Kifo cha David Balali: Kauli mbalimbali toka kwa watanzania

Bado nasimamia msimamo wangu wa kuzikataa hizi habari za kifo cha Ballali kwa asilimia 95. Najua kuwa sio business yangu kukubali au kukataa vifo vya watu. Hata hivyo, ninajua pia kuwa Ballali alikuwa gavana wa BoT wakati wa wizi mkubwa kabisa wa mabilioni ya watanzania ukitokea.

Kama yeye si mtuhumiwa, hilo halijathibitishwa kwa sasa kama ambavyo haijathibitishwa kuwa alikuwa mtuhumiwa au shahidi. Ninachojua mimi ni kwamba, kama nimeweka pesa zangu kwenye briefcase na nikamkabidhi kaka yangu kuichunga, nikirudi na kukuta kiwango kikubwa cha pesa kimepotea na kaka yangu bado anaishikiria briefcase yangu, yeye atakuwa ni mshukiwa wa kwanza kabisa kabla ya mengine yote kutokea.

Bado story ya Ballali juu ya kile kilichotokea BoT wakati akiwa gavana inafuatiliwa kujua ukweli wake. Katika hili, kwa vile yeye alikubali pesa zikatoka na hakusema au kufanya chochote, nitachukulia chochote anachosema kwa tahadhali kubwa mpaka ithibitishwe otherwise.

Huu ni msimamo na mtizamo wangu binafsi. Simlazimishi yeyote yule kukubaliana nami katika hili. Nilikubali na kutetea kifo cha Ballali kwa nguvu sana kwa zaidi wiki moja na sikuitwa mpumbavu. Ninategemea kuwa kama uchunguzi wangu ukinipelekea mimi kuamini tofauti basi nitaendelea kutoitwa mpumbavu as longer as silazimishi yeyote yule kukubaliana nami.

Asante!
 
So, ukweli ni upi? Balali kafa ama hajafa?

Anayejua aje hapa anyooshe rekodi.....
 
So, ukweli ni upi? Balali kafa ama hajafa?

Hapa naona itabidi kila mtu afanya wito mwenyewe.
Familia imetangaza kuwa Ballali amekufa na serikali ikafuatia.
Ibada ya mazishi na mazishi vimefanyika na watu wakahudhuria.

Baadhi ya wana JF wakafuatilia na kukosa uthibitisho unaojitegemea katika hili na wakafikia kutoa walichopata hapa. Ikasemwa kuwa Ballali alitumia jina sio lake akiwa hospitali. Ikaonekana kuwa CME haina report ya kifo cha Ballali.

Katika hili Ngabu unaweza kufanya wito wako mwenyewe na usionekane juha au mpumbavu. Ni suala tu la kuiamini familia ya Ballali au la. Inasikitisha na inatisha lakini ukichukulia kuwa kuna mabilioni yamepotea BoT wakati Ballali akiwa gavana, unapata sababu nyingine ya kufikiria mara mbili mbili kama ukubali au uchunguze kidogo ili kujua kilichotokea.
 
Hapana, Mtanzania.
Hapa sikubali. Mkapa na mkewe walituomba kura they are fair game.
Ballali na mkewe hawakuwa viongozi wetu. They never campaigned for any position of public leadership. Let's be fair. Otherwise nitaomba Moderator aingilie kati na kama mimi ndiye mwenye makosa nipigwe palanja.

Ndugu Yangu Jasusi,

Ballali alikuwa na kazi kubwa sana TZ na kulipwa mapesa mengi ili atulindie uchumi wetu. Yeye alikuwa ni public figure na wanachodaiwa kufanya kama ni kweli ni kitu ambacho kina madhara makubwa kwa taifa.

Kama ndugu kuna mambo matatu muhimu ambayo ungeweza kufanya, ni kukaa kimya, kuacha kusoma na mwisho kujibu maswali ya wana JF.

Kuna maswali ya msingi kabisa ambayo tumeshindwa kupata majibu yake na hayo ndiyo yanafanya baadhi yetu tuendelee kutilia wasiwasi hii habari nzima.

Kuna watu ambao sio public figures kabisa na wamejadiliwa hapa ndio iwe Ballali ambaye anahusika na kashfa ya wizi wa mabilioni?

Waache wana JF wajadili kama ambavyo wewe mwenyewe umeshiriki kwenye mijadala mbalimbali. Hata hao nao wana ndugu na wajomba hapa, au ndo ile ya damu nzito kuliko maji?

Pole sana kama yanayojadiliwa hapa yamekuongezea simanzi, tuko kazini, hatuwezi kuacha kutafuta ukweli kwasababu tu mwana JF mmoja analia, hapo tutakuwa tumeacha kumkoma nyani giladi.
 
Hapa naona itabidi kila mtu afanya wito mwenyewe.
Familia imetangaza kuwa Ballali amekufa na serikali ikafuatia.
Ibada ya mazishi na mazishi vimefanyika na watu wakahudhuria.

Baadhi ya wana JF wakafuatilia na kukosa uthibitisho unaojitegemea katika hili na wakafikia kutoa walichopata hapa. Ikasemwa kuwa Ballali alitumia jina sio lake akiwa hospitali. Ikaonekana kuwa CME haina report ya kifo cha Ballali.

Katika hili Ngabu unaweza kufanya wito wako mwenyewe na usionekane juha au mpumbavu. Ni suala tu la kuiamini familia ya Ballali au la. Inasikitisha na inatisha lakini ukichukulia kuwa kuna mabilioni yamepotea BoT wakati Ballali akiwa gavana, unapata sababu nyingine ya kufikiria mara mbili mbili kama ukubali au uchunguze kidogo ili kujua kilichotokea.

Dada M/kike,

Hata watu wa kawaida mtaani bongo, niliwakuta juzi kijiwe cha fundi viatu wauza machungwa na wauza karanga wanajua kabisa mchezo ulio fanyika!

Yaani kama alivo sema Mkijiji, naona kwa hili halikukaa vyema kutuzuga hadi tuka zugika, labda wapange nyingine lakini tumewagundua kwamba wanataka kutuzuga kuficha soo la EPA hakuna mauti hapa!
 
Mimi binafsi ni ndugu wa Balali(Dr) kidini lakini,mpka sasa his "dearth" has caused a lot of angry public discussion and disagreement na hiyo imetokana na usiri wa kifisadi uliofanywa na wahusika.

Mimi kama ndugu wa Balali(Dr) sijaamini kama kafariki kama kuna mtu atakuja na evidence za Dearth statement toka huko anakojua yy nitamuelewa.
Jasusi nisaidie ndugu yangu
 
Dada M/kike,

Hata watu wa kawaida mtaani bongo, niliwakuta juzi kijiwe cha fundi viatu wauza machungwa na wauza karanga wanajua kabisa mchezo ulio fanyika!

Yaani kama alivo sema Mkijiji, naona kwa hili halikukaa vyema kutuzuga hadi tuka zugika, labda wapange nyingine lakini tumewagundua kwamba wanataka kutuzuga kuficha soo la EPA hakuna mauti hapa!

Kweli kabisa Rwabugiri,

Naomba pia ifahamike hapa kuwa mimi sina ugomvi binafsi na familia ya Ballali au yeyote yule aliyeweka habari za kifo cha Ballali. Nilikubaliana na habari zile ambazo Invisible na Mkjj walipewa na wanafamilia na wakaziweka hapa.

Kwa hili, kama tukiamua kuwaamini wanafamilia itabidi wote tukubaliane kuwa ni kweli Ballali amekufa. Niliendelea na utetezi wangu hasa baada ya mkulu wangu FMES kupata uthibitisho katika hili. Ninajaribu sana kuwaamini wote hapa na kwa kweli kwa wale ambao hawamjui Jasusi, yeye ni mtu ambaye tumekuwa naye bega kwa bega katika mengi hapa JF na amekuwa msaada sana kwa dataz nyingi sana hapa za kuwakamata mafisadi.

Niliuita huu uamuzi kama uamuzi wa uchungu. Hakuna anayependa kubishana na taarifa za kifo cha yoyote yule. Kumbuka kuwa wamarekani walijua kuwa watu watabisha kuwa Sadam na watoto wake wamekufa ikawalazimu waweke picha zao kwenye mtandao na vyombo vya habari ili kukata mzizi wa fitina. So far kilichotokea hapa kwenye kifo cha Ballali ni usiri na nadhani hata familia ya Ballali wanawish kuwa wangefanya otherwise kwenye hili.

Tuendelee tu kwenye hili hadi wahusika wengine kwenye hii case kina Mramba na Mgonja wafikishwe kwenye sheria na story nzima ya wizi wa mabilioni ya watanzania kule BoT ijulikane.

Asante!
 
Nadhani ukiangalia sana...siwalaumu wanaoona kuwa Ballali hajafa au wenye kushuku katika sakata zima. Kama nilivyosema nilikuwa naandika makala ndefu ya kuchambua jambo hili na kwanini kuwalaumu wanaoshuku na kuhoji ni kufanya makosa kwani wamepewa sababu. Tetesi za kutokufa au mchezo zisingetokea endapo kungekuwa na kitu kimoja tu nacho ni uwazi na ukweli. Kukosekana kwa hilo kumefanya watu wapike maneno mengi na ndio maana jitihada za kuwashawishi watu wakubali tu kuwa kafa kwa kuangalia picha sidhani kama zitafanikiwa. Ndio maana aidha ni bora kuendelea na ukimya kuliko kujaribu kuufafanua.
 
Hivi hii thread yenyewe sio mzaha? Balali ni binadamu kama sisi. Ana ndugu, familia, na watu wanaompenda. Hajapatikana na hatia yoyote ya hayo anayotuhumiwa. Habari zikaja kwamba amefariki. Wengine wakaja na habari (maoni yao) kuwa hawaamini kama amefariki. Hivi mnadhani ndugu wa Balali (regardless of whether he's dead or not) wakiingia humu na kusoma yote yanayosemwa kuhusu uhai wake watajisikiaje? Uhai wa mtu sio jambo la mzaha.

...Jamani, tuwe sensitive kidogo kwa baadhi ya mambo.

Nyani;

Idi Amini hakupatikana na hatia, alikuwa binadamu kama sisi, na alikuwa na famililia, na watu wanaompenda, na ndugu, na siku alipo kufa watoto na wake zake wakaingia magazetini wakasoma mashitaka ya umma (public condemnation) kuhusu shutuma mbali mbali dhidi yake. Unadhani watu walikuwa 'insensitive' kwa watoto wa Iddi Amini kwa kusema marehemu Iddi Amini alikuwa kauzu?

Ballali alikuwa bosi wa sehemu hela zilipo potea.

Zingine zimelipa madeni kwa kampuni za wezi (nasema wezi kwa sababu wamekubali kurudisha hela).

Zingine Ballali akaongopa kwamba zimeenda Usalama wa Taifa (nasema akaongopa kwa sababu Waziri wake, Meghji, amemruka na kusema fedha zilikuwa haziendi Usalama wa Taifa)

Zingine zikaenda kujenga maorofa pacha kitapeli, (nasema kitapeli kwa sababu wataalam wa Civil Engineering wamesema fedha zilizo tumika zilizidi zile ambazo zingejenga ghorofo hili hilo mjini Manhattan, ardhi ya gharama kujenga kuliko zote duniani.)

Zingine zikaenda kulipia kesi za BOT kifisadi fisadi (nasema kifisadi kwa sababu wakaguzi wa mahesabu wamesema kwamba gharama za mawakili zilizidi asilimia inayo ruhusiwa kulingana na ukubwa wa kesi yenyewe, kwa mujibu wa sheria)

Sasa, hawa watoto watakao sikitishwa kusoma huu ubao hapa, mbona Baba yao hakuwa "sensitive" wakati anafanya huu ufidhuli wenye vigezo hivyo hapo juu?
 
Kwanza, kifo cha Amin hakikuwa na utata. Je, Balali kafa au hajafa?
Halafu unazungumza kwa mamlaka kama unao ushahidi wa yeye kutenda yale anayotuhumiwa. Hiyo kesi yake mahakamani ilikuwa lini na verdict yake ni ipi?

Unaona Mwanakijiji alivyokuwa upset na kifo changu. Mwenzio nilikaripiwa vikali sana Jumamosi (Lol). Sasa itokee kweli Balali hajafa, unadhani ndugu zake na yeye mwenyewe atajisikiaje na huo uzushi? Au itokee kuwa ni kweli kafa, halafu baadhi ya watu wansema tena kwa uhakika kabisa kuwa hajafa, unadhani ndugu zake watajisikiaje?

Mimi beef yangu kubwa ni huu uzushi (utata) wa kifo chake. Which is which? Do you know for a fact?
 
Kwanza, kifo cha Amin hakikuwa na utata. Je, Balali kafa au hajafa?
Halafu unazungumza kwa mamlaka kama unao ushahidi wa yeye kutenda yale anayotuhumiwa. Hiyo kesi yake mahakamani ilikuwa lini na verdict yake ni ipi?

Unona Mwanakijiji alivyokuwa upset na kifo changu. Mwenzio nilikaripiwa vikali sana Jumamosi (Lol). Sasa itokee kweli Balali hajafa, unadhani ndugu zake na yeye mwenyewe atajisikiaje na huo uzushi? Au itokee kuwa ni kweli kafa, halafu baadhi ya watu wansema tena kwa uhakika kabisa kuwa hajafa, unadhani ndugu zake watajisikiaje?

Ngabu,

labda niweke wazi kuwa mimi hapa nimesema kuwa siamini kuwa Ballali amekufa kwa significance level ya 95%. Sijasema kwa hakika kuwa hajafa na bado sijaona aliyesema kwa hakika kuwa Ballali hajafa (I might be wrong).

So far, mimi na baadhi ya watu hapa tunakataa habari za kifo cha Ballali kwa vile vigezo vyote vya kuthibitisha kifo - hospitali aliyofia au kuthibitishwa kifo, siku ya kifo, record za kifo kwenye office ya CME - havithibitishi hili. Kubisha habari za kifo ni tofauti na kusema kwa hakika kuwa Ballali yuko hai. Najua wewe unaelewa hili ila nimeamua kutoa maelezo kwa niaba ya wasomaji tu.
 
Nadhani ukiangalia sana...siwalaumu wanaoona kuwa Ballali hajafa au wenye kushuku katika sakata zima. Kama nilivyosema nilikuwa naandika makala ndefu ya kuchambua jambo hili na kwanini kuwalaumu wanaoshuku na kuhoji ni kufanya makosa kwani wamepewa sababu. Tetesi za kutokufa au mchezo zisingetokea endapo kungekuwa na kitu kimoja tu nacho ni uwazi na ukweli. Kukosekana kwa hilo kumefanya watu wapike maneno mengi na ndio maana jitihada za kuwashawishi watu wakubali tu kuwa kafa kwa kuangalia picha sidhani kama zitafanikiwa. Ndio maana aidha ni bora kuendelea na ukimya kuliko kujaribu kuufafanua.

MKJJ don't go too low on this, i 'll never buy the cheap news that Daudi faked death, this is another world and this happened in the first world where everything is open and can be investigated and be discovered easily. Mkandara ameonyesha very clear how we can investigate if or not this death occurred. If we believe Daudi and the family faked this death then our thinking is different! America is not a banana country, and if you believe this guy was a public figure, then how easily you believe a public figure like Daudi can fake death?

Read here MFWK anavyosema:
"Hapa naona itabidi kila mtu afanya wito mwenyewe.
Familia imetangaza kuwa Ballali amekufa na serikali ikafuatia.
Ibada ya mazishi na mazishi vimefanyika na watu wakahudhuria".

MMMMMM.
Believe me this man is dead, a painful death; MFWK is used to this; I am waiting for you another another day when you will be seeking apology for this spin!!
 
MWFK
please be straight forward! what does this mean?
"labda niweke wazi kuwa mimi hapa nimesema kuwa siamini kuwa Ballali amekufa kwa significance level ya 95%. Sijasema kwa hakika kuwa hajafa na bado sijaona aliyesema kwa hakika kuwa Ballali hajafa (I might be wrong)."
 
Okay.. lemi get some facts from you!..

Well this is the first world where everything is open....

1. Do you know when Ballali died?
2. Do you know where he died (home or hospital)?
3. Do you know why there are no records of his death?

Read here MFWK anavyosema:
"Hapa naona itabidi kila mtu afanya wito mwenyewe.
Familia imetangaza kuwa Ballali amekufa na serikali ikafuatia.
Ibada ya mazishi na mazishi vimefanyika na watu wakahudhuria".

MMMMMM.
Believe me this man is dead, a painful death; MFWK is used to this; I am waiting for you another another day when you will be seeking apology for this spin!!

Mhh..

Mimi nimechunguza na sikupata uthibitisho wowote wa kujitegemea wa kifo cha Ballali. Call this a spin or anything but wewe ndio una burden ya kuthibitisha hiki kifo. Inaonekana unaona kuwa investigation yako yaweza kuwa bora kuliko ile iliyofanyika. Mbona usilete uthibitsho wa dunia ya kwanza hapa? jina la hospital, tarehe ya kifo, aliyethibitisha kifo, record za kifo, nk?
 
Mwafrika wa Kike,
Naungana kabisa na wewe katika kudiriki kukataa kifo cha Balalli, pamoja na kwamba kwa kufanya hivi nitakuwa naumiza na kuongeza majonzi kwa familia husika.
1. Kwa wadhifa aliokuwa nao Balalli, nashindwa kuamini kwa kweli amefariki kutokana na jinsi mambo yalivyopelekwa. Hivi kweli Balalli akasirike kiasi hicho hata asitake watu kuhudhuria mazishi yake? Asitake hata mama yake kushuhudia mwili wake naye apate closure, kuwa mwanae amefariki. Mh!!!!!
2. Hivi ni kweli familia ya Balalli na ya mkewe ni ndogo hivyo kiasi kwamba msiba huo umekuwa ni kama mtu asiye na watu. Pamoja na kuendelea na privacy issues bado haiingiii kwa namna ilivyopelekwa. Ni ugonjwa gani wa siri hivyo? Ni mtu gani angependa kuuguza kwa muda mrefu kiasi hicho bila hata kutaka sympathy ya waliomzunguka? Kweli Balali alikuwa mgonjwa kutokutaka kabisa kuonwa na ndugu, jamaa au marafiki?
3. Kwa nafasi aliyokuwa nayo Balalli hata kama angekuwa halipiwi na serikali nina hakika kwa kiasi kikubwa kuna taarifa zake ambazo zingepatikana. Kwa namna taarifa zilivyokuwa zinatolewa naona kuna utata.
4. Mwanzoni nilitaka kuamini ni mapungufu yetu ya kiutendaji kwa kutokufuatilia mambo, hasa ubalozi nikifikiria wana wajibu wa kujali rai wao wakiwa hai au wafu, lakini kila nikifikiri naondoa fikira hiyo si sahihi. Taarifa ya kifo USA be it in Boston or DC ichukue
siku 3 au zaidi. Bado taarifa hizo haijulikani ni ipi ni sahihi.
5. Ni kwanini watu wazuiwe kushiriki msiba wake huko Boko kama tu zilivyo mila na desturi zetu? Yaani familia ya Balali imebadilika kiasi hicho na kuwa na utamaduni wa kigeni kabisa na kwa ghafla? Mh!!! Hivi ndivyo kweli alivyotaka mama yake Balali, ndugu zake au yeye mwenyewe? Mbona waliomchafulia jina kama kweli limechafuliwa, wala hawana uchungu naye, kwanini amuumize mama yake mzazi kama ni kweli amefariki?
6. Kulikuwa na tetesi siku za nyuma kuwa yuko Malta, hivi hili liliishia wapi?

Sijui nikikutana naye itakuwaje.
 
MWFK
please be straight forward! what does this mean?
"labda niweke wazi kuwa mimi hapa nimesema kuwa siamini kuwa Ballali amekufa kwa significance level ya 95%. Sijasema kwa hakika kuwa hajafa na bado sijaona aliyesema kwa hakika kuwa Ballali hajafa (I might be wrong)."

Hii inamaanisha kuwa, nimeacha asilimia tano ya kumwamini Jasusi na FMES kwenye hili. Siwezi nikapinga hii habari kwa asilimia mia kwa vile bado nina imani na hawa wana JF. Otherwise, uchunguzi wangu unaonyesha otherwise kuhusu kifo cha Ballali.

Kumbuka kuwa niliamini na kutetea kifo cha Ballali hadi nilipofanya uchunguzi na kuambiwa tofauti. Kumbuka kuwa ndugu zake Ballali wamesuggest hapa kuwa Ballali alitumia jina tofauti akiwa hospitali - hii inakuambia nini kuhusu yale ambayo nimechunguza na kupata?
 
Ngabu,

labda niweke wazi kuwa mimi hapa nimesema kuwa siamini kuwa Ballali amekufa kwa significance level ya 95%. Sijasema kwa hakika kuwa hajafa na bado sijaona aliyesema kwa hakika kuwa Ballali hajafa (I might be wrong).

So far, mimi na baadhi ya watu hapa tunakataa habari za kifo cha Ballali kwa vile vigezo vyote vya kuthibitisha kifo - hospitali aliyofia au kuthibitishwa kifo, siku ya kifo, record za kifo kwenye office ya CME - havithibitishi hili. Kubisha habari za kifo ni tofauti na kusema kwa hakika kuwa Ballali yuko hai. Najua wewe unaelewa hili ila nimeamua kutoa maelezo kwa niaba ya wasomaji tu.

Sister girl, you are my favorite person. My frustration on this whole thing is not aimed at you. Afterall, how can I do that to my future sister in law? That's a no no!! My beef is with whoever led you and others to think that he's dead while some of the records that establish a persons death contradict with what we've been told. So my question is still: Which is which? Najua uko makini sana na huwezi tu kukurupuka bila sababu. Na sababu hapa umeilezea vizuri kabisa na hata mimi mwenyewe najiuliza maswali hayo hayo unayojiuliza wewe (great minds think alike....kwikwikwiii). Kwa hiyo bibie, frustration zangu zinaelekezwa kwa chanzo au vyanzo vya habari hii. Na kama Balali ndiye chanzo, then yeye ndiye wa kulaumiwa and you better believe I'll jump on him like never before.
 
ur planning to do this when he is alive or when you find out he is really dead.. naona unataka kuanzisha kasheshe nyingine ya kupanga kumrukia marehemu anayedaiwa kuwa hai. Yangu macho.
 
You are coping out, and you are making it worse.

Because you are trying to imply that MFWK is just a gullible sponge who absorbs whatever is thrown at her. I thought she gave absolutely independent reasons as to why she is a non-believer.

You're in hole, stop digging!
 
ur planning to do this when he is alive or when you find out he is really dead.. naona unataka kuanzisha kasheshe nyingine ya kupanga kumrukia marehemu anayedaiwa kuwa hai. Yangu macho.

No..no..no!! I meant to say if it turns out that he's alive and he faked his own death. Nilisahau kuweka hilo bayana.
 
Back
Top Bottom