Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kwi kwi kwi!!! mbona tumesikia dada zake wakisema? Mimi nafikiri Jasusi ni mwanaume kwahiyo huwezi kuwa mmoja wa dada zake Balali.

Naweza kukutafutia statements kibao za ndugu zake Ballali. Kwa Anna Muganda atasema nini wakati na yeye yumo kwenye list ya mafisadi?

Sijaona mahali ambapo dada zake wamesema kitu. Nirushie basi tuendelee kukata issue.
 
Jasusi,

Mimi niko nawe kwenye hili na ninaamini kuwa yanayokuja ni makubwa na yatakuja haraka kuliko inavyodhaniwa.

That will be great MWK. Mwenzako mie as days passby the line between optimism and pessimism is becoming thiner than thicker; hope I am wrong. But then the whole thing, whenever it comes out, maybe too little and too late! Lest we forget, timeliness is the greatest determinant of success and this is particularly true in politics.
 
Kitila,
Aliyesema ukweli utajulikana ni mimi. Hayo ni maoni yangu binafsi. Msinijumlishe kwenye kundi eti ndugu zake Balali wameanza kusema. Hawajasema kitu. Anna hajasema kitu.
Kama ni madongo nirushieni mimi mwana JF I can take it. But leave the rest of them alone. This applies to you too Mtanzania.

Jasusi pole sana kama hii imekulenga. Ila kombora lako limetokana na piece ile kutoka kule Tanzanite na magazeti ya nyumbani. Nafikiri utakuwa ulisoma kwenye Tanzania Daima na magazeti mengine yaliyowanakiri baadhi ya ndugu za Balali huko Washington DC wakisema kuwa ndugu zake wataongea. Tena walisema walikuwa na mpango wa kuongea na waandishi wa habari ili kuweka mambo wazi kuhusu ufisadi wa BoT na chanzo cha kifo chake lakini wakaonywa waache, au umesahau hii habari ambayo nafikiri pia ilipostiwa hapa JF?
 
That will be great MWK. Mwenzako mie as days passby the line between optimism and pessimism is becoming thiner than thicker; hope I am wrong. But then the whole thing, whenever it comes out, maybe too little and too late! Lest we forget, timeliness is the greatest determinant of success and this is particularly true in politics.

Kitila,

The whole thing ina maswali mengi zaidi kuliko majibu.... kitu kimoja nimegundua katika pitapita yangu ni kuwa, hata kama kuna mtu au kundi la watu linacheza mchezo wa kuigiza hapa, nia yake(o) ni kuchukua muda wangu na wengine hapa kuhangaika kujua kama Ballali amekufa or not badala ya kujua kile ambacho Ballali alitakiwa kusema kuhusu wizi wa BoT.

Kuna wakati Kocha maarufu kwenye college basketball hapa US - Coach K wa Duke aliwahi kuhojiwa aeleze ni kwa nini wakati fulani anaruhusu timu pinzani kufunga au kuongoza kwa muda kabla hajaleta mashambulizi ya hakika na yenye ushindi dk za mwisho na kumnyima mpinzani nafasi ya kusawazisha, jibu lake lilikuwa rahisi sana:

Kwa sababu naweza - ( Because I can!) - huku akicheka.....

So far, that's all I can say on this issue......
 
Kinachoshangaza ni kwamba hakuna hata mmoja wetu(watanzania) aliye pata hata picha ya mazishi jamani, Us ni mbali sana, sasa sisi tulioko huku nyumbani yaaani ni utata jamani, yaaani mzee wetu kazikwa kama si mzaliwa wa taifa letu hili la tanzania, tena gavana wetu,aaaaaaaaaa!!!!!! inasikitisha sana jamani,

Mkumbuke kwamba mzee wetu hakuwa mkimbizi, hizi tuhuma tuu alikuwa nazo hakuna uthibitisho wowote, ni kwanini mmemzika huko jamani?
 
Isaya,

mafisadi wengi wanakufa na kuzikwa kama yatima... kumbuka Mobutu na Amini
 
Mkuu Jasusi,

Soma hizi links mbili, kuna zingine pia na tumejadili hata hapa JF.

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/22/habari1.php

http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/5/23/index.php

Mtanzania,
Hujaprove chochote. Dada zake Balali hawajasema kitu. Katika ile thread ya 5/22 jamaa wa familia aliyezungumza na Tanzania Daima ni mimi.
Katika hiyo thread ya 5/23 inaonyesha bayana kwamba dada zake Gavana "walishauriwa" wasiseme kitu. Kwa hiyo madongo bado nirushieni mimi. Dada zake Gavana hawajasema kitu na kama nielewavyo kwa sasa hawatasema kitu.
 
Jasusi pole sana kama hii imekulenga. Ila kombora lako limetokana na piece ile kutoka kule Tanzanite na magazeti ya nyumbani. Nafikiri utakuwa ulisoma kwenye Tanzania Daima na magazeti mengine yaliyowanakiri baadhi ya ndugu za Balali huko Washington DC wakisema kuwa ndugu zake wataongea. Tena walisema walikuwa na mpango wa kuongea na waandishi wa habari ili kuweka mambo wazi kuhusu ufisadi wa BoT na chanzo cha kifo chake lakini wakaonywa waache, au umesahau hii habari ambayo nafikiri pia ilipostiwa hapa JF?

Kitila,
Ni kweli kulikuwa na mpango wa kutoa family statement baada ya simu za waandishi habari kuzidi kutuandama. Lakini baada ya kikao cha familia ilionekana wazi kuwa chochote tutakachosema hatutaweza kunyamazisha maswali na tetesi za watu. Ikaamuliwa wasiseme kitu. Wamesharudi Dar na sijasikia lolote katika magazeti ya Bongo---au labda kesho?
 
Mtanzania,
Hujaprove chochote. Dada zake Balali hawajasema kitu. Katika ile thread ya 5/22 jamaa wa familia aliyezungumza na Tanzania Daima ni mimi.
Katika hiyo thread ya 5/23 inaonyesha bayana kwamba dada zake Gavana "walishauriwa" wasiseme kitu. Kwa hiyo madongo bado nirushieni mimi. Dada zake Gavana hawajasema kitu na kama nielewavyo kwa sasa hawatasema kitu.

Jasusi,

Nashukuru sana kwa ufafanuzi kwamba wewe ndio source ya habari za Tanzania Daima.

Sina matatizo na wewe maana tumetoka mbali pamoja katika haya mapambano na mafisadi.

Kama ambavyo nimewahi andika mara nyingi, mafisadi ni ndugu zetu, ni kaka zetu, dada zetu, waume zetu, wake zetu, watoto zetu nk. Ni muhimu kuendelea kukemea ufisadi hata kama unawahusu watu wa karibu na sisi.

Lengo hapa ni Ballali na wala sio familia yake.
 
Kutokana na taarifa iliyopo kwenye gazeti la Raia Mwema, Marehemu Balalli aliacha wosia wa kimaandishi kuhusu mchoro mzima wa EPA na kina nani waliokuwa wanashinikiza.
Gazeti kinaendelea kusema kuwa maelezo haya aliwapatia watu wapatao watano ikiwa pamoja na wanasiasa na wanasheria.
Upatikanaji wa nyaraka hii utasaidia kufumbua fumbo hili.
 
Unaposema anaongea irresponsibly una maana gani?

Na pia unaposema kwa karne hii Chama hiki hakiwezi ongoza nchi pia una maana gani? Ama umeridhishwa na jinsi ambavyo tunaongozwa na Serikali ya Kifisadi ya Awamu ya Nne?

Mzozo wa mizozo swali lako limetulia,

Ninaposema kuwa anaongea irresponsible ninamaanisha kuwa unapowaambia watu kuwa wanaishi kwenye hatari ni vyema uwaelezee kwa mapana na marefu juu ya hiyo hatari. Ni sawa na mtu anayemwambia jirani yake ndani kwako kuna nyoka kaingia, bila kumuelezea ukubwa wa nyoka mwenyewe, ameingia saa ngapi na may be kumshauri jinsi ya kumshughulikia huyo nyoka.
Mbowe aliposema kuwa serikali ya CCM inauwa watu, kwa njia nyingine alikuwa anatoa vitisho kwa wale wote wanaotaka kuipinga serikali hiyo kuwa nao wanaweza kuuliwa wakati wowote. Hivyo basi alikuwa responsible kuelezea kwa mapana na marefu jinsi alivyopata taarifa za mauaji hayo na kuwashauri wale wote wanaoipinga serikali hiyo wafanye nini ili kuepukana na kuuliwa.

Ninaposema kuwa chama hiki kwa karne hii hakiwezi kuongoza nchi sizungumzii CCM bali ninazungumzia CHADEMA. Nadhani unazifahamu sera za CHADEMA na vizuri. Ukisikiliza msingi wa muundo wa serikali ambayo CHADEMA inaamini ndio unaweza kuleta maendeleo utaona waziwazi kuwa chama hiki kwa karne hakiko kwenye hesabu ya vyama vinavyoweza kuongoza nchi.
CHADEMA wanaamini kuwa ili waweze kuleta maendeleo Tanzania inabidi kuwe na majimbo ambayo kuundwa kwake kutahusisha kuondoa cheo cha Rais wa Zanzibar! Kwa sera hii tu ambayo viongozi wa chama wamedhikirika kukosa makadirio ya muda unaohitajika kuitekeleza, hakuna haja hata ya kuangalia sera nyingine bila kujua kuwa CHADEMA uongozi wa taifa kwa karne hii hawauwezi. Ila kama nilivyoandika sehemu nyingi, CHADEMA ni chama ambacho kimeonyesha ushirikiano mzuri na waandishi wa habari na wananchi katika kufichua ufisadi. Sasa tufamu kuwa kufichua ufisadi haimaanishi kuwa tayari kuongoza nchi.
Ili CHADEMA iwe tayari kuongoza nchi kwanza kabisa inabidi itupilie mbali sera ya majimbo au at least ifute ndoto za kuondoa cheo cha Rais wa Zanzibar.
 
Kutokana na taarifa iliyopo kwenye gazeti la Raia Mwema, Marehemu Balalli aliacha wosia wa kimaandishi kuhusu mchoro mzima wa EPA na kina nani waliokuwa wanashinikiza.
Gazeti kinaendelea kusema kuwa maelezo haya aliwapatia watu wapatao watano ikiwa pamoja na wanasiasa na wanasheria.
Upatikanaji wa nyaraka hii utasaidia kufumbua fumbo hili.

Hawa inatakiwa watusaidie hili tuweze kujua hasa hasa ni nani aliyetuingiza mjini. Hii itakuwa taarifa muhimu sana. Hivi hawajulikani waliopewa taharifa? Nafikiri kama wakili Mkono ameipata inaweza kuwa vigumu kuipata.
 
Mzozo wa mizozo swali lako limetulia,

Ninaposema kuwa anaongea irresponsible ninamaanisha kuwa unapowaambia watu kuwa wanaishi kwenye hatari ni vyema uwaelezee kwa mapana na marefu juu ya hiyo hatari. Ni sawa na mtu anayemwambia jirani yake ndani kwako kuna nyoka kaingia, bila kumuelezea ukubwa wa nyoka mwenyewe, ameingia saa ngapi na may be kumshauri jinsi ya kumshughulikia huyo nyoka.
Mbowe aliposema kuwa serikali ya CCM inauwa watu, kwa njia nyingine alikuwa anatoa vitisho kwa wale wote wanaotaka kuipinga serikali hiyo kuwa nao wanaweza kuuliwa wakati wowote. Hivyo basi alikuwa responsible kuelezea kwa mapana na marefu jinsi alivyopata taarifa za mauaji hayo na kuwashauri wale wote wanaoipinga serikali hiyo wafanye nini ili kuepukana na kuuliwa.

Ina maana wewe unabisha kuwa watu hawaishi kwa hatari hapo Tanzania na wakati wowote wanaweza kufa kutokana na sera mbovu za ccm?

Ninaposema kuwa chama hiki kwa karne hii hakiwezi kuongoza nchi sizungumzii CCM bali ninazungumzia CHADEMA. Nadhani unazifahamu sera za CHADEMA na vizuri. Ukisikiliza msingi wa muundo wa serikali ambayo CHADEMA inaamini ndio unaweza kuleta maendeleo utaona waziwazi kuwa chama hiki kwa karne hakiko kwenye hesabu ya vyama vinavyoweza kuongoza nchi.
CHADEMA wanaamini kuwa ili waweze kuleta maendeleo Tanzania inabidi kuwe na majimbo ambayo kuundwa kwake kutahusisha kuondoa cheo cha Rais wa Zanzibar! Kwa sera hii tu ambayo viongozi wa chama wamedhikirika kukosa makadirio ya muda unaohitajika kuitekeleza, hakuna haja hata ya kuangalia sera nyingine bila kujua kuwa CHADEMA uongozi wa taifa kwa karne hii hawauwezi.

CCM wakiacha wizi wa pesa BoT na wakaendesha uchaguzi halali na haki bila kutisha wananchi na kuua watu kwa kutumia jeshi na polisi wanaweza kushindwa kwenye uchaguzi.

Ila kama nilivyoandika sehemu nyingi, CHADEMA ni chama ambacho kimeonyesha ushirikiano mzuri na waandishi wa habari na wananchi katika kufichua ufisadi. Sasa tufamu kuwa kufichua ufisadi haimaanishi kuwa tayari kuongoza nchi.
Ili CHADEMA iwe tayari kuongoza nchi kwanza kabisa inabidi itupilie mbali sera ya majimbo au at least ifute ndoto za kuondoa cheo cha Rais wa Zanzibar.

Haya ni mawazo yako na so far yatachukuliwa hivyo. Chadema wanafaa mara mia zaidi kuongoza nchi zaidi ya ccm ambao wamefilisi na kuuza nchi kwa wageni kwa visingizio vya uwekezaji na ujasiriamali.
 
Originally, Kada alikuwa Chadema au upinzani, baadaye akahamia upande wa pili baada ya kuudhiwa na watu huko, sasa eti amedhaminiwa na ccm? Kwa hiyo ina maana zamani alikuwa amedhaminiwa na upinzani?

Hivi Mkuu Umeangalia vizuri?

Kada ukichambua vizuri alisha andika kuwa yeye anamwakilisha JP, sasa JP anayemwakilisha sasa(Kulingana na alichokiandika zamani) ndiyo CCM?
 
Hawa inatakiwa watusaidie hili tuweze kujua hasa hasa ni nani aliyetuingiza mjini. Hii itakuwa taarifa muhimu sana. Hivi hawajulikani waliopewa taharifa? Nafikiri kama wakili Mkono ameipata inaweza kuwa vigumu kuipata.

Ukisoma vizuri stori hii, inaonekana Gazeti hili linawajua waliopewa nyaraka hizo. Ingekuwa vizuri lingewataja majina ili kutoa shikinizo la kuwafanya wahusika watoe tamko.
Haya mambo ya kuongea kwa mafumbo hayatusaidii.
 
Ina maana wewe unabisha kuwa watu hawaishi kwa hatari hapo Tanzania na wakati wowote wanaweza kufa kutokana na sera mbovu za ccm?

CCM wakiacha wizi wa pesa BoT na wakaendesha uchaguzi halali na haki bila kutisha wananchi na kuua watu kwa kutumia jeshi na polisi wanaweza kushindwa kwenye uchaguzi.

Haya ni mawazo yako na so far yatachukuliwa hivyo. Chadema wanafaa mara mia zaidi kuongoza nchi zaidi ya ccm ambao wamefilisi na kuuza nchi kwa wageni kwa visingizio vya uwekezaji na ujasiriamali.

Mjadala haukuwa sera ni madai yaliyotolewa na mwenyekiti wa chadema kuwa serikali ya CCM inauwa watu na nilichosema ni kwamba ameongea irresponsibly, kwa kuwa hakutoa ufafanuzi wala ushahidi wa alichosema. Jifikiria ungekuwa ni member wa family ya Amina Chifupa halafu unamsikia Mbowe anasema kuwa ndugu yako ameuliwa na serikali,ungekuwa katika hali gani?

Najua kuwa mambo mengi ninayosema hayako shared na chadema, ndio maana wanabaki walipo.
 
Najua kuwa mawazo haya hayako shared na chadema, ndio maana wanabaki walipo.

siku za ufisadi na wizi wa ccm zinahesabiwa. Wewe endelea kuamini kuwa chadema wamebaki walipo kwa dhana kuwa ccm itaendelea kuiba kura milele.

Taratibu tu kila kitu kinawekwa wazi na itakuwa kazi kuiba kura kama yaliyompata Mugabe.
 
Unachosema kina ukweli, lakini ili kitokee ni LAZIMA kufanyike mabadiliko makubwa ya kisera na kiitikadi ndani ya chadema.

CCM haiko madarakani kwa sababu ya wizi wa kura.
 
Dk. Ballali kuumbua vigogo (Raiamwema)

Mwandishi Wetu Mei 21, 2008

Wosia wake wataja walioshinikiza EPA

Wanasiasa, wanasheria wauhifadhi

KIFO cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Timoth Said Ballali (65) kinazidi kuibua mambo mengi, sasa waliokuwa karibu naye wanataka undani wa wosia aliouandika kwa mkono wake na maelezo aliyoandika alipohojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuondoka nchini kwenda Marekani, uanikwe.

Watu mbalimbali walio karibu na familia ya Ballali, wakiwamo wanasiasa na wanasheria, waliozungumza na Raia Mwema wiki hii, wamesema ni wakati mwafaka kwa sasa mambo yote aliyoyaacha gavana huyo wa zamani yawekwe wazi ili kuondoa utata kwamba kuna jambo linalofichwa.

Wakati hayo yakiendelea, habari zinasema kwamba kuna mkakati maalumu wa kuhakikisha kwamba siri ya waraka huo haitolewi hadharani na baadhi ya watu mashuhuri wamethubutu kusafiri hadi nchini Marekani kufanikisha mkakati huo bila kujua mengi zaidi yapo nyumbani Tanzania.

Akizungumza na Raia Mwema wiki hii, mwanasheria mmoja mashuhuri amesema anafahamu na ameuona waraka aliouandika Ballali kwa mkono wake akielezea mambo mengi ya msingi aliyotuhumiwa nayo ikiwamo lile sakata la fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) uliokuwa ukisimamiwa na BoT, ambako zaidi ya Sh. bilioni 133 zinadaiwa kupotea.

"Ballali aliandika kwa mkono bila kupigwa chapa mambo yote yaliyotokea ambayo anatuhumiwa kuyafanya kama mhalifu na amewataja watu wote kwa majina na muda bila kuacha katika waraka wake huo ambao ameweka saini na kuhitimisha kwa alama za vidole," anasema mwanasheria huyo ambaye hajawahi kutajwa popote kuwa na mahusiano na Ballali wala BoT.

Maelezo ya mwanasheria huyo yameshabihiana karibu kwa kila kitu na Mbunge mmoja wa Upinzani ambaye pia ni mmoja wa viongozi muhimu katika kambi ya upinzani ambaye naye amekiri kuuona waraka. Mwanasiasa huyo hakukiri wala kukanusha kuwa na nakala ya waraka huo wa Ballali.

Wote wawili wanasema kwamba waraka huo unaweza ama uko mikononi mwa watu zaidi ya watano wakiwamo wanasheria, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa sasa na wa zamani, wanasiasa wawili wa kambi ya upinzani na baadhi ya wanafamilia na hivyo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kuubadili ama kuuficha "milele"..

Kwa mujibu wa habari hizo, sehemu ya waraka huo inaelezwa kuelezea kwa kina kuhusu nini hasa kilichofanyika hadi BoT ikaidhinisha kutolewa kwa kiasi cha Sh bilioni 133/- na Ballali anaeleza kwa uwazi wahusika wote wakuu wakiwamo viongozi wa juu wa Serikali na wanasiasa walioshinikiza na waliochukua sehemu kubwa ya fedha za EPA pamoja na watendaji wa BoT walioshiriki katika zoezi hilo.

Waraka huo ambao kwa sasa unatafutwa kwa udi na uvumba unadhihirisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Serikali kutokana na baadhi ya wahusika muhimu wanaotajwa na Ballali kutozungumzwa popote linapozungumzwa suala la EPA na hata katika vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa waliouona waraka huo wa wosia, Ballali, kwa mfano, anaeleza jinsi alivyosita kuidhinisha malipo ya Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ambayo pekee ilikabidhiwa kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh. bilioni 40/-) kwa kutumia nyaraka za kughushi.

"Ballali ameeleza katika waraka ule kwamba alikataa kuidhinisha malipo hayo akielezea jinsi isivyo sahihi kutumia nyaraka za kughushi lakini aliitwa na mwanasiasa mmoja akiwa na mwanasiasa mwingine mkongwe mwenye ushawishi hadi sasa ambako aliamrishwa kuidhinisha malipo hayo mara moja.

"Unajua alivyoitwa aliwaeleza athari za kutumia nyaraka za kughushi wakamlazimisha na baada ya kuona wanamlazimisha akawaambia kama BoT itaidhinisha basi mtu anayatakiwa kukabidhiwa fedha hizo hastahili kwa kuwa kuna fedha nyingine zaidi ya Dola za milioni 60 alizotakiwa kurejesha kwanza kabla ya kukabidhiwa fedha zozote, lakini akalazimishwa kumlipa huyo huyo," anasema mwanasheria aliyezungumza na Raia Mwema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara huyo ambaye ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania alikuwa akiwasiliana na wanasiasa waliomshinikiza Ballali amlipe kiasi cha kumpigia simu Ballali kabla hata ya kuondoka viwanja vya majengo alikokutana nao.

"Unajua inatisha kwani Ballali anasema katika waraka wake huo kwamba alipotoka tu kuzungumza na wazee wale kabla hata ya kuondoka akapigiwa simu na mfanyabiashara huyo akimuuliza kama alikwisha kupata maelekezo na yeye kumtaka aende ofisini ambako atakutana na msaidizi wake ambaye ndiye anayeshughulikia fedha za EPA," anasema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara aliyekabidhiwa fedha hizo ana uhusiano wa karibu sana kibiashara na kijamii na ofisa wa BoT aliyehusika pia na sehemu ya mchakato wa EPA, jambo ambalo limeelezwa kwamba linazidi kuibua utata baada ya wote wawili kutotajwa popote katika sakata hilo.

"Sijasikia popote huyo ofisa wa BoT akitajwa maana hata nafasi ya ugavana alikuwa akitajwa kuwa anaweza kupewa lakini bahati ndiyo akateuliwa Profesa Benno Ndulu, maana angeteuliwa (anamtaja jina) mambo yangeendelea kuwa mabaya zaidi na siri nyingi zingefichwa lakini sasa najua mambo yatajulikana tu," anasema.

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inatajwa kuchota zaidi ya Sh. bilioni 40/- hadi sasa haijulikani ilipo pamoja na kuwapo madai kwamba ilikabidhiwa kwa mfanyabiashara mmoja mwenye kashfa nyingi nchini ili ionekane kuwa ni ya kwake lakini hadi sasa haijaelezwa bayana hasa ni mali ya nani.

Kampuni hiyo kwa kumbukumbu za Msajili wa Makampuni (BRELA) inaonyeshwa kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina kampuni tofauti jirani lakini namba hiyo haionekani na kinachoonekana ni viwanja kuanzia Plot 77 na hata Plot 86 na Plot 88 katika eneo hilo maarufu la viwanda lakini plot ilipo Kagoda haionekani popote.

Aliyesimamia na kufuatilia BoT na hatimaye chukua fedha za kampuni hiyo katika Benki ya CRDB Limited tawi la Azikiwe anajulikana waziwazi na wafanyakazi wa maeneo hayo, lakini kumbukumbu zake zinaelezwa kupotea ama kufichwa na wahusika kwa nia ya kuwasaidia watuhumiwa ama kwa sababu za kichunguzi.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba wapelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwisha kuchukua nyaraka zote muhimu ikiwa ni pamoja na kadi ya benki iliyotumika kufungulia akaunti tawi la Azikiwe, ikiwa na picha na saini za wahusika wote muhimu kwa uhakika zaidi.

Sakata la BoT na zaidi akaunti ya EPA lilichukua sura mpya baada ya kuelezwa kwamba sasa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha fedha zote kiasi cha Sh. bilioni 133 zinarejeshwa kabla ya kuchukuliwa hatua kwa wale waliofanya makosa ya kijinai katika kupata fedha hizo.

Imeelezwa katika hali ya kutatanisha tayari hata fedha kutoka kwa wamiliki wa Kagoda nazo zimekwishakuanza kurejeshwa japo kwa awamu, jambo linalodhihirisha kwamba Serikali inawafahamu kwa hakika kabisa wamiliki wa Kagoda na inawaficha ama inataka kuwalinda kwa sababu za kisiasa zaidi.

Katika uchunguzi wa awali wa mkaguzi wa nje, Samuel Sithole wa kampuni ya kimataifa ya Deloitte & Touche tawi la Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo "nyeti" ya kiusalama.

Hata hivyo, siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na Gavana Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo ambaye sasa ameachwa nje ya Baraza la Mawaziri.

Baada ya kifo cha Ballali sasa inaelezwa kwamba uchunguzi unaoendelea dhidi ya wanaotajwa kuchukua fedha za EPA unaweza kufungwa kwa kuwa shahidi muhimu atakuwa hawezi kutoa maelezo yake mahakamani jambo ambalo linaelezwa kuweza kuichafua zaidi serikali.

Ballali ambaye amefariki dunia akiwa nchini Marekani na kuzikwa huko huko anaelezwa kuondoka na siri nzito ikiwa ni pamoja na mazingira ya kuondoka kwake, kuugua na hata kifo kumkuta huku serikali ikiendelea ‘kuweweseka' na ‘kutapatapa' kutokana mkanganyiko mkubwa wa yaliyomsibu gavana huyo wa zamani.

Hata mahali na siku aliyofariki Ballali ni mambo yaliyoelezwa kuwa na utata hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba alifia Boston, huku wengine wakisema alifia nyumbani kwake Washington DC Ijumaa ya Mei 16, 2008 na baadaye taarifa zake kutangazwa Jumanne usiku ikiwa ni siku tano baadaye, huku baadhi wakianza kudai kwamba alifariki Jumapili ya Mei 18, 2008. Hata mazishi yake yalifanywa kuwa siri na ni wanafamilia wachache tu waliobahatika kuuona mwili wake Jumanne Mei 20, 2008.

Mwili wa marehemu Ballali ulihifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko Washington DC, kabla ya ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC. Kanisa hilo lipo 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037 na baadaye kuzikwa kwa faragha katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, Maryland.

Pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali, hasa magazeti na kutangazwa majukwaani, Ballali hakuwahi kushtakiwa rasmi pamoja na kuwapo taarifa kwamba aliwahi kuhojiwa na TAKUKURU.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.

"Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti," alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.

Aliongeza Warioba: "Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.

"Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.

"Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.

"Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.

" Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika."

Ballali ambaye ameacha mke na familia, amekuwa akitamka wazi kwamba hajawahi kuiba hata senti moja ya umma katika kipindi chote akiwa BoT na kuwashutumu watu ‘aliowakwamisha' kuwa chanzo cha kuandamwa kwake na tuhuma mbalimbali kabla ya kukataliwa kujiuzulu na hatimaye uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Marehemu Ballali alijiunga na Benki kama Gavana Julai 14, 1998 hadi Januari 8, 2008.

Ballali alikwenda ghafla nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana akiwa na nia ya kurejea nchini, alikwama huko baada ya kubainika na matatizo makubwa tumboni kabla ya kulazwa hospitali na kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Kwa mujibu wa habari za awali, Ballali aliieleza familia yake kwamba alikuwa akihofia kula kitu chenye madhara makubwa hasa baada ya madaktari wa Marekani kumfanyia uchunguzi mara tu alipowasili nchini humo, madhara ambayo alionyesha kuhisi kuyapata alipokuwa nyumbani hasa kati ya miji ya Dar es Salaan na Dodoma.

Wakati akiendelea na matibabu, Ballali aliandika barua kuelezea nia yake ya kuomba kujiuzulu kutokana na kuendelea kuzorota kwa afya yake huku akiwa bado na majukumu mazito ya kusimamia uchumi wa Taifa.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za upande wa Serikali kuthibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Ballali siku kadhaa kabla ya serikali kutangaza matokeo ya ukaguzi wa kampuni ya nje iliyopewa kazi ya kukagua hesabu za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kupitia ripoti ya wakaguzi hao, ndipo alipotamka kumfuta kazi Ballali bila kuzungumzia lolote kuhusu kujiuzulu kwake.
 
Back
Top Bottom