Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Mjadala haukuwa sera ni madai yaliyotolewa na mwenyekiti wa chadema kuwa serikali ya CCM inauwa watu na nilichosema ni kwamba ameongea irresponsibly, kwa kuwa hakutoa ufafanuzi wala ushahidi wa alichosema. Jifikiria ungekuwa ni member wa family ya Amina Chifupa halafu unamsikia Mbowe anasema kuwa ndugu yako ameuliwa na serikali,ungekuwa katika hali gani?

Mimi nina ndugu na marafiki Tanzania ambao wanakufa kila siku kwa kukosa madawa na huduma za kueleweka za usafiri na afya kutokana na wizi wa serikali ya ccm. Katika hili nikisikia mtu amesema kuwa ndugu yangu ameuliwa na serikali sitashangaa.

Najua kuwa mambo mengi ninayosema hayako shared na chadema, ndio maana wanabaki walipo.

Haya ni maoni ya Kingunge Ngombale Mwiru kwa hiyo sishangai wewe kuyatoa
 
Unachosema kina ukweli, lakini ili kitokee ni LAZIMA kufanyike mabadiliko makubwa ya kisera na kiitikadi ndani ya chadema.

CCM haiko madarakani kwa sababu ya wizi wa kura.

Najua utaendelea kukana hili kama mzee wetu kule Zimbabwe ambaye hadi leo anaamini kuwa Mungu ndiye kamuweka madarakani ili "awalinde" wazim
 
Dk. Ballali kuumbua vigogo (Raiamwema)

Mwandishi Wetu Mei 21, 2008

Wosia wake wataja walioshinikiza EPA

Wanasiasa, wanasheria wauhifadhi

KIFO cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Timoth Said Ballali (65) kinazidi kuibua mambo mengi, sasa waliokuwa karibu naye wanataka undani wa wosia aliouandika kwa mkono wake na maelezo aliyoandika alipohojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuondoka nchini kwenda Marekani, uanikwe.



Watu mbalimbali walio karibu na familia ya Ballali, wakiwamo wanasiasa na wanasheria, waliozungumza na Raia Mwema wiki hii, wamesema ni wakati mwafaka kwa sasa mambo yote aliyoyaacha gavana huyo wa zamani yawekwe wazi ili kuondoa utata kwamba kuna jambo linalofichwa.

Wakati hayo yakiendelea, habari zinasema kwamba kuna mkakati maalumu wa kuhakikisha kwamba siri ya waraka huo haitolewi hadharani na baadhi ya watu mashuhuri wamethubutu kusafiri hadi nchini Marekani kufanikisha mkakati huo bila kujua mengi zaidi yapo nyumbani Tanzania.

Akizungumza na Raia Mwema wiki hii, mwanasheria mmoja mashuhuri amesema anafahamu na ameuona waraka aliouandika Ballali kwa mkono wake akielezea mambo mengi ya msingi aliyotuhumiwa nayo ikiwamo lile sakata la fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) uliokuwa ukisimamiwa na BoT, ambako zaidi ya Sh. bilioni 133 zinadaiwa kupotea.

“Ballali aliandika kwa mkono bila kupigwa chapa mambo yote yaliyotokea ambayo anatuhumiwa kuyafanya kama mhalifu na amewataja watu wote kwa majina na muda bila kuacha katika waraka wake huo ambao ameweka saini na kuhitimisha kwa alama za vidole,” anasema mwanasheria huyo ambaye hajawahi kutajwa popote kuwa na mahusiano na Ballali wala BoT.

Maelezo ya mwanasheria huyo yameshabihiana karibu kwa kila kitu na Mbunge mmoja wa Upinzani ambaye pia ni mmoja wa viongozi muhimu katika kambi ya upinzani ambaye naye amekiri kuuona waraka. Mwanasiasa huyo hakukiri wala kukanusha kuwa na nakala ya waraka huo wa Ballali.

Wote wawili wanasema kwamba waraka huo unaweza ama uko mikononi mwa watu zaidi ya watano wakiwamo wanasheria, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa sasa na wa zamani, wanasiasa wawili wa kambi ya upinzani na baadhi ya wanafamilia na hivyo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kuubadili ama kuuficha “milele”..

Kwa mujibu wa habari hizo, sehemu ya waraka huo inaelezwa kuelezea kwa kina kuhusu nini hasa kilichofanyika hadi BoT ikaidhinisha kutolewa kwa kiasi cha Sh bilioni 133/- na Ballali anaeleza kwa uwazi wahusika wote wakuu wakiwamo viongozi wa juu wa Serikali na wanasiasa walioshinikiza na waliochukua sehemu kubwa ya fedha za EPA pamoja na watendaji wa BoT walioshiriki katika zoezi hilo.

Waraka huo ambao kwa sasa unatafutwa kwa udi na uvumba unadhihirisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Serikali kutokana na baadhi ya wahusika muhimu wanaotajwa na Ballali kutozungumzwa popote linapozungumzwa suala la EPA na hata katika vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa waliouona waraka huo wa wosia, Ballali, kwa mfano, anaeleza jinsi alivyosita kuidhinisha malipo ya Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ambayo pekee ilikabidhiwa kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh. bilioni 40/-) kwa kutumia nyaraka za kughushi.

“Ballali ameeleza katika waraka ule kwamba alikataa kuidhinisha malipo hayo akielezea jinsi isivyo sahihi kutumia nyaraka za kughushi lakini aliitwa na mwanasiasa mmoja akiwa na mwanasiasa mwingine mkongwe mwenye ushawishi hadi sasa ambako aliamrishwa kuidhinisha malipo hayo mara moja.

“Unajua alivyoitwa aliwaeleza athari za kutumia nyaraka za kughushi wakamlazimisha na baada ya kuona wanamlazimisha akawaambia kama BoT itaidhinisha basi mtu anayatakiwa kukabidhiwa fedha hizo hastahili kwa kuwa kuna fedha nyingine zaidi ya Dola za milioni 60 alizotakiwa kurejesha kwanza kabla ya kukabidhiwa fedha zozote, lakini akalazimishwa kumlipa huyo huyo,” anasema mwanasheria aliyezungumza na Raia Mwema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara huyo ambaye ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania alikuwa akiwasiliana na wanasiasa waliomshinikiza Ballali amlipe kiasi cha kumpigia simu Ballali kabla hata ya kuondoka viwanja vya majengo alikokutana nao.

“Unajua inatisha kwani Ballali anasema katika waraka wake huo kwamba alipotoka tu kuzungumza na wazee wale kabla hata ya kuondoka akapigiwa simu na mfanyabiashara huyo akimuuliza kama alikwisha kupata maelekezo na yeye kumtaka aende ofisini ambako atakutana na msaidizi wake ambaye ndiye anayeshughulikia fedha za EPA,” anasema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara aliyekabidhiwa fedha hizo ana uhusiano wa karibu sana kibiashara na kijamii na ofisa wa BoT aliyehusika pia na sehemu ya mchakato wa EPA, jambo ambalo limeelezwa kwamba linazidi kuibua utata baada ya wote wawili kutotajwa popote katika sakata hilo.

“Sijasikia popote huyo ofisa wa BoT akitajwa maana hata nafasi ya ugavana alikuwa akitajwa kuwa anaweza kupewa lakini bahati ndiyo akateuliwa Profesa Benno Ndulu, maana angeteuliwa (anamtaja jina) mambo yangeendelea kuwa mabaya zaidi na siri nyingi zingefichwa lakini sasa najua mambo yatajulikana tu,” anasema.

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inatajwa kuchota zaidi ya Sh. bilioni 40/- hadi sasa haijulikani ilipo pamoja na kuwapo madai kwamba ilikabidhiwa kwa mfanyabiashara mmoja mwenye kashfa nyingi nchini ili ionekane kuwa ni ya kwake lakini hadi sasa haijaelezwa bayana hasa ni mali ya nani.

Kampuni hiyo kwa kumbukumbu za Msajili wa Makampuni (BRELA) inaonyeshwa kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina kampuni tofauti jirani lakini namba hiyo haionekani na kinachoonekana ni viwanja kuanzia Plot 77 na hata Plot 86 na Plot 88 katika eneo hilo maarufu la viwanda lakini plot ilipo Kagoda haionekani popote.

Aliyesimamia na kufuatilia BoT na hatimaye chukua fedha za kampuni hiyo katika Benki ya CRDB Limited tawi la Azikiwe anajulikana waziwazi na wafanyakazi wa maeneo hayo, lakini kumbukumbu zake zinaelezwa kupotea ama kufichwa na wahusika kwa nia ya kuwasaidia watuhumiwa ama kwa sababu za kichunguzi.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba wapelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwisha kuchukua nyaraka zote muhimu ikiwa ni pamoja na kadi ya benki iliyotumika kufungulia akaunti tawi la Azikiwe, ikiwa na picha na saini za wahusika wote muhimu kwa uhakika zaidi.

Sakata la BoT na zaidi akaunti ya EPA lilichukua sura mpya baada ya kuelezwa kwamba sasa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha fedha zote kiasi cha Sh. bilioni 133 zinarejeshwa kabla ya kuchukuliwa hatua kwa wale waliofanya makosa ya kijinai katika kupata fedha hizo.

Imeelezwa katika hali ya kutatanisha tayari hata fedha kutoka kwa wamiliki wa Kagoda nazo zimekwishakuanza kurejeshwa japo kwa awamu, jambo linalodhihirisha kwamba Serikali inawafahamu kwa hakika kabisa wamiliki wa Kagoda na inawaficha ama inataka kuwalinda kwa sababu za kisiasa zaidi.

Katika uchunguzi wa awali wa mkaguzi wa nje, Samuel Sithole wa kampuni ya kimataifa ya Deloitte & Touche tawi la Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo “nyeti” ya kiusalama.

Hata hivyo, siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na Gavana Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo ambaye sasa ameachwa nje ya Baraza la Mawaziri.

Baada ya kifo cha Ballali sasa inaelezwa kwamba uchunguzi unaoendelea dhidi ya wanaotajwa kuchukua fedha za EPA unaweza kufungwa kwa kuwa shahidi muhimu atakuwa hawezi kutoa maelezo yake mahakamani jambo ambalo linaelezwa kuweza kuichafua zaidi serikali.

Ballali ambaye amefariki dunia akiwa nchini Marekani na kuzikwa huko huko anaelezwa kuondoka na siri nzito ikiwa ni pamoja na mazingira ya kuondoka kwake, kuugua na hata kifo kumkuta huku serikali ikiendelea ‘kuweweseka’ na ‘kutapatapa’ kutokana mkanganyiko mkubwa wa yaliyomsibu gavana huyo wa zamani.

Hata mahali na siku aliyofariki Ballali ni mambo yaliyoelezwa kuwa na utata hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba alifia Boston, huku wengine wakisema alifia nyumbani kwake Washington DC Ijumaa ya Mei 16, 2008 na baadaye taarifa zake kutangazwa Jumanne usiku ikiwa ni siku tano baadaye, huku baadhi wakianza kudai kwamba alifariki Jumapili ya Mei 18, 2008. Hata mazishi yake yalifanywa kuwa siri na ni wanafamilia wachache tu waliobahatika kuuona mwili wake Jumanne Mei 20, 2008.

Mwili wa marehemu Ballali ulihifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko Washington DC, kabla ya ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC. Kanisa hilo lipo 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037 na baadaye kuzikwa kwa faragha katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, Maryland.

Pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali, hasa magazeti na kutangazwa majukwaani, Ballali hakuwahi kushtakiwa rasmi pamoja na kuwapo taarifa kwamba aliwahi kuhojiwa na TAKUKURU.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.

“Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti,” alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.

Aliongeza Warioba: “Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.

“Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.

“Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.

“Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.

“ Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika.”

Ballali ambaye ameacha mke na familia, amekuwa akitamka wazi kwamba hajawahi kuiba hata senti moja ya umma katika kipindi chote akiwa BoT na kuwashutumu watu ‘aliowakwamisha’ kuwa chanzo cha kuandamwa kwake na tuhuma mbalimbali kabla ya kukataliwa kujiuzulu na hatimaye uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete.





Marehemu Ballali alijiunga na Benki kama Gavana Julai 14, 1998 hadi Januari 8, 2008.

Ballali alikwenda ghafla nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana akiwa na nia ya kurejea nchini, alikwama huko baada ya kubainika na matatizo makubwa tumboni kabla ya kulazwa hospitali na kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Kwa mujibu wa habari za awali, Ballali aliieleza familia yake kwamba alikuwa akihofia kula kitu chenye madhara makubwa hasa baada ya madaktari wa Marekani kumfanyia uchunguzi mara tu alipowasili nchini humo, madhara ambayo alionyesha kuhisi kuyapata alipokuwa nyumbani hasa kati ya miji ya Dar es Salaan na Dodoma.

Wakati akiendelea na matibabu, Ballali aliandika barua kuelezea nia yake ya kuomba kujiuzulu kutokana na kuendelea kuzorota kwa afya yake huku akiwa bado na majukumu mazito ya kusimamia uchumi wa Taifa.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za upande wa Serikali kuthibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Ballali siku kadhaa kabla ya serikali kutangaza matokeo ya ukaguzi wa kampuni ya nje iliyopewa kazi ya kukagua hesabu za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kupitia ripoti ya wakaguzi hao, ndipo alipotamka kumfuta kazi Ballali bila kuzungumzia lolote kuhusu kujiuzulu kwake.

Taratibu tu kitaeleweka kama hii game inaenda overtime au inakwisha ndani ya robo nne.
 
Mimi nina ndugu na marafiki Tanzania ambao wanakufa kila siku kwa kukosa madawa na huduma za kueleweka za usafiri na afya kutokana na wizi wa serikali ya ccm. Katika hili nikisikia mtu amesema kuwa ndugu yangu ameuliwa na serikali sitashangaa


Kwa hiyo Mbowe aliposema serikali imewauwa Balali na Amina alimaanisha kuwa imesabababisha wakose dawa?

Kingunge is one very smart Tanzanian, Muulize Mbowe juu ya hili.
 
Mtanzania,
Umeisoma hii? Nimesema kuwa serikali imekuwa inazungumza from both sides of its mouth. Leo wanasema hili kesho lile. Sasa wanamwita shahidi muhimu baada ya kifo chake kwa sababu wanafikiri hakuna ushahidi tena. I have confidence in Raiamwema and this article is timely.
 
Ukisoma vizuri stori hii, inaonekana Gazeti hili linawajua waliopewa nyaraka hizo. Ingekuwa vizuri lingewataja majina ili kutoa shikinizo la kuwafanya wahusika watoe tamko.
Haya mambo ya kuongea kwa mafumbo hayatusaidii.

Hapana. Mimi nisingependa watajwe majina kwa sasa kwani Makachero bado wanatafuta watu wowote walio na ushahidi. Sitaki yawapate..........
 
Kwa hiyo Mbowe aliposema serikali imewauwa Balali na Amina alimaanisha kuwa imesabababisha wakose dawa?

Kingunge is one very smart Tanzanian, Muulize Mbowe juu ya hili.

Definition yoyote utakayoweka kwenye hili utarudi bado kuwa wameuliwa. Sikushangai ukimsifia fisadi kuwa ni smart.... just show all your colors
 
Definition yoyote utakayoweka kwenye hili utarudi bado kuwa wameuliwa. Sikushangai ukimsifia fisadi kuwa ni smart.... just show all your colors


Naona umeanza kuonyesha dalili za uvivu wa kufikiria.
Unaweza kuonyesha ufisadi wowote wa Kingunge?
 
Naona umeanza kuonyesha dalili za uvivu wa kufikiria. Unaweza kuonyesha ufisadi wowote wa Kingunge?

ukianza maneno ya kejeli haitabadili unachosema kuwa points...

Ufisadi wa kingunge... let me see... vipi tukianza na parking system...

mengine nitakuletea kadri tunavyoendelea hapa.
 
ukianza maneno ya kejeli haitabadili unachosema kuwa points...

Ufisadi wa kingunge... let me see... vipi tukianza na parking system...

mengine nitakuletea kadri tunavyoendelea hapa.

Simzungumzii mtoto wa Kingunge, namzungumzia Kingunge mwenyewe.
 
Nadhani labda tukubaliane tu kuwa mimi na wewe tuna mitazamo tofauti juu ya uwezo na mwelekeo wa vyama vya upinzani. Na pia juu ya kauli mbalimbali za viongozi wa vyama hivyo, in this case kauli ya Mbowe.

Sio lazima sote tuwe na fikra sawa.

Asante kwa changamoto uliyotoa.
 
Hapana. Mimi nisingependa watajwe majina kwa sasa kwani Makachero bado wanatafuta watu wowote walio na ushahidi. Sitaki yawapate..........

Wanawatafuta wenye ushahidi ili wawanyamazishe au ili wapate evidence kupata ufumbuzi?
 
Kifo cha Balali: Tusimzingizie Mungu!

Lula wa Ndali-Mwananzela Mei 21, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

WANADAMU ni wa ajabu sana. Na maajabu yao huyaonyesha pale wanapojikuta wanabanwa kutoa maelezo ya jambo wasilolielewa au wanalokwepa kulielewa.

Hivyo wanadamu mara nyingi katika historia yetu, tumejikuta tukidai matukio ya asili ya ulimwengu kuwa ni vitendo vya "miungu" au "mizimu". Hivyo ngurumo za radi zikasemwa ni "miungu wanagombana" na radi "mungu anatupiga picha" na vitu kama hivyo.

Hata hivyo, tunapopata ujuzi zaidi ndivyo maelezo yetu yanavyobadilika. Baada ya kujifunza kuhusu umeme basi tumeweza kuelewa radi ni nini na ngurumo ni nini.

Linapokuja suala la kifo, hata hivyo, hatuna ujuzi wa kutosha lakini tunafahamu kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100, sote tutakufa. Hakuna mtu ambaye ni mjanja, mwenye pesa zaidi au mwenye akili zaidi ambaye ameweza kukipiga chenga kifo, na hakuna fisadi aliyekubuhu ambaye anaweza kukipa rushwa. Hata hivyo, japo ni kweli kuwa sote tutakufa mara, sababu za vifo ni nyingi na za namna mbalimbali.

Linapokuja suala la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Dk. Daudi Balali aliyeripotiwa kufa Mei 16, 2008 na kuzikwa wiki moja baadaye, tunajikuta tunahoji kifo chenyewe. Kuna baadhi ya watu ambao wanahoji "kwanini afe kabla ya kukamatwa" na wengine wanaouliza "kwanini afe wakati uchunguzi unakaribia kukamilika"? Na wapo wale ambao wamezua hadithi kuwa Ballali amekufa kwa sumu na ya kuwa watu wanaohusika ni watu fulani ambao wana "sifa hizi na zile". Kuna wengine ambao wanaamini Ballali hajafa kabisa na yuko "Argentina kwenye ufukwe wa bahari akinywa Margarita na kutumbua fedha yake".

Sitazungumza sana kuhusu mambo yale ambayo yamekwisha kuzungumzwa na wengine, lakini moja ambalo sina budi kulizungumza leo ni hili; Watanzania tuache kumsingizia Mungu vifo ambavyo tunajua maelezo yake. Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya Ballali, Rais Jakaya Kikwete alisema hivi (kati ya aliyosema) "Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia. Ni kazi ya Mungu haina makosa."

Maneno haya kwa kuyaangalia kwa haraka yana ukweli lakini tukiyaangalia kwa kuliangalia tukio lenyewe tunajikuta tunakabiliwa na swali muhimu kama kweli tulichoshuhudia ni kazi ya Mungu au ni kazi ya wanadamu. Kumsingizia Mungu na kumbebesha lawama ya uzembe au makosa ya wanadamu si tu ni kukufuru lakini kwa kweli ni kukejeli akili za wanadamu. Haiwezekani mtu afe kutokana na uzembe au mkono wa mwanadamu mwingine halafu sisi tumsingizie Mungu. Hilo haliwezekani.

Sasa msinidhanie kuwa nimesema Serikali au mtu fulani kamuua Ballali. Ninachosema, hata hivyo, ni kuwa ni vigumu kuamini kuwa kifo cha Dk. Ballali kilitokana na kazi ya Mungu ambayo "haina makosa". Inakuwaje kama waliokosea ni binadamu? Hiyo ndiyo hoja yangu leo.

Utata uliozunguka kuondoka, ugonjwa, matibabu na hatimaye kifo cha Dk. Ballali kunaweza kumfanya hata mtoto mdogo kuuliza "nini tatizo". Alipokufa Waziri Mkuu Edward Sokoine, tuliambiwa alikuwa anatoka wapi, alifia wapi, na mauti yalimkuta katika mazingira gani. Na zaidi ya yote tunakumbuka zile picha za Mwalimu Julius Nyerere kuangalia mwili wa Sokoine na kuangusha machozi. Hawakutuficha. Kama watu wote waliamini habari hizo hilo ni suala jingine.

Alipokufa Baba wa Taifa tuliambiwa ameondoka lini, na amekwenda wapi, amelazwa wapi na ugonjwa uliompata. Na kwa kadiri siku alivyokuwa hospitalini tuliambiwa nani amemtembelea na tulipata salamu zake pia. Na hata siku alipokufa tulitangaziwa kama Taifa kuwa kiongozi muasisi wa Taifa amefariki dunia. Wenye maswali walikuwa nayo; mbona hatukuwahi kusikia Nyerere anaumwa leukemia? Nyerere alikuwa anafanyiwa uchunguzi kila mwaka iweje ndani ya miezi mitatu tu wagundue ana kansa ya damu ambayo si kama unaambukizwa leo kesho unaanza kuugua na baadaye kufa? Lakini hatukuuliza maswali hayo mengi kwa sababu viongozi wetu hawakutuficha walijaribu kuja na kutupa taarifa.

Katika mifano hiyo miwili ya viongozi wa kitaifa waliokuwa madarakani walikuwa na ujasiri wa kulipa taifa habari na hawakuacha maneno ya njama na shuku yaenee. Nakumbuka Mwalimu ilimbidi atumie muda wa ziada kuwahakikishia wananchi kuwa kweli Sokoine amekufa katika ajali hasa baada ya kila aina ya "misukule" ilikuwa ikitajwa kuonekana karibu kila kona ya nchi.

Lakini linapokuja suala la Dk. Ballali Serikali ilikuja na sera ya ajabu ambayo haijawahi kushuhudiwa nchini ; sera ya ukimya na utata! Hakuna wakati ambapo Watanzania wamepewa habari zisizokuwa habari kuhusu mtu mmoja kama wakati huu.

Kwanza kabisa Serikali haikusema ni lini Ballali aliondoka nchini baada ya kuitwa Dodoma. Tulichoambiwa ni kuwa Ballali "ameondoka kwa matibabu" kwenda Boston, Marekani. Sasa hapo ndipo utata ulipoanza. Ballali alianza kuumwa lini na aliondoka lini kwenda Marekani. Alipoondoka alikuwa katika hali gani? Kwenye machela, alikimbizwa kwa ndege maalum, au aliondoka kwa kutembea mwenyewe kama alivyofanya Mwalimu? Serikali ikakaa kimya na kusema "kaenda Boston". Wakataka tuwaamini.

Mara ikaja hoja huko Boston amepelekwa hospitali gani kwa hayo matibabu. Serikali ikaanza kutupiana mpira, "yuko Boston kwa matibabu" lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kuwaambia Watanzania Ballali amelazwa hospitali gani. Sababu kubwa ni kuwa wangetaja hospitali kuna watu wangejaribu kufuatilia. Hawakutaka kusema hivyo. Kwa nini? Jibu ni jepesi; Ballali hakupelekwa Boston kwenye hospitali yoyote ile.

Jambo la tatu ni kuwa wamewachukulia Watanzania wengi kuwa hawajui. Ballali alilazwa kwa muda gani kwenye hiyo hospitali (iwe Boston au kwingineko)? Kwa muda mrefu wamewaacha watu waamini kuwa Ballali "amelazwa". Ukweli wa mambo ni kuwa ni hospitali chache sana zinazomlaza mtu zaidi ya wiki moja. Hospitali za Marekani kama hauna sababu ya kukaa hospitali watakuondoa kwani ni gharama kubwa sana. Mara nyingi wanajitahidi kuhakikisha wagonjwa wanaondoka mapema wanapopata nafuu na zaidi ya yote mashirika mengi ya Bima yana kauli katika tiba anayopewa mgonjwa.

Tuliambiwa kuwa Bima yake kutoka Benki Kuu ndio walikuwa wanamlipia. Sasa hawa ndio wa kuwauliza walikuwa wanalipia kwenye hospitali gani na kwa kiasi gani na kwa muda gani. Ninachoweza kusema pasipo kuwa na wasiwasi sana ni kuwa hao waliokuwa wanalipa hizo fedha walikuwa hawazilipi kwenye taasisi inayoeleweka.

Aidha, walikuwa wanalipa kwa mtu binafsi ambaye anadaiwa kuzipeleka pesa huko hospitali au walikuwa wanamlipa Ballali moja kwa moja kwa kisingio kuwa atapeleka fedha hizo kwa hiyo taasisi. Kina Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Salva Rweyemamu hapa hawatasema, kwani sera yao ni utata na ukimya. Kama kweli wanataka tuamini kilichotokea ni kazi ya Mungu basi waseme "nani alikuwa anapokea fedha za matibabu ya Ballali huko "Boston"?

Jambo la nne la sera ya utata na ukimya ya Serikali linakuja baada ya muda pale Serikali ilipopata usahaulifu wa ghafla. Walipoanza kuulizwa tena kuhusu Ballali waliotakiwa kujua wakaja na kusema kuwa "hawajui alipo". Lakini wakati wanasema hivi tukasikia kuwa Ballali ameonana na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, ambaye naye alipoulizwa Ballali alipo na yeye akapata usahaulifu wa ghafla. Wote waliosema walimtembelea Ballali "hospitali" hawakumbuki ni hospitali gani walikomtembelea. Wanatutaka tuamini tu.

Kilele cha usahaulifu huo kilitokea wiki chache zilizopita wakati Waziri wa Fedha Mustafa Mkullo alipodai kuwa na yeye alienda Washington DC na alijaribu "kumtafuta" Ballali bila mafanikio. Tukiwa bado midomo yetu imeachama kwa mshangao saa chache baadaye msemaji wa Ikulu akaja na kuwaambia wananchi kuwa hawajui Ballali aliko na ni mtu huru na ya kuwa serikali haimtafuti "kwa sasa" na kama wakitaka kumpata wanaweza kumpata kwani "serikali ina mkono mrefu". Tukasema well Ikulu has spoken. Binafsi nilisikia kuchanganyikiwa, sasa kama walikuwa hawajui aliko wataanza wapi kumtafuta?

Mara siku chacha baadaye swali likaulizwa kwenye mtandao kama Ballali yuko hai au amekufa? Wakati swali hili linatafutiwa majibu siku mbili baadaye Ballali anafariki. Cha kushangaza ni kuwa hakuna mtu aliyejua kuwa Ballali amekufa hadi siku ya Jumanne! Wale waliokuwa wanajua wakaiminya hiyo habari kwa siku hizo zote. Na hata habari zilipotoka zikawa ziko juu juu tu, amekufa kwa ugonjwa gani, amefia wapi n.k Kwa vile watu waliambiwa kuwa Ballali yuko Boston kwa matibabu basi inawezekana kuwa Ballali amefia Boston.

Hili la kufia Boston likarudiwa katika salamu za rambirambi za pole kwa wanafamilia. Cha kushangaza ni kuwa taarifa nyingine za uhakika kabisa zikaja na kusema Ballali amefia nyumbani kwake, hakufia hospitalini kama watu walivyoambiwa. Miye nikajiuliza ni nani aliyempa habari Rais kuwa Ballali amefia Boston? Maana hii inanikumbusha stori ya "mapanki" na "kampuni ya rada inamilikiwa na serikali ya Uingereza". Hivi hakuna mtu anayeweza kuthibitisha kauli zinazotolewa na Rais hadharani? Hivi ikijakuonyeshwa kuwa Ballali kafia nyumbani si Rais wetu ataonekana kituko? Serikali iseme sasa au inyamaze milele; Ballali amefia wapi?

Kabla hawajajibu wakumbuke kuwa kama amefia Boston Jimbo la Massachussets na baadaye kwenda kuzikwa Washington DC watahitaji kuonyesha (a) jinsi gani mwili ulisafirishwa kutoka jimbo moja kwenda jingine (majimbo haya si kama mikoa yetu) na zaidi ya yote alipofia huko Boston mwili ulishughulikiwa na nani? Wakumbuke pia kuwa umbali toka Boston hadi DC ni karibu maili 400 ambayo ni sawa na kilometa 630 hivi. Umbali huu ni sawa na kutoka Pugu hadi Itigi.

Waliusafirisha mwili kwa njia gani? Vinginevyo Serikali isahihishe tamko lake kuhusu wapi Ballali alifia. Kama waliweza kutuambia kuwa Nyerere alifia hospitali ya St. Thomas pale Uingereza nina uhakika wanauwezo kabisa wa kutuambia Ballali alifia wapi na mahali pekee ambapo wanaweza kusema ni "nyumbani" kwani hawawezi kudai amefia hospitali ambayo haina jina. Mwaiona ngondoo hiyo, mwafunga milango!

Sasa naweza kuendelea na kuhoji mambo mengine mengi yanayohusiana na utata wa jambo hili. Ninachotaka kusema ni kuwa kifo cha Ballali kina utata wa ajabu kiasi kwamba ni vigumu kuamini kuwa kweli kafa au tumepigwa changa la macho. Hakuna kitu chochote kinachoweza kuthibitisha kuwa Ballali kweli kafa akiwa amegubikwa na wingu la kashfa kubwa zaidi au ndio wametuchorea picha ya mlango ukutani na kututaka tutoke nje wajue nani kichaa?

Utata wa "kifo" cha Ballali umeletwa na Serikali na inajua sababu zake. Usiri na kufichana na baadaye kutuambia kuwa ni kazi ya Mungu ni vitu vya kushangaza. Hii kazi ya Mungu tusiihoji sasa? Je kila kifo ni kazi ya Mungu? Kama ni hivyo kwa nini tunapelekana mahakamani mtu akimuua mwanadamu mwingine? Kwa nini Ukiwaona Ditopile alifunguliwa kesi wakati kilichotokea ni "kazi ya Mungu". Ni hatari sana kuchanganya kazi za wanadamu na kazi za Mungu vinginevyo tutahalalisha uhalifu hivi hivi!

Labda niwakumbushe maneno ya Rais Kikwete mwenyewe. Alipozungumza Machi 13, 2006 kwenye ile semina ya elekezi kule Ngurdoto kati ya mengi aliyoyasema, alisema hivi kuhusu majukumu ya viongozi "Siri ya kufanikiwa kufanya hayo ni kwa sisi viongozi kuwa tayari kufanya uchambuzi wa ukweli kuhusu hali ilivyo na kuwa tayari kukiri mapungufu... Kiongozi mzuri ni yule ambaye yuko tayari kujikosoa na kukosolewa."

Kama hilo halikutosha kwenye semina hiyo hiyo Rais Kikwete akaongeza na kusema maneno ambayo naamini leo hii ameyageuka "..sisi kama viongozi na watendaji wakuu wa Serikali iliyochaguliwa kidemokrasia tunao wajibu wakati wote wa kuwafahamisha wale waliotuchagua mambo yote muhimu tunayoyafanya kwa ajili yao. Huu ni wajibu wa msingi ambao hatuwezi kuukwepa kwa vile ni sehemu ya uwajibikaji kwa umma. Utekelezaji wake utasaidia sana kuimarisha hadhi, heshima na uhalali wa Serikali machoni mwa wananchi na utaifanya Serikali iaminike zaidi. Vyombo vya habari vipo kwa ajili hiyo. Tuvitumie."

Vyombo vya habari vimebembeleza kupewa taarifa za uwazi na ukweli kuhusu Serikali yao lakini inaonekana wameamua kuendesha Serikali kama genge la watunzao siri. Kimsingi alichokisema ndicho kinatokea sasa hivi, kwani hadhi, heshima na uhalali wa Serikali machoni pa wananchi umeanza kutiwa uchafu. Ni Jukumu la Serikali kuwa wa kweli na kukubali makosa na mapungufu yao badala ya kujifanya watu wasiokosea.

Imetosha kudanganyana, Serikali isimame kusema kweli, Ballali alilazwa wapi, jimbo gani, amefia wapi na jimbo gani, na alikufa lini? Vinginevyo nimeanza kupoteza heshima kwao na kwa nini Serikali imewaficha wananchi habari za mtu muhimu kabisa kwenye uchunguzi wa EPA? Je, tukisema Serikali imekula njama katika ugonjwa na kifo cha Ballali tutaitwa wachochezi?

Na huu mtindo wa kumsingizia Mungu katika mambo ambayo yeye alitupa akili kuyashughulikia lazima nao ukome. Vinginevyo tuambieni tu kuwa "fedha za EPA zilichotwa kwa mapenzi ya Mungu" ili tujue yaishe.

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk
 
[
B]Mara ikaja hoja huko Boston amepelekwa hospitali gani kwa hayo matibabu. Serikali ikaanza kutupiana mpira, “yuko Boston kwa matibabu” lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kuwaambia Watanzania Ballali amelazwa hospitali gani. Sababu kubwa ni kuwa wangetaja hospitali kuna watu wangejaribu kufuatilia. Hawakutaka kusema hivyo. Kwa nini? Jibu ni jepesi; Ballali hakupelekwa Boston kwenye hospitali yoyote ile. [/B]

Mkuu Bubu,

Heshima mbele mkuu kwa hii article, mimi nilidhani kuwa ndugu yangu anatania, kumbe anaenda kufanya kweli, duh! Yaani JF idumu milele!
 
[

Mkuu Bubu,

Heshima mbele mkuu kwa hii article, mimi nilidhani kuwa ndugu yangu anatania, kumbe anaenda kufanya kweli, duh! Yaani JF idumu milele!

Inanikumbusha kauli ya Balozi wetu ambaye alikuwa anahudhuria kikao cha Mabalozi miezi michache iliyopita pale Z'bar, alipoulizwa Ballali kalazwa hospitali gani akadai kasahau jina la hospitali!!! katika ile mipango ya kuendeleza usanii kumbe jamaa alikuwa anauguzwa nyumbani kwake!!!!
 
FMES,
Mkuu lakini tuache utani huyu jamaa katafutwa siku nyingi toka aliposema anarudi Bongo kutoa ushahidi, sisi wengine tulizipata kupitia migahawani..Lakini duh! ama kweli Tanzania inatisha wala sio kidogo. Mimi nadhani afadhali hata hao Wa South Afrika wanaoua wageni kuliko Wabongo wanaondoa roho za vipenzi wao huku wakilia kwa uchungu...
Damn, ama kweli NDIVYO TULIVYO hata sisi kina machinga tusiojua lolote nasikia tunatafutwa sasa sielewi kwa kitu gani haswa!...
Mkuu hii mpya, jihadharini sana, hawana utu hawa watu ni wanyama.
 
mbowe maskini weee ! i cant wait to see him being questioned maana keshaingia kwenye tundu bado kunyolewa mbawa tu asiruke !
 
Its Ok! Time will tell & In case they fool themselves that we are fools then 2010 will tell, tunacho omba uzima tu & May God Bless.
 
Kama Mbowe alisema haijamchukulia hatua?

Membe kasema eti serikali haihusiki je?hilo linatosha kuwa jibu juu ya kifo cha Balali?

Serikali hii ina wakati mgumu sana hadi sasa na tunasubiria Bunge la bajeti ......kuhakikisha kuwa hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe, na ripoti ya EPA itawekwa hadharani waziwazi..
 
Back
Top Bottom