tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Naingia kwenye hoja moja kwa moja pasipo kuwachosha wala kuwapotezea muda. Naomba niwapitishe kwenye kisa kichungu lakini chenye nguvu kinachotokea Zambia leo, ambacho kila dikteta wa Kiafrika anapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa sana.
Mnamo mwaka 2017, Edgar Lungu alikuwa Rais wa Zambia. Wakati huo, mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, alikuwa kiongozi wa upinzani tu. Lungu hakupenda kupingwa, hivyo alifanya kile ambacho viongozi wengi wa Afrika hufanya; alitumia mamlaka ya nchi kuwaadhibu wapinzani wake. Aliagiza Hakainde akamatwe na kutupwa gerezani.
Lakini mnamo 2021, mambo yalibadilika. Wananchi wa Zambia walipiga kura, na meza ikapinduka. Hakainde Hichilema akachaguliwa kuwa Rais. Edgar Lungu sasa akawa mpinzani. Akawekwa kando na akawa hana udhibiti tena.
Ilipofika mwaka 2025 Edgar Lungu akaanza kuumwa. Hali yake ilihitaji matibabu ya haraka nje ya nchi. Familia yake iliomba ruhusa kutoka kwa Serikali ya Hakainde Hichelema ili asafirishwe hadi Afrika Kusini kwa matibabu.
Lakini serikali ya Hichelema ikachelewsha ruhusa ya Lungu kwenda kutibiwa. Ruhusa haikuja haraka. Mchakato ulikuwa wa polepole, na kila walipozidi kuchelewa kulifanya hali ya afya ya Lungu kuzidi kudorora.
Mpaka walipomruhusu Lungu kusafiri, walikuwa wamechelewa. Alitua Afrika Kusini, lakini afya yake ilikuwa tayari imezorota kupita kiasi. Ndani ya siku chache, Edgar Lungu alifariki.
Sasa taifa linaomboleza, lakini uchungu katika moyo wa familia yake ni mkubwa zaidi. Wanaamini kwamba ikiwa serikali ingemruhusu kuondoka mapema, huenda angali hai hadi leo.
Katika uamuzi wa ujasiri na wa kimhemko, familia imekataa mazishi ya serikali. Hawataki serikali ambayo wanalaumu kwa mateso yake kumlaza. Badala yake wameamua kumzika Lungu huko Afrika Kusini.
Ndiyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, mkuu wa zamani wa nchi atazikwa katika nchi ya kigeni. Hii sio tu kuhusu Zambia. Huu ni ujumbe kwa viongozi wote wa Afrika wanaotumia madaraka kunyamazisha upinzani.
Nguvu ni ya muda. Watu unaowaonea leo wanaweza kukuongoza kesho. Na jiulize siku hiyo ikifika watakuchukuliaje? Hebu kisa hiki cha Edgar Lungu kiwe onyo. Usitumie madaraka kukandamiza watu. Kwa sababu bila kujali jinsi unavyopanda juu, siku moja meza itapinduka.
Pumzika kwa Amani Edgar Lungu.