Mwafrika wa Kike,
Mimi ningependa sana unipe sababu ambazo unafikiria zimemfanya Balali a fake kifo!..
I mean nashindwa kuelewa mtu mzima kama yule kwa nini aka fake kifo, hali mnasema ni mmoja kati ya Mafisadi ambao wanaiendesha nchi..
Ofisi ya Kikwete walisema hawamhitaji, sasa hicho kifo cha nini ama alikuwa kaweka Life Insurance ya mabillioni!
Mkandara,
Kukaa Keko na kujificha Kisiwani wapi nafuu?
Kwa Mafisadi kuumbuliwa na Ballali kungeliwamaliza wote kisiasa na kijamii.
Dawa ni kujifanya amekufa, yeye atapona kukamatwa na kuishia Keko na hao mafisadi wenzake hakutakuwa na ushahidi wa nguvu wa kuwahusisha moja kwa moja hasa huyo Mkapa na Apson na wenzao wengine.
Alichofanya Ballali ni kama kutoroka jela, je ni wahalifu wangapi wakipewa nafasi wanaweza kushindwa kufanya alichofanya Ballali?
Kama amekufa usiri wote huu una faida gani? Wewe kweli kaka yako amekufa, unachukua siku tano kumwambia mamake? Haiingii kabisa kichwani.
Leteni hospitali basi alikofia hata kama alikuwa anatumia jina fake, mkitupa hospitali mengine tutajua.
Ukiona gavana mzima wa nchi anaanza kutumia majina fake kuogopa usalama wa taifa, kitu gani kitamfanya ashindwe ku fake kifo kuogopa hao hao usalama wa taifa na mkono wa sheria?