Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Bado nasimamia msimamo wangu wa kuzikataa hizi habari za kifo cha Ballali kwa asilimia 95. Najua kuwa sio business yangu kukubali au kukataa vifo vya watu. Hata hivyo, ninajua pia kuwa Ballali alikuwa gavana wa BoT wakati wa wizi mkubwa kabisa wa mabilioni ya watanzania ukitokea.
Kama yeye si mtuhumiwa, hilo halijathibitishwa kwa sasa kama ambavyo haijathibitishwa kuwa alikuwa mtuhumiwa au shahidi. Ninachojua mimi ni kwamba, kama nimeweka pesa zangu kwenye briefcase na nikamkabidhi kaka yangu kuichunga, nikirudi na kukuta kiwango kikubwa cha pesa kimepotea na kaka yangu bado anaishikiria briefcase yangu, yeye atakuwa ni mshukiwa wa kwanza kabisa kabla ya mengine yote kutokea.
Bado story ya Ballali juu ya kile kilichotokea BoT wakati akiwa gavana inafuatiliwa kujua ukweli wake. Katika hili, kwa vile yeye alikubali pesa zikatoka na hakusema au kufanya chochote, nitachukulia chochote anachosema kwa tahadhali kubwa mpaka ithibitishwe otherwise.
Huu ni msimamo na mtizamo wangu binafsi. Simlazimishi yeyote yule kukubaliana nami katika hili. Nilikubali na kutetea kifo cha Ballali kwa nguvu sana kwa zaidi wiki moja na sikuitwa mpumbavu. Ninategemea kuwa kama uchunguzi wangu ukinipelekea mimi kuamini tofauti basi nitaendelea kutoitwa mpumbavu as longer as silazimishi yeyote yule kukubaliana nami.
Asante!