Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Amechomwa moto au amezikwa kawaida? Kuna mtu yeyote hapa anayejua mahali kaburi lilipo? Hivi kuna uwezekano gani wa kuibana serekali itoe proof kuhusu hili suala? Au ndio tumeshapigwa bao?
 
Amechomwa moto au amezikwa kawaida? Kuna mtu yeyote hapa anayejua mahali kaburi lilipo? Hivi kuna uwezekano gani wa kuibana serekali itoe proof kuhusu hili suala? Au ndio tumeshapigwa bao?

Sikujua Balali alikuwa baniani.
 
Mazishi yalikuwa ya faragha na picha za mgando na Video hazikuruhusiwa na hata picha via phone's hawa wa gazeti wao waliipata wapi ?

sasa huu ufaragha ndo unatisha, kuna mambo yataendelea kusumbua akili zetu nayo ni haya

1.kwa mtu kama balali, mhehe wa iringa kuamua kuzikwa marekani, bila mama yake mzazi kuwepo, angalau tunajua upendo wa mtoto kwa mama

2 mama yake kupewa ulinzi mkali kiasi ambacho hakieleweki ni kwa nini, kwa upeo wangu mdogo ni kuwa wanaogopa mzee wa miaka 94 anaweza asiweke siri na akatoa yote dililikasanuka. niliwahi kwenda kumzika rafiki yangu aliyekuwa mwalimu the then IDM, babake alikuwa mzee sana, nadhani miaka hiyo hiyo ya 90 and above,. baada ya mazishi tukaenda kuagana naye , kumuarifu kuwa tulikuwa tunarudi idm, yeye bila kujua akatupa tena salamu, yaani mkifika huko msiache kumsalimia sana NANI! huyu nani ndo huyo tulikuwa tumekuja kumzika. sasa huenda ndo hayo yanayoogopwa
3. maizshi ya faragha? mazishi ya princess diana, yalifanyika kwa faraja, na hata mother Theresa of calcura, lakini hadhira ilishirikishwa na ufaraja ulikuwa hatua za mwsisho tu, tena wakati wa kushusha mwili kaburini. HUU UFARAGHA WA MAZISHI YA BALALI SIYO FARAGHA TENA BALI USIRI? KULIKONI

4 HADI SASA HAKUNA MSEMAJI WA FAMILIA YA BALALI, HIVI HAKUWA NA NDUGU HAPA?

MH! MENGI YANAKUJA
 
Tanzania Tanzania,
Nakupenda kwa moyo wote
Nilalapo nakuota wewe
Niamkapo NIMEKUFA kupoteza ushaidi!!

Swala la kifo cha Balali litaendelea kuwa kitendawili. Tusubiri hotuba ya mwisho wa mwezi huenda JK akalighusia baada ya membe kutufananisha na wachawi.
 
Mgonjwa mahututi afie nyumbani halafu mpaka hii leo jina la hospitali ambayo alikuwa anatibiwa bado ni siri kali pamoja na kuwa BoT walikuwa wanamlipia bills zake za hospitali!!! Kwanini jina la hospitali ambako Ballali alikuwa anatibiwa bado ni siri pamoja na kuwa kishafariki?
 
Sasa ni wazi kuwa baadaye nitaanzisha thread ya kuomba radhi kwenu wewe na MKJJ.

Ni wazi kuwa mmesikiliza vilio vyetu na kuweka empathy na kutuelewa wasiwasi wetu ulikuwa ni wa kibinadamu tu na wala si kwa ubaya!

Hongera sana kwa uamuzi mchungu...Ila tuko pamoja!
Na ninasikilizia tu kwasababu muda si mrefu mtasababisha tuwatafute ili tuwabebe ama kusukuma magari yenu huku marekani!

Ni mategemeo yangu kuwa tutafanya hivyo JULY 4 Huku Columbus na kusheherekea uhuru..

Uhuru si tu wa Marekani...Bali uhuru wa kifikra na mwanzo wa mapinduzi ya kijamii na kisiasa kwenye Taifa letu!

Ni serikali yenyewe ama ni mpango wa Mungu kuwa sasa watanzania walioko Marekani wanatazamwa kwa makini na kwa moyo wa matumaini na watanzania wote walioko nyumbani ambao wanatuangalia sisi kama mabalozi wao kwenye kupigania haki kwenye ardhi ambayo wengi wao wanaisikia ama kuiona tu kwenye TV.

Ardhi ambayo wanatamani ipasuke ili iweze kumtoa Ballali...Ardhi ambayo wangekuwa na uwezo..

Basi wangeivamia na kuja kutafuta haki yao ambayo ilikuwa ikilelekea kuyumba kutokana na umbali wa kule waliko!

Kazi imeanza...Mungu ibariki Tanzania.
 
Nisaidieni kwa hili. Mimi ninachofahamu usiri mara nyingi kwenye misiba au sababu ya kifo ni pale ambapo aliyefariki alikuwa mgonjwa wa UKIMWI.
Nimewaza na kuwazua kama alikuwa mgonjwa kipindi chote hiki na hakuna aliyefahamu anaumwa kitu gani je yawezeana alikuwa anaumwa UKIMWI. Pili ikiwa amefia nyumbani basi pia yawezekana ni hilohilo ugonjwa umemuua kama kweli amefariki.
Mimi sioni sababu ya ndugu zake kubaki wana-save face. What face is there to save ikiwa tayari mtu wao alishaburuzwa kwenye matope unless wanataka ku-save face ya mkewe.............si unatujua sisi waafrika tulivyo. And the funny thing there is no secret under the skies, watakaotoka msibani watanong'ona mpaka basi. Naam, tutayasikia tu.
 
UKIMWI?
I doubt it..Kwa mapesa yote hayo angeshindwa kupata madawa ya Magic Johnson kweli?
 
siku nne kabla hawajatutangazia apotea duniani-au kufa Balozi wa TZ USA bwana Sefue alikwenda nyumbani kwa Balali na walikuwa na maongezi naye.
Sasa sirikali kusema haijui alipo; Mkulo kuja DC na kusema alimtafuta Balali hakumwona lakini balozi aweza kwenda kwake ushahidi ninao wa yeye kukiri alikwenda kwa Balali na kuongea naye, giza lazidi kuwa nene.

Plastic surgery yamfanya Balali kutumia fedha zetu, kuficha siri na kuficha wezi wenzake.
 
Sefue alialikwa kwenye 'mazishi' ya Ballali je alihudhuria? Anaweza kuhojiwa na waandishi wa habari akatoa kauli kwamba hakumbuki kama alihudhuria mazishi ya Ballali au la!!!! au akadai alikuwa nje ya US hivyo hakupata nafasi hiyo.
 
Nime-search Ballali na nimepata very interesting details hadi possible associates wake ila sasa nashindwa jinsi ya kuzimwaga hapa maana ni taarifa hizo inatoa list ya watu wakaribu nao pia ni ndefu design.
Nataka to copy the whole screen ili itoke hapa live. Anayeweza ujasusi basi afuatilie wengine tuko mbali. Hata hivyo naweza nikatoa link mwenye kujua technological manjonjo aweze kuzimwaga hapa.

web page ni hii
http://preview.ussearch.com/preview/ala/newsearch?&searchLName=Ballali&searchState=MA&searchCity=boston&adID=619200D473&adsource=9&TID=0&cid=people&searchtab=people
 
Sefue alialikwa kwenye 'mazishi' ya Ballali je alihudhuria? Anaweza kuhojiwa na waandishi wa habari akatoa kauli kwamba hakumbuki kama alihudhuria mazishi ya Ballali au la!!!! au akadai alikuwa nje ya US hivyo hakupata nafasi hiyo.

Balozi Sefue na wenzake wa ubalozini walikuwepo.....
 
Bi Mkubwa hiyo web site uliyoiweka hapa basi nikaingiza jina la fisadi Mkapa na kupata jina la kitongoji ambapo ana nyumba yake.

Name: Benjamin W Mkapa
Age: 69
City/state: Bethesda, MD
Relative:Anna J Mkapa
 
Mhn..Halafu huko BETHESDA sijui kuna nini!
Yani nyumba wote wanazo huko...Kuna mtu ameshaweza kwenda huko kwa Mkapa kuangalia kama hajajificha huko nyumbani kwake? lol!
 
Hiyo web site hapo juu kiboko. Nimeingiza majina machache ya mafisadi basi nikakutana na address za watoto wao na Mzee wa vijisenti naye ana address moja Washington kwa jina lake la Andrew Chenge.
 
Mgonjwa mahututi afie nyumbani halafu mpaka hii leo jina la hospitali ambayo alikuwa anatibiwa bado ni siri kali pamoja na kuwa BoT walikuwa wanamlipia bills zake za hospitali!!! Kwanini jina la hospitali ambako Ballali alikuwa anatibiwa bado ni siri pamoja na kuwa kishafariki?

Mimi niliwahi kusikia kwamba hospitali aliyokuwa akitibiwa Ballali Boston inaitwa "New England Medical"....Iko Washington Street, Boston, karibu na "China Town" ......opposite na "Double Tree Hotel".
 
Bi Mkubwa hiyo web site uliyoiweka hapa basi nikaingiza jina la fisadi Mkapa na kupata jina la kitongoji ambapo ana nyumba yake.

Name: Benjamin W Mkapa
Age: 69
City/state: Bethesda, MD
Relative:Anna J Mkapa

Viongozi wetu ni wezi hakuna mfano mbaya zaidi hawana creativity na ni picha ya stagnant thinking capabilities. Ndio nini wote wajimwage Bethesda, MD?? Ina maana kuwa kuna mtu wao huko anayewatafutia nyumba yaani real estate agent.

Bado ninaendelea kuitia mtandao vizuri na ninaangalia jina moja hadi lingine kwenye list iliyotoka ya associates wao. Mmoja tu ambaye nimempata kwenye list ya Mkewe Ballali alikuwa balozi wa mrekani nchini Zimbabwe na alikuwa Foreign services hapa marekani.

Na kama list nilivyosema ni ndefu ajabu ila tutapata mtu anayewaunganisha wote hawa.
 
Mkuu Wangu Mwafrika Wa Kike,

Naomba nikupe heshima kubwa sana, na ninaheshimu sana the fact kwamba hapa JF tunakuwa na hoja tofauti on the ishu bila kutishana wala matusi, ninaomba kusema yafuatayo kulingana na uchunguzi wangu kuhusu kifo cha Balali, niliyoyagundua

1. Balali ninaamini 100% kuwa amefariki na kuzikwa majuzi kule Silver Spring, walioruhusiwa kuona maiti ni balozi Sefue, ndugu wa karibu, na maofisa wachache toka IMF, mwili wa marehemu haukuchomwa ila ulizikwa kama ulivyo. Hakuna laiyekuwa akiuliza kadi za kualikwa kuanzia kanisani mpaka kwenye mazishi, hivyo kupelekea watu wengi ambao hawakualikwa ku-gate crash, mke wake wa zamani alikuwepo so was watoto wake wawili wa mke wa kwanza, na pia mke wa sasa alikuwepo na mtoto wa mke ambaye sio wa Balali alikuwepo pia, Balali na mama wa sasa aliyemuacha hawakuwa na mtoto.

2. Hapa niweke marekebisho makubwa kwa kauli zetu nyingi sana, Balali hakuwahi kuwepo Boston hata wakati mmoja au wowote ule, Marehemu hakuwahi kufanya kazi World Bank kama wengi tulivyoaminishwa, aliwahi kufanya kazi IMF, akiwa na level ya juu sana iliyokuwa inampa nafasi ya kuwasiamia ma-Gavana wote wa Afrika kimashauriano, kwa hiyo alipochukua kazi ya u-Gavana wetu, wakuu huko IMF walishitushwa sana.

3. Niendelee zaidi na uchunguzi wangu ni kwamba Balali, ni kweli alikuwa na nyumba huko DC eneo la Bethesda, mahali panapoitwa Potomac, ambako pia balozi wetu anaishi, lakini aliporudi bongo aliipangissha ile nyumba , na kununua nyumba nyingine mahali panapoitwa Foggbottom, Washington DC eneo wanalosihi watu wakali kama Condy Rice na Bob Dole na wengineo, na ndipo alipofia yaani nyumbani kwake hapo, na hiyo nyumba ipo karibu na Watergate Hotel au apartments.

4. Balali aliondoka mara ya mwisho akielekea US kutokea Dodoma, alianza kupata maumivu makubwa ya tumbo, aliunganisha na kwenda US ambako alikuwa akitbiwa na baadye alipona na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake, ambako alikufa ghafla, siku ya Jumapili iliyopita.

5. Mara baada tu ya kuondoka kwa Balali, na habari zake kuanza kutoka kwenye media na kila mahali, kuna kundi la "Majambazi" lillilokwenda nyumbani kwa Mama wa Balali na kumpa kipigo kikali sana na kuipekua nyumba nje ndani, kule Boko na kuondoka na somethings, lakini haijulikani ni watu gani hawa kama ni majambazi kweli au "Majambazi", mke wa sasa wa Balali ilibidi arudi nyumbani kumuuguza mama mkwe, na ndio chanzo cha kuwekewa walinzi kwenye nyumba hiyo, kama ni wa serikali au wa binafsi hilo sikuweza kuthibitisha.

6. Ninaomba kusema hivi, kuwa serikali haijawahi kuwa ana habari yoyote ya uhakika na hii ishu, zaidi tu ya kuokoteza okoteza hasa hapa JF, hii ni kwa maoni yangu binafsi na mengi ninyoyajua.

Kwa hayo machache, ninaomba kusema kuwa ninaamini 100%, kuwa Balali amekufa, lakini pia ninaheshimu sana hoja ya Ndugu yangu Mwafrika Wa Kike kuwa anaamini kuwa hajafariki. Ningewaomba ndugu zangu wengine humu kuwa tujaribu kutafuta ukweli wa hii habari ili tuweze kuelimishana, hayo niliyoyasema nimeyafanyia kazi kubwa sana ikiwa ni pamoja kutembelea miji yote mitatu ya Boston, Dc, na Louisiana na bado ninaendelea lakini sio kwa kasikubwa tena kama mwanzoni,

Na pia ninaomba niwaombe radhi sana wanafamilia wa marehemu, kuwa sina nina ya kuendelea kuwaumiza na never ending stories on hiki kifo, lakini ni vyema tukweka record straight.

Ahsanteni Ndugu Zangu! JF mbele Zaidi!
 
Ndugu zangu Watanzania, inatia moyo mkubwa sana kuona jinsi tunavyoshiriki katika vita hivi dhidi ya mafisadi. Sasa mpaka maaskofu nao wamejiunga katika vita hivi vya kuikomboa Tanzania toka mikononi mwa mafisadi. Waziri Mkuu Pinda pia ametamka hadharani vita dhidi ya mafisadi ni ya kila Mtanzania. Pamoja na kuwa mafisadi bado hawajaanza kushughulikiwa kama ambavyo tunavyotarajia lakini taratibu tunawaweka roho juu huku wakijua kwamba kikomo cha ufisadi wao dhidi ya nchi yetu hakiko mbali, naam waswahili walisema za SIKU ZA MWIZI NI AROBAINI taratibu tutawashinda mafisadi na kuitakasa nchi yetu ili ipate maendeleo yanayostahili kwa manufaa yetu na vizazi vyetu vijavyo. Mwenyezi Mungu awabariki popote pale mlipo duniani na pia atusaidie ili tuwashinde mafisadi na kuwatokomeza kabisa.

Mungu ibariki Tanzania
 
Hii ni bizarre twist, hapa bado kuna fumbo kubwa linalotakiwa kufumbuliwa. The target ni mafisadi kuwekwa wazi na kuchukuliwa hatua, na hili linawezekana whether Balali amekufa na kuzikwa DC, au awe hai na amejificha Ansucion au Buenos Aires. Kuwapata mafisadi na majina yao kuwekwa wazi ni matter of time, huenda baadhi ya watu wanataka kununua muda ili kucapitalize 2010, na hii habari ya Balali ni kama kionjo tu, siamini kama ni yeye pekee anayemfahamu Mr Epa, yaani mwizi mkuu na aliyetoa baraka za wizi wa EPA, kuna watanzania wengi wanawajua watu hao !
 
Back
Top Bottom