Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Mwafrika wa Kike,
Mimi ningependa sana unipe sababu ambazo unafikiria zimemfanya Balali a fake kifo!..
I mean nashindwa kuelewa mtu mzima kama yule kwa nini aka fake kifo, hali mnasema ni mmoja kati ya Mafisadi ambao wanaiendesha nchi..
Ofisi ya Kikwete walisema hawamhitaji, sasa hicho kifo cha nini ama alikuwa kaweka Life Insurance ya mabillioni!

Mkandara,

Kukaa Keko na kujificha Kisiwani wapi nafuu?

Kwa Mafisadi kuumbuliwa na Ballali kungeliwamaliza wote kisiasa na kijamii.

Dawa ni kujifanya amekufa, yeye atapona kukamatwa na kuishia Keko na hao mafisadi wenzake hakutakuwa na ushahidi wa nguvu wa kuwahusisha moja kwa moja hasa huyo Mkapa na Apson na wenzao wengine.

Alichofanya Ballali ni kama kutoroka jela, je ni wahalifu wangapi wakipewa nafasi wanaweza kushindwa kufanya alichofanya Ballali?

Kama amekufa usiri wote huu una faida gani? Wewe kweli kaka yako amekufa, unachukua siku tano kumwambia mamake? Haiingii kabisa kichwani.

Leteni hospitali basi alikofia hata kama alikuwa anatumia jina fake, mkitupa hospitali mengine tutajua.

Ukiona gavana mzima wa nchi anaanza kutumia majina fake kuogopa usalama wa taifa, kitu gani kitamfanya ashindwe ku fake kifo kuogopa hao hao usalama wa taifa na mkono wa sheria?
 
Nimetua Bongo juzi nikitokea kwenye mizunguko kadhaa, nimekuta hapa habari inayosema chama kimoja cha siasa kilifanya press conference na kukataa kwamba Ballali hajafa, kinaiuliza serikali ni kwa nini imeweka ulinzi mkali nyumbani kwa Ballali, tena iweje familia isiweke msiba wowote, si Dar es salaam, wala mkoani alikozaliwa
 
1.
Augustine, if its a bitter-pill then I'm sure Jasusi a.k.a Invisible already swallow it!!

Mkuu kama huji uliza kwanza, hivi ni nani hapa JF asiyejua kuwa Jasusi na Invisible ni watu wawili tofauti? Sasa kama mambo madogo tu kama haya hujui sasa unapata wapi nguvu ya kuongelea makubwa kama unavyojifanya kujua?

2.
What a fault they done by only recognized FMES to join their conspiracy team and forget that behind leaving many JF members who's ability to analyze things is unquestionable. The picture is clear that "someone is trying to use them to make JF's members believe Government conspiracy on this fate"!

Mkuu kutofautiana mawazo yangu na Mwafrika Wa Kike, basi imekuwa ni ku-join conspiracy ya Balali mbona ni mawazo shallow sana haya? Mimi nimefanya uchunguzi wangu na nimesema hivi ningekuwa ninapewa info na any member wa Balali, nisingethubutu hata kuandika on the ishus hapa, wewe mtu ambaye hata huelewi kuwa Jasusi sio Inviisible, sasa kweli anayetumiwa hapa ni nani si wewe ambaye hujui kitu wala huwezi kuuliza mkuu?

3.
Have you noted that the source, which claimed to be reliable by FMES,

Tizama unavyochekesha, ni wapi nimesema source zangu kwenye hii ishu?

4.
are the one used and supported by both Jasus and Salva (Magogoni)? Unless they tell people the truth Ballali's gost will keepon stinks to them and their families!

Mkuu jifunze namna ya ku-debate hapa JF, ni kwamba Mwafrika Wa Kike amesema hivi amefanya uchunguzi na kutoa matokeo ya uchunguzi wake, mimi imesema nimefanya uchunguzi na kutoa matokeo yangu, sasa na wewe tuambie umefanya nini zaidi tu ya kuweka logic zisizokuwa na msingi, mimi siiwezi hata kusema kuwa kuna anyekutuma kwa sababu hakuna mtu anyeweza kumtuma mtu asiyekuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri ambao unaonyeshwa na maneno yako, kwamba ni mtupu,

Kama unaamini Balali amekufa, basi weka hoja zako na kama huamini weka hoja zako, name calling maana yake ni moja tu huna ukweli wala hoja, labda ni vyema ukakaa pembeni maana unaona Mtanzania, anaweka hoja kwa nini haamini kuwa Balali hajafa, jifunze hoja mkuu!
 
Wakuu,

Kwa uchunguzi niliofanya mimi hata kama sio scientific lakini naamini picha inaanza kujengeka.

Habari zote za Ballali kuumwa, kupewa sumu na kufa zimetoka na zinaendelea kutoka source moja. Mwanzo wa yote ni huyo mama Anna Muganda na baada ya hapo inashuka chini kupitia familia yake.

Haya mambo huenda yalipangwa siku nyingi kwa habari kutolewa kidogo kidogo kuanzia ile ya sumu Dodoma mpaka hizi zingine. Hakukuwa na sumu yoyote ila hiyo ilikuwa ndio njia ya kuondokea TZ. Hakuna Dr. wa Ballali anayeweza kuuhakikishia ulimwengu kwamba Ballali alilishwa sumu.

Ukifuatilia kwa karibu utagundua sources za Invisible, Tanzania Daima, Mbowe, Jasusi, FMES zinatoka sehemu moja, juu kabisa ya mti amekaa mke wa Ballali. Je katika hao wote ni nani ameona mwili au picha ya mwili wa marehemu Ballali na lini?

Jasusi ametuita wengine Thomaso lakini mimi pamoja na kumfahamu Jasusi kwa miaka na miaka na kuheshimiana sana lakini kweli hili sikubaliani naye kwa asilimia 100. Naamini na yeye yuko juu kabisa kwenye mti wa kudanganya Watanzania, yeye ndio kama msemaji (master of SPIN) wa huo udanganyifu na njama nzima. Kama itakuja onekana tofauti basi nitamuomba msamaha Jasusi ila kwa hili mimi simwamini Jasusi kama ambavyo siamini kifo cha Ballali.

Mimi niliandika siku ya kwanza kwamba namwonea huruma Invisible maana ni kijana makini na yeye alituma hii habari akiamini ni kweli kumbe wajanja wameamua kumtumia yeye ili kuupa udanganyifu wao nguvu. Walijua hapa JF Invisible anaaminiwa karibu na sisi sote.

Kitu kingine ninachoamini ni kwamba walijaribu kumtumia Mzee Mwanakijiji, lakini huyu mzee kaona mengi, akataka habari zaidi na zaidi na baada ya muda akaanza kugundua mapengo kwenye habari yenyewe. Pia walijaribu kumtumia wetu Mwafrika wa Kike, lakini Mwafrika wa Kike naye hana rafiki, anachunguza hata ndugu zake. Alipoamua kuchunguza akaanza kuona mapengo.

Wote tunamjua FMES hapa kwa data, ila FMES ana tatizo moja, ni royal mpaka siku ya mwisho kwa marafiki wake. Huwa anajiuliza maswali mengi mazito mambo yanapohusu watu wa mbali lakini penye ndugu au marafiki wa karibu tusimtegemee FMES. Ninaamini
FMES hana uhakika na kifo cha Ballali ila tu ameamua kutetea ili kutokuwaudhi baadhi ya marafiki au ndugu. Ninamwelewa kwa msimamao wake huo maana ninamjua kwa muda mrefu kwamba atakuwa wa mwisho kumsaliti rafiki.

Naamini serikali inahusika kwenye hili kupitia usalama wa taifa. Inawezekana JK binafsi hahusiki lakini kuna watu wengi wenye uhusiano na usalama wa taifa wa zamani, naamini wanahusika na hili.
 
Nimetua Bongo juzi nikitokea kwenye mizunguko kadhaa, nimekuta hapa habari inayosema chama kimoja cha siasa kilifanya press conference na kukataa kwamba Ballali hajafa, kinaiuliza serikali ni kwa nini imeweka ulinzi mkali nyumbani kwa Ballali, tena iweje familia isiweke msiba wowote, si Dar es salaam, wala mkoani alikozaliwa

LOOOOOOOOOOOOHHHHH!!!!!bado ulinzi mkali nyumbani kwa mama yake??serikali haioni hata aibu kwa ujinga huoo yaan inafanya mambo yanayolead nianze ku question elimu na hekima za hao watu huo juu!maana hata watu waliopita sekondari wakasoma seriously cant do things the way serikali yetu ya do if ndio wao wanado...nahisi wengi wao huko juu wameishia primary huko kwengine kooote walikua wanakwenda tu darasani kuonekana wapo!!

msiba hata ukitokea nje ya dunia kawaida familia as a family wanaweka msiba tz ikiwezekana nyumbani kwa marehemu au wazazi wake if nt ndugu wa karibu lakini huu yote hayo eti hayajafanywaaA??doooh nasikitika kusema mijitu iliyoplan this thing ni mijitu mizima ovyooooooooooooo
 
Mkuu Wangu Mtanzania,

Heshima mbele, nilipokwenda Louisiana kufuatilia hii ishu sikuonanana mke wa Balali akanipa info wala Jasusi, hapana, hizi habari nimezitafuta mwenyewe kwa njia zangu, sasa pkaifikia mahali dada yangu akaalikwa kwenye mazishi kwa kweli ni lazima niwe na dini pia maana siasa inafika mahali inaisha lakini sio Mungu,

Maneno yako ni mazito na yamejaa hoja nzito sana, ninaikubali analysis yako on Mwanakijiji 100%, na sina tatizo na msimamo wako on hiki kifo, lakini msimamo wangu hauko influenced na anything au anybody, the matter of fact sasa hivi hata hiyo familia ya Balali watakuwa wanajiuliza sana nani ananipa hizi info, binafsi ninajaribu kuwa na maswali kama wewe,

Familia ya Balali wana what to gain kwa kuvuta hii stint? Serikali ninajua ina a lot to gain, lakini sio familia ya Balali kwa kushirikiana na serikali hiyo haniingii kichwani mkuu hebu nisaidie hapo? Ninakubali sana hoja zako na MMJ na MWK, lakini hapa mwishoni ndio ninapata taaabu sana mkuu hebu nisaidie hapo, WHY? Ukinisaidia hapao nitamnwaga more ugly dataz on this Balali thing au mtu yoyote yule akiweza kunipa a strong argument kwa nini Familia ya Balali wavute hii deal?
 
•
Mkapa aenda 'Boston kwa Ballali' (Majira)

Na Mwandishi Wetu

RAIS mstaafu Bw. Benjamini Mkapa anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Ulaya na Marekani ambapo ziara hiyo itamfikisha mjini Boston, jimboni Massachusetts alikoishi gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) marehemu Dkt. Daudi Ballali.

Katika siku za karibuni mji wa Boston umejikita kwenye hisia za Watanzania kufuatia mlolongo wa tukio la ugonjwa hadi kifo cha ,Dkt. Ballali ambaye aliishi mjini humo hadi alipofariki kwa ugonjwa, Mei 16 mwaka huu na kuzikwa Washington DC.

Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu, Rais Jakaya Kikwete alikaririwa akisema "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Ndugu Daudi Ballali kilichotokea Mei 16, 2008 huko Boston Marekani."

Aliongeza kuwa "Wakati huu mkijiandaa na mazishi yake, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na ndugu wote. Naungana nanyi katika wakati huu mgumu na wa majonzi mkubwa uliowakuta.

Dkt. Ballali aliondoka nchini Agosti mwaka jana kwenda Boston,Marekani kwa matibabu ingawa hadi anafariki hakuna aliyekuwa tayari kubainisha ugonjwa wala hospitali aliyokuwa akitibiwa gavana huyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, Dar es Salaam na Msaidizi wa Rais huyo mstaafu,Dkt. Aziz Mlima, ziara ya Bw. Mkapa itaanzania London Uingereza ambapo atahudhuria Mkutano wa Bodi ya Wadhamini na Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Uwekezaji Afrika (ICF) ambayo yeye ni Mwenyekiti mwenza.

Taarifa hiyo ilifafanua kwamba Bw. Mkapa pamoja na Mwenyekiti mwenza wa pili wa ICF, Bw. Niall FitzGerald, watashirikiana kuongoza mikutano hiyo inayotarajiwa kufanyika Juni 2 na 3 mwaka huu.

Baada ya mkutano huo, Rais mstaafu atakwenda mjini Boston, jimboni la Massachusetts, Marekani kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Aga Khan ambacho yeye ni mjumbe.

Taarifa hiyo ilibainisha kwamba Taasisi ya Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, inatarajia kujenga Chuo Kikuu mkoani Arusha Tanzania.

ICF yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, inahusika na shughuli za kusaidia Afrika kujenga mazingira mazuri ya kuvutia biashara na kuiwezesha kutambua mchango wake kama mshiriki katika biashara za kimataifa.

Katika kutekeleza majukumu yake, taasisi hiyo inafanya jitihada za kuondoa vikwazo vilivyopo, vinavyotarajiwa na vinavyozuia uwekezaji wa ndani na nje kwa kusaidia waafrika kujiandaa kulitangaza bara hilo kama kivutio cha uwekezaji.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba kwa sasa ICF inayo miradi katika nchi mbalimbali za Afrika na kutoa mfano wa mkataba kati ya taasisi hiyo na Mahakama ya Tanzania uliosainiwa wiki mbili zilizopita kwa ajili ya kuijengea uwezo wa kuharakisha shughuli zake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ICF inatoa kipaumbele kwenye eneo la haki miliki na utekelezaji wa mikataba, usajili wa biashara na utoaji leseni, kodi na ushuru, masoko ya fedha, kujenga uwezo wa miundombinu, soko la wafanyakazi na ushindani.

Ilieleza kwamba taasisi hiyo inapata fedha za kuendesha shughuli zake kutoka katika serikali mbalimbali, taasisi za kimataifa na nchi wahisani zikiwemo Ujerumani, Iyalandi, Uingereza, Norwei, Ufaransa, Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Taasisi ya Fedha ya Kimataifa (IFC) na Unilever.

Wafadhili wengine wa ICF ni Benki ya Standard, Taasisi ya Shell Foundation, Kampuni ya Simu ya Celtel na Umoja wa Ulaya. Taarifa hiyo ilibainisha kwamba nchi nyingine zipo katika mazungumzo kwa ajili ya kuipatia taasisi hiyo msaada zaidi.
 
Hata nikikutajia hospitali yenyewe haitasaidia kwa sababu aliandikishwa kwa jina bandia baada ya magazeti ya Tanzania kuripoti kuwa serikali imetuma makachero kumtafuta. Kumbuka kuwa huyu ni mtu ambaye kuna baadhi ya watu wazito hawakutaka arudi Tanzania alive.

Kati ya mambo ambayo sikutegemea yafanyike ni kama hili, hivi katika nchi kama MAREKANI ambayo ninaamini vyombo vyake vya usalama vinafanya kazi vizuri sana unapata tishio kuwa mtu wako ametumiwa na Makachero hivi unaweza kukimbilia kubalisha jina kwanza. Especially kwa mtu aliyekuwa amefikia kiwango cha juu sana katika jamii na anawatu wakubwa sana ambao wanaweza kusaidia?

Halafu kuna kitu ambacho hakijaulizwa sana humu hila kuna aliyeuliza kwamba kwa nini Balali afake kifo? Labda tena nirudi pale juu, kwanini afake jina?

Halafu tukienda mbali tunakuta BoT mapesa yaliyochukuliwa baadhi wanasema yanaweza kuelekea matrioni, wakati huo huo hakuna investiment kubwa aliyo nayo au pesa aliyo nayo Balali. Wale wazoefu wa Bongo unaweza kuwapa watu kiasi hicho bila wewe uliyetoa kupata mgao wako? Je kwa nini kuna kipindi alikuwa anatetea wakati anajua kila kitu? Hata alipofika marekani ambapo alijua yuko salama bado akawabubu saana.

Je alipofika USA akiwa na burungutu la madocuments wakati huo huo anajua anatafutwa, kwa nini akutafuta hata wapinzania tanzania akawapa hizo information za deal nzima, au kuwapa watoto wake wazipeleke kwa wanasheria hili aweze angalau kujilinda? badala yake documents zote zikaangukia kulekule zilikotoka? nikimaanisha kwa Mukono?

Je katika nchi ya Tanzania ambayo wenye nazo wako juu ya sheria hakuna uwezekano kuwa Balali aliwekeza sana sana katika biashara ya madini ambayo yanaweza kufanya hata watu wakubwa waliokaribu naye wakaona yote lakini wakasema pamoja na fedhea yote lakini inalipa?
 
Haya mambo ni mazito. Maswali mengi kuliko majibu. Hebu kwanza tukubaliane haya halafu tuendelee. Kuna watu wanne muhimu sana hapa:

1) Mwanakijiji: alitoa habari za "kifo" cha Balali mapema sana kabla ya Invisible kwa njia ya mafumbo. Huyu alikuwa na anajua mengi lakini hataki kutumbia. Sasa tumuombe atuweke sawa hii issue iishe.

2) Ifike mahala Invisible atueleze hizo habari za kifo nani alimwambia. Hii tena haiwezi ikawa siri kwa sababu marehemu ameshazikwa (kama kweli alifariki) kwa hiyo hakuna atakayemlaumu

3) Jasusi: Huyu anatia huruma kwa sababu yupo katikati ya mchezo. Ingekuwa mimi ni yeye ama ningeacha kabisa kuchangia anything about Balali au ningejipotelea zangu hapa JF nisionekane kabisa maana ameshaharibu credibility na hakuna atakachosema kuhusu Balali wenye akili zao wakamkubalia. Ninachomuomba sasa hivi, kama ataaamua kuendelea kuchangia hii mada, ni kwamba, kama kweli yeye anajua ndugu yake amekufa, aache kabisa habari zake za kutuambia kwamba ukweli utajulikana. Hakuna ukweli tutakaokuja kuujua kuhusu wezi wa hela zetu pale BoT zaidi ya ule tunaojua sasa kwamba wale majambazi walipewa funguo na kusindikizwa na Balali. Kama Jasusi mlishindwa kumshawishi ndugu yenu kutupa ukweli akiwa hai, tafadhali acha kusema haya maneno maana wengine unatuumiza roho na kuzidi kututia uchungu.

4) FMES: Huyu alikanusha habari za kifo cha Balali mapema sana, tena katika post za mwanzo kabisa za ile thread ya Invisible. Alionekana kuwa na uhakika sana kuhusu ukweli kwamba Balali alikuwa hajafa. Ajabu kubwa kuliko zote, akaibuka na thread ya kutuambia kwamba sasa amethibitisha kwamba Balali amekufa jambo ambalo anaendelea kulitetea katika hii thread ya MWK. Kama tukienda na conspiracy theory ya Mtanzania na MWK, kwamba Balali hajafa, ambayo na mimi sasa wameshanishawishi kabisa kukubaliana nao, ni wazi kwamba FMES alikuwa amesaulika katika ule mduara wa waliokuwa wanapika uongo kuhusu kuugua na kifo cha Balali. Inaonekana baadaye akakumbukwa na kupewa directions kwamba aje hapa abadili msimamo wake wakitarajia kwamba, kwa uzito wake hapa JF, hoja zake zitakubalika.

Lazima tukiri kwamba huu mchezo umechezwa vizuri na wahusika wanaijua vizuri sana nguvu ya JF sasa hivi, na ndio maana wakawatumia vinara kabiaa wa JF katika kusambaza na kuaminisha habari za kiini macho kuhusu Balali. Vinara hawa waliotumika, ama kwa kujua au bila wao kujua, ndio hao niliowatajia hapo juu: Invisible, MKJJ na FMES.

Sasa kubwa kuliko zote:

i) Kwa nini serikali ya CCM chini ya JK imeamua kuishi kwa kuwadanganya wananchi wake? Kama wameamua kutudanganya kuhusu jambo jepesi kama la kuugua na kufa kawa Balali, tutawaamini vipi katika mambo makubwa ya nchi yetu?

ii) Na ni kwa nini watanzania tunaendelea kukikumbatia chama ambacho kinatoa viongozi wanaotudanganya?

iii) Ooops, nilisahau kwamba jamii hupata viongozi inayostahili. Kama tunaweza kuwa na wenzetu hapa JF, ambao tumeaminiani na kuheshimiana siku zote hizo na bado wanashiriki katika kutudanganya, tuna haki gani kuwalaumu serikali wanapotudanganya? Kwani sisi tunatofauti gani na wao?
 
Wapinzani wanaendelea kushikilia kwamba Ballali hajafa, wanamtaka mzee wa kaya aseme mwenyewe, wamesisitiza hilo katika press conference iliyomalizika sasa hivi hapa Dar, wametoa tamko ambalo sehemu yake ya mwanzo inasomeka hivi

National Convention for Construction and Reform-Mageuzi


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

.
Utangulizi
Juma lililopita (24/5/2008),chama chetu kilitoa tamko kwamba,aliyekuwa
Gavana wa BoT, Ndg Daud Ballali yuko hai,yaliyojitokeza baada ya kauli hiyo
hayajabadili msimamo wetu.Serikali imeshindwa kuthibitisha kifo cha Ballali
na badala yake inatoa vitisho kwa wale wanaoamini kama sisi, kuwa Ballali
yuko hai

Chama chetu kimepata taarifa kutoka kwa wanachama wetu sehemu mbalimbali za mikoa ya Dar es salaam na Iringa kwamba,nyumba zote zinazohusishwa na Daud Ballali,ziwe zake mwenyewe,wazazi,shangazi,wajomba,wakwe nk,hazina
dalili zozote za kuwepo na msiba, baadhi ya nyumba hizo zimewekewa ulinzi
mkali ili ‘waombolezaji' wasiingie kwenye nyumba hizo bila kupewa kwanza
vibali.

Aidha jina la Ballali bado lipo kwenye pay roll ya watumishi wa
serikali...
.....(tamko la leo lilikuwa na dhima ya kuwashughulikia wabunge mafisadi na wale wote ambao kashfa ya BOT inawagusa)
 
Mmmh, ngoja nizungushe karai........
tv-Columbo5.jpg


justone.GIF
 
Nio Mafinga Niaizieni Huko Kwa Balai Nikawhi Pilau La Kuvunja Matanga..kwi Kwi
 
If Balali is dead, why shroud his "funeral" in secrecy??? Mtu amekufa, kufichaficha ya nini tena? Kuwasiliana na Ikulu kwanza kabla ya kuwaambia mama yake na nduguze nako kunazua maswali.
Familia ya Balali ingepungukiwa nini kama ingefanya maziko yake kuwa wazi, mfano, kutoa heshima za mwisho kwa wahudhuriaji wote?
 
Mkuu jmushi1,
Nafikiri unauchukulia mtandao, hususan injini za kutafuta vibaya. Aghalabu hazitoi habari za ukweli, nia yao ni kujitangaza tu. Kwa mfano, huwezi kuamini tovuti isemayo government search huku ikiwa na dot com badala ya dot gov. Nasikitika kusema huku ni kupotoshana.

Wakuu wengine wote hapa naomba mnisaidie kitu kimoja; suppose Ballali is not dead, then what? Whether this guy is dead or not, in my opinion, is not relevant to BoT mess since RO declared that he is not wanted (I suppose, they don't want him to spill the beans). The burning question inside Mpanda Merikebu is, why do we waste energy and talent on Ballali who he appears to be just a conduit, or someone who was used/pressured to channel funds to others, while all the recipients, conspirators and thugs using the system are still living lavishly and insult our intelligence by statements such as "vijisenti" or "sina uwezo bali nategemea pensheni"? C'mon people!!! We are better than this.

So, instead of going about finding out whether this man is dead or alive, why can't we just go straight and ask tough questions to the individuals linked to this mess? Don't we all remember when Mama Meghji said she was informed by Mgonja that she was duped by Ballali and what happened? Meghji is gone, Mgonja is still collecting his share of Meremeta. Why didn't Mgonja get the boot as well? This is just a simple example of the big picture we should be looking at. We've seen the list but I think it is unjustifiably unfair for us to talk about Ballali alone while there is at least half a score individuals who should have lion's share of this shameful mess.

Hizo za FBI huziamini?
Mimi nafanya whatever i can na ndio maana nazileta hizo juhudi hapa JF ili tuweze kuzijadili na kuzifanyia uchunguzi.
Hakuna ninacholeta hapa ambacho nimeconclude...Bali tunajua azma ni moja ya kupata ukweli.
 
Mtanzania, Kitila Mkumbo na MWK, nawashukuru kwa mpangilio mzuri sana wa hoja zenu.

Namwomba Mzee Mwanakijiji atufafanulie ilikuwaje hadi akaweza kutangaza"kufa" kwa Ballali mapema. Namwamini sana huyu mwenzetu, na ni tumaini langu kwamba atatufafanulia ili tuondoe wasiwasi.
 
1.
Wote tunamjua FMES hapa kwa data, ila FMES ana tatizo moja, ni royal mpaka siku ya mwisho kwa marafiki wake. Huwa anajiuliza maswali mengi mazito mambo yanapohusu watu wa mbali lakini penye ndugu au marafiki wa karibu tusimtegemee FMES. Ninaamini

Samahani nilikuwa nimetoka kidogo, kwenye hii analysis hujanifanyia haki mkuu, kwa sababu hakuna rafiki yangu kama Mama Mongella, lakini ilipothibitishwa kuwa amefanya madudu unayakumbuka vizuri maoni yangu kwake, Masha ni rafiki yangu ni kweli, wewe na wengine wengi hapa mlimshambulia sana, lakini binafsi kwenye mashambulizi yenu sikuona a serious charge au ushahidi wa kutosha kama unaoudai kwenye kifo cha Balali, sasa iweje iwe tatizo mimi kudai ukweli lakini sio tatizo wewe unapodai ukweli?

2.
FMES hana uhakika na kifo cha Ballali ila tu ameamua kutetea ili kutokuwaudhi baadhi ya marafiki au ndugu. Ninamwelewa kwa msimamao wake huo maana ninamjua kwa muda mrefu kwamba atakuwa wa mwisho kumsaliti rafiki.

Mkuu this is another mistake, hapa JF ninaandika kwa kutumia uzalendo, lakini sio nje ya hapa, na huko kote ninatumia one thing only nacho ni cedibility na ukweli wa dataz, nimesema wazi kuwa ninaamini 100% kuwa Balali amefariki na sababu nikaziweka wazi kwa kila mtu, sasa for you kusema kuwa sina uhakika, wakati ninaamini nia na madhumuni yako ni ku-prove kuwa Balali hajafa sasa I can understand ukizi-dispute hoja za wale tunaoamini kuwa amefariki, lakini sio mambo ya characterization za wale tunaoamini tofauti na unavyoamini,

Credibility ya binadamu kama mimi ianaanzia nyumbani na kwenye maisha yangu ya kila siku, inaenda mpaka kwenye kila kona ya maisha yangu, na wewe unajua kuwa siku zote ninasema ninakiamini, nisichokiamini huwa sisemi hata siku moja, kwa hiyo ninarudia tena kuwa ninaamini 100% kuwa Balali amekufa, na sina tatizo kusikiliza hoja za mtu yoyote hapa anayeweza kuongea kihoja kuwa Balali hajafa,

Physically, nimefanya uchunguzi wangu binafsi kwa kutumia exeperience nzito niliyonayo accademically, kwa sababu nimesoma sana mambo ya uchunguzi kwenye Criminology na Science ya Police, ambayo nina Associate Degree on it, nikaishia ku-conclude kuwa ni kweli Balali amefariki, sikatai mapungufu ya habari za kifo hiki, ambayo binafsi ninayaona kuwa ni mawili tu makubwa kama vile jina la hospitali aliyofariki marehemu na siku hasa aliyofariki marehemu, lakini katika uchunguzi wowote ule si kweli kuwa utaishia kupata 100% juice ya ishu, na siku zote unaenda na other overwhelming evidence ambazo in this case kwangu ni 80% against 20%, tatizo ni pale unapokuwa na 50% against 49%, hapo ningekuwa pamoja na wewe mkuu kukataa, kama nilivyokataa mwanzoni.

Msimamo ninarudia kuwa ninaamini 100%, kuwa Balali amefariki na kwamba in due time ukweli wote wa hospitali na the rst utatoka tu, na ninaahidi kuwa ikithibitishwa kuwa yupo mzima, nitajiuzulu kabisa siasa na forum au anything to do na kutoa habari kwa wananchi.
 
"Msimamo ninarudia kuwa ninaamini 100%, kuwa Balali amefariki na kwamba in due time ukweli wote wa hospitali na the rst utatoka tu, na ninaahidi kuwa ikithibitishwa kuwa yupo mzima, nitajiuzulu kabisa siasa na forum au anything to do na kutoa habari kwa wananchi"
Mkuu FMES,
Heshima na taadhima mbele, hata kama ikijulikana kuwa Balali amefake kifo chake sitakulaumu, kwa sababu inawezekana kabisa kwa sababu moja au nyingine watu watakuwa wametaka ifahamike hivyo, hilo halitakuwa kosa kwako. NI kweli kuna maswali mengi ya kujiuliza. Hizo question mark ndio zinafanya baddhi yetu tuhoji lakini haina maana kuwa information yako haina credibility, na hakuna haja ya kujiuzulu Tanzania inakuhitaji
 
Back
Top Bottom