KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
Mkuu Kada ninachokwambia kuna watu wazembe katika kutekeleza majukumu yao. Mimi ninatolea mfano jinsi uzembe ulivyo na kuonyesha mambo mbali mbali basi tu.
gotcha ! tupo pamoja !
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Kada ninachokwambia kuna watu wazembe katika kutekeleza majukumu yao. Mimi ninatolea mfano jinsi uzembe ulivyo na kuonyesha mambo mbali mbali basi tu.
Watu wanadhani maneno aliyosema mbowe ni ya raha au sijui mahaba ! lakini either way, huyu jamaa ni too much keshasema vya kusema na sasa ni wakati wa yeye kuhojiwa ! kama alikuwa hajui nini alichosema, why even say it ??
usitake kuchanganya madawa ! hayo ya kiwira na hili ni kitu kimoja!(LAKINI NI LAZIMA KWAMBA UFAHAMU NINACHOJARIBU KUSEMA HAPA SIO MAMBO YA KISIASA BALI NI MAMBO YA KITAIFA, KWA MANUFAA YAKO WEE NA YANGU MIMI PIA)....MFANO MZURI USHASEMA WEWE MWENYEWE HUO WA KIWIRA, SASA UTASHANGAA KAMA HAO WAZEE WALIOSHIRIKI WAKIULIWA ILI KUFICHA USHAHIDI WAKATI MBOWE ANAJUA NJIA INAYOTUMIWA KUULIA HAO MAFISADI ? HUONI KWAMBA KAMA MBOWE ATAHOJIWA, TUTAFANIKISHA MAMBO MENGI IKIWA NI PAMOJA NA KUWABANA MAFISADI ZAIDI NA ZAIDI ?? hao wa kiwira bado wapo hai right, sasa unaonaje kama mbowe akihojiwa ili ithibitike njia inayotumiwa kuuliwa hao viongozi ili mafisadi zaidi na zaidi wasiuliwe na mwishowe wahojiwe na hatimae kugundua ukweli !
kama atahojiwa unasema ndio utaona serikali inafanya kazi hapo nakuunga mkono maana we are for the same course, kutaka mbowe ahojiwe ili kuonyesha serikali inafanya kazi na hao mafisadi waliobaki watahojiwa na sio kusikia leo au kesho fisadi fulani aliyedaiwa kushiriki kwenye mgodi wa kiwira kafa ! sasa hapo tutalalamika tena kwamba tumepigwa changa la macho au ??
natumai utaelewa !
gotcha ! tupo pamoja !
Umakini wa Mbowe kwenye siasa nautilia mashaka. Anachanganya mambo yake ya familia na CHADEMA, hilo ni kosa kubwa.
Kama hili alijua Ballali yuko wapi, lakini akaamua kukaa kimya wakati wanasiasa
wenzake wa upinzani wangependa kujua Ballali yuko wapi ili kumuumbua.
Kwenye kifo kawa wa kwanza kuambiwa na kawa wa kwanza kusema anaamini kweli kafa. Sasa anaanza kusema serikali imemuua, hapo naona anatudanganya Watanzania.
Kada hiyo proposal achana nayo, narudia achana na mbowe shugulikieni mafisadi tu.
Kitu kikubwa kinachohatarisha amani ya nchi yetu ni mafisadi/wezi uchwara. washauri jamaa zako wachukuwe hatua katika hilo la ujambazi, baada ya hapo kila kitu kitakuwa solved na hautasikia maneno mazito kama uliyoyasikia.
Bwana KADA MPINZANI huyu Mbowe hana sera na kwa kuwa hilo gazeti la Tanzani daima ni mali yake basi amekuwa akiongea anavyotaka lakini nafikiri sasa wakati umefika kwa usalama wa taifa kufanya kazi yake.
KadaMchafu huna maana, kwani ww unaongea upupu tu..sina la ziada maana najiskia hasira kuona fisadi akitamba hapa JF..
Mbowe atoa kauli nzito kifo cha Ballali
na Lucy Ngowi Tanzania Daima~Sauti ya Watu
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Daudi Ballali kina mkono wa baadhi ya vigogo wa serikali, kwa sababu alikuwa shahidi muhimu katika vita ya ufisadi.
Alisema kuna kitendawili kinachotegwa sasa na baadhi ya vigogo wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwa Ballali alikuwa shahidi muhimu sana katika vita ya ufisadi aliyodai kufanywa na chama tawala.
Kuteketea kwa Ballali, tutaamini kuna mkono mchafu wa baadhi ya viongozi wa serikali, kwa sababu ni shahidi muhimu katika vita ya ufisadi. Wasifikiri kufa kwa Ballali, ndiyo mwisho wa mapambano, lakini nawaambia ndiyo kwanza vita ya ufisadi itapamba moto.
Ufisadi na mchezo mchafu wa CCM, umewatesa watoto wetu, wazazi wetu na sasa basi, tutapambana hadi watakapouana wote waishe. Wamemuua Ballali, Amina Chifupa wataendelea kuuana, alisema mwenyekiti huyo.
EPA ni sehemu tu, pesa nyingine hazijaundiwa tume. Tunamwambia Rais Kikwete, utawala wake kwa miaka miwili iliyobakia utakuwa ni wa kuunda tume tu. Wamemwondoa Ballali kwa sababu ndani ya Ballali, kuna mambo mengi yaliyofichika, alisisitiza.
Kada!
Hivi Ngoja nikukumbushe Kada kuna siku ulisema unamtetea JEET PATEL hivi ni kweli? kama ni kweli then naona mantiki yako ya kutaka mbowe ahojiwe
hahahaaaaa. am loving it !
Kifo cha Ballali kwa kweli wengi waTanzania tunaamini kuna wingu ndani yake.
Lakini Mbowe alivyoongelea hapo juu highlighted aidha he was ill advised or mis quoted by reporter...kwa sababu mjue sasa Serikali na CCM watakuja juu na kupinga na watatishia kwenda mahakamani...hii ndio itakuwa big story na watu kusahau hoja kuu UFISADI.......mark my word kuanzia kesho media,vijiweni na hapa JF issue itakuwa Mbowe Vs Establishment.........wananchi wanachotaka ni kuwa mafisadi wafichuliwe waletwe kwenye vyombo vya dola na kuwajibishwa lakini siyo ku grab frontpage.
Sasa mbona hujajibu maana nitamalizia kwamba unataka kutufanya tutoke kwenye EPA maana wewe unaweza kupoteza mengi.
KUna Matatizo gani ya kuwa na issue ya MBowe VS establishment? Mbowe ni mpiganaji na lazima apambane na ufisadi wa ccm kila mara unapojitokeza.
Post yangu inasema na ina maana kwa kauli aliyotoa Mbowe...
butty camp hiyooooooooo..........!
Umejitahidi sana... imekuchukua dakika karibu 63 kabla hujaanza kuandika utumbo na pumba. Hii ni JF, ufisadi na utetezi wake hauna nafasi.
Endelea na butty camp maana hicho tu ndicho unaweza kusema na sio kutetea ufisadi.
Kwi kwi kwi...
I luuuuuuuv JF.
kwani uongo ! nenda booty camp ! unahitajika huko ! pumba zako kalishe mbuzi !