamini kuwa hii ni moja kati ya best ever ndani ya hii forum, kwa sababu huu ni mjadala ambao umetoa the best out of waananchi, yaani demokrasia at work, pia kuna mivutano imetokea lakini ya jana ni ya jana, leo ni siku mpya.

2. Binafsi bado ninasema kuwa msimamo wangu ni ule ule, kuwa Balali amefariki tena ninaamini kwa 100%, nafikiri sihitaji kurudia sababu, zote nimezitoa, ninajua kuwa msimamo katika maisha sio kitu cha mzaha kama ya kununua samaki sokoni, na ninajua pia kuwa msimamo siku zote ni lazima ujaribiwe kwa njia mbali mbali kuanzia za natural, mpaka un-natural, lakini binadamu imara kama mimi ni msimamo ndio unakupa usingizi safi, kujua kuwa hukuyumba pamoja na all the attacks, kwa sababu unaamini kuwa ulichokuwa unasimamia na kuamini ni ukweli wa Mungu, sio wa binadamu mwingine.

3. Nimetafuta mwenyewe facts za kifo, nimeishia kupata kama 90%, nilichoshindwa ni Tarehe na jina alilolitumia akiwa Hospitali, na ni lazima niwe mkweli kwenye hili kuwa hiki kifo sio your average au as usual one, lakini looking back nimewahi kuona vifo vingi vya aina hii, ingawa this one is different.

Nimeona Waziri Kibona, Gavana Rutihinda, Mzee Mwaikambo, na pia Amina Chifupa wakitangulia kwenye haki under very unusual ways, na pia wakiwa handled baada ya kufa under very same circumstances kama za Balali, lakini bado this one ni for the record kama sio history.

4. Kuna a very strong argument, kuwa marehemu was very bitter kwa kusingiziwa some crimes he did not commit, kama hii ni kweli basi yeye na familia yake wametuangusha sana sisi masikini, kwamba kusoma kote huko majuu na kuweza kufanya kazi kote huko majuuu, tena kwenye mashirika makubwa sana ya dunia, halafu kuja kuishia kuchezewa na wanasiasa wa bongo hawa wahuni wa kutupwa ambao mimi hata wakinipa soda ambayo haijafunguliwa siwezi kuikubali, na kuishia kutangulia kwenye haki bila ya kutufumbulia ukweli ulipo na hata kufanya mambo mengi kama ni ya kweli kwa siri, kwa sababu ya kuwaogopa hawa wahuni kwa kweli inasikitisha sana,

5. Ninaelewa kuwa ameacha ushahidi mzito sana, ninasema hivyo kwa sababu ninajua mengi yanayoendelea behind the scene na hii ishu, lakini nina wasi wasi sana kuwa huenda hata huo ushahidi aliouacha ukawa batili, kama wamefanya haya kwa the originator wa ushahidi. can you imagine watafanya nini kwa messenger wa kuleta huo ushahidi? This is a very sad story kuwaachia watoto wetu wa taifa la kesho, kwa sababu wote tumeona mazingara yaliyomtanguliza Amina, ambaye hakuwemo kwenye EPA wala BOT, sasa kwa nini tuliruhusu this one again? Kwenye hili taifa zima we are guilty sawa huenda tuna akili sana kama tunavyoonyesha humu JF, lakini ukweli ni kwamba bado tuko mbali sana na kwenye kujifunza na makosa, na believe me sasa hivi we are about to do the same na Mkapa, yaani ku-commit the same mistake kama ya Balali, halafu tutanza kutafutana uchawi.

Samahani kwa kuwachosha, lakini ninaomba kusema kuwa kwangu sina wasi wasi kuwa in due time, ukweli utatoka tena wazi na WHYs zote zitajibiwa, na ninaahidi kuwa iwapo itagundulika kuwa Balali hakufariki, basi nitajiuzulu rasmi kujihusiaha na siasa, au any kind of kutoa info kwa wananchi au mtu yoyote mwingine zaidi yangu, na nitajiondoa kabisa kwenye matayarisho yangu ya kuingia kwenye national politics ambako ni the matter of time kabla sijajikita hukona nitasema wazi hapa hapa JF,

Ninaheshimu sana wale wanaoamini kuwa Balali hajafariki, na hasa wale wenye hoja nzito, kwa haya machache ninaomba ku-retire unless ukitokea ushahidi mpya na mzito, lakini otherwise ninawpa heshima wajumbe wote kwa kazi nzito ya kuijadili hii topic, ya jana ya jana sasa tugange yajayo!

JF Mbele!

Mkulu FMES,

Hata mimi nimepata ujumbe wako na nimekuelewa. Kitu kimoja labda nikiweke wazi hapa ni kuwa, sidhani kama kuna haja ya wewe kuresign kutoka JF au kwenye siasa kama ikijulikana kuwa Ballali yuko hai.

Kinachotafutwa hapa ni ukweli na nothing but the whole truth. Kama haya mambo yangekuwa straight kama inavyotegemewa kwenye issue kama hizi hapa US, mimi na baadhi ya watu tusingekuwa na haya maswali lukuki.

Ijulikane kuwa mimi niliamini habari hizi na kuzitetea kwa nguvu kwa zaidi ya wiki hapa kabla sijaamua otherwise. Hapa ni swala la kuwekana sawa maana kuna watu wengi nyumbani kwenye media na kwingineko wangependa kufanya uchunguzi huu lakini hawawezi kutokana na sababu mbalimbali.

Kama Ballali amekufa that's fine, kama hajafa that's also fine kwa sababu si tu amepotea ili asipatikane, bali pia inaongeza kazi ambayo sidhani kama inatakiwa ya kumtafuta. Mimi nitahangaika na hao waliobaki. Kwa sasa bado nitazikataa hizi habari za kifo cha Ballali kwa asilimia 95 mpaka nikithibitishiwa otherwise.

Ugomvi wangu sasa unahamia kwa Mramba na Mgonja ambao walidhani kuwa kifo cha Ballali kimemaliza na kufunika uovu wote walioifanyia Tanzania.

Asante na heshima mbele.
 
Tunaomba MJJ ufunge mjadala unaibua hisia tofauti kwa members wa JF kila mtu ashike imani yake.
 
Tunaomba MJJ ufunge mjadala unaibua hisia tofauti kwa members wa JF kila mtu ashike imani yake.

Taratibu mkuu!

Ingawa pia najua kuwa sio kazi ya Mkjj kufunga mijadala hapa, lakini nakuuliza tu kaswali kadogo - Kwa nini mjadala ufungwe?
 
Tunaomba MJJ ufunge mjadala unaibua hisia tofauti kwa members wa JF kila mtu ashike imani yake.

Usiwe na wasiwasi mijadala ya JF hufa kifo cha kawaida.. lakini mingine inatabia ya kufufuka fufuka... halafu mwanzilishi wa hii ni mwafrika... mng'ang'anie yeye..
 
Umenichekesha... maana tunaweza kujikuta tunaanzisha mjadala mwingine kabisa kuhusu kama kweli mjadala umekufa au la..

Duh!! hii imenichekesha sana....
Kwenye hili mimi sina la kuchangia tena kwa hiyo nitaendelea na kufanya kile nikiwezacho nacho ni to have more fun than any human being should be allowed to have.......(btw, Rush has given me the permission to do so...Lol)
 
Duh!! hii imenichekesha sana....
Kwenye hili mimi sina la kuchangia tena kwa hiyo nitaendelea na kufanya kile nikiwezacho nacho ni to have more fun than any human being should be allowed to have.......(btw, Rush has given me the permission to do so...Lol)

sawa bwana.. na mimi amenipa ya jinsi ninavyowajua CCM "like every square inch of my glorious..... "
 
Yaelekea wanaongea uongo mpaka wanajisahau....Mkulo si alidai balali hajulikani aliko??? Nadhani huu ndio mwaka wa shetani kama alivyoimba Amani Temba (Mh.Temba).
 
Yaelekea wanaongea uongo mpaka wanajisahau....Mkulo si alidai balali hajulikani aliko??? Nadhani huu ndio mwaka wa shetani kama alivyoimba Amani Temba (Mh.Temba).

Inakuwaje mtu anapoamini uwongo wake?
 
mbowe alikubali kwamba ballali kafariki na tena akachukua uamuzi wa kuongea kwa niaba ya chama chake, na kusema kwamba wao kama chadema wanaamini, iweje wafuasi wa mbowe wasiamini anachoamini master wao ??
 
Ni haki yangu kuukataa uwongo kama ilivyo wajibu wangu kuukubali ukweli, itakuwa ni makosa makubwa kuukataa ukweli eti kwa vile siupendi- gamba la nyoka
 
Kada Mpinzani
Hii inaonyesha Chadema si chama cha ndiyo bwana. Sorry, nilikuwa nimepumzika huu mjadala lakini I could'nt resist this.
 
mbowe alikubali kwamba ballali kafariki na tena akachukua uamuzi wa kuongea kwa niaba ya chama chake, na kusema kwamba wao kama chadema wanaamini, iweje wafuasi wa mbowe wasiamini anachoamini master wao ??


Sorry Gamba la Nyoka,
I meant Kada Mpinzani. See, I should have stayed away.
 
Kada Mpinzani
Hii inaonyesha Chadema si chama cha ndiyo bwana. Sorry, nilikuwa nimepumzika huu mjadala lakini I could'nt resist this.

ballali-mbowe connection(undugu wao) > mbowe-chadema connection katika hili suala la kufa kwa ballali ! wafuasi wake hawana uhusiano wa kiundugu na ballali even though mbowe did have that undugu with him(ballali)!!
 
Hizi habari nilisema hapa kuwa ni mbinu ya wapinzani kuichafua ccm. Kila kitu wao wanalaumu ccm. pesa za EPA hazikuchukuliwa na ccm kama chama ila wanachama wachache tu wenye tamaa. Ballali amekufa na mwacheni yeye na familia yake sasa wapumzike kwa amani.

Wengine tuendelee na ujenzi wa nchi.
 
Hizi habari nilisema hapa kuwa ni mbinu ya wapinzani kuichafua ccm. Kila kitu wao wanalaumu ccm. pesa za EPA hazikuchukuliwa na ccm kama chama ila wanachama wachache tu wenye tamaa. Ballali amekufa na mwacheni yeye na familia yake sasa wapumzike kwa amani.

Wengine tuendelee na ujenzi wa nchi.

mzee, hii kampeni yao haijaanza jana wala leo, na wataiendeleza milele, mbaya ni kwamba watu washastuka and its never too late wimbi kugeuka na kuwaandama wao !
 
Back
Top Bottom