Kifo cha Edgar Lungu na uhaini wa Tundu Lissu ni funzo kwa Rais Samia

Naingia kwenye hoja moja kwa moja pasipo kuwachosha wala kuwapotezea muda. Naomba niwapitishe kwenye kisa kichungu lakini chenye nguvu kinachotokea Zambia leo, ambacho kila dikteta wa Kiafrika anapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa sana.

Mnamo mwaka 2017, Edgar Lungu alikuwa Rais wa Zambia. Wakati huo, mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, alikuwa kiongozi wa upinzani tu. Lungu hakupenda kupingwa, hivyo alifanya kile ambacho viongozi wengi wa Afrika hufanya; alitumia mamlaka ya nchi kuwaadhibu wapinzani wake. Aliagiza Hakainde akamatwe na kutupwa gerezani.

Lakini mnamo 2021, mambo yalibadilika. Wananchi wa Zambia walipiga kura, na meza ikapinduka. Hakainde Hichilema akachaguliwa kuwa Rais. Edgar Lungu sasa akawa upinzani. Akawekwa kando na akawa hana udhibiti tena.

Ilipofika mwaka 2025 Edgar Lungu akaanza kuumwa. Hali yake ilihitaji matibabu ya haraka nje ya nchi. Familia yake iliomba ruhusa kutoka kwa Serikali ya Hakainde Hichelema ili asafirishwe hadi Afrika Kusini kwa matibabu.

Lakini serikali ya Hichelema ikachelewsha ruhusa ya Lungu kwenda kutibiwa. Ruhusa haikuja haraka. Mchakato ulikuwa wa polepole, na kila walipozidi kuchelewa kulifanya hali ya afya ya Lungu kuzidi kudorora.

Mpaka walipomruhusu Lungu kusafiri, walikuwa wamechelewa. Alitua Afrika Kusini, lakini afya yake ilikuwa tayari imezorota kupita kiasi. Ndani ya siku chache, Edgar Lungu alifariki.

Sasa taifa linaomboleza, lakini uchungu katika moyo wa familia yake ni mkubwa zaidi. Wanaamini kwamba ikiwa serikali ingemruhusu kuondoka mapema, huenda angali hai hadi leo.

Katika uamuzi wa ujasiri na wa kimhemko, familia imekataa mazishi ya serikali. Hawataki serikali ambayo wanalaumu kwa mateso yake kumlaza. Badala yake wameamua kumzika Lungu huko Afrika Kusini.

Ndiyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, mkuu wa zamani wa nchi atazikwa katika nchi ya kigeni. Hii sio tu kuhusu Zambia. Huu ni ujumbe kwa viongozi wote wa Afrika wanaotumia madaraka kunyamazisha upinzani.

Nguvu ni ya muda. Watu unaowaonea leo wanaweza kukuongoza kesho. Na jiulize siku hiyo ikifika watakuchukuliaje? Hebu kisa hiki cha Edgar Lungu kiwe onyo. Usitumie madaraka kukandamiza watu. Kwa sababu bila kujali jinsi unavyopanda juu, siku moja meza itapinduka.

Pumzika kwa Amani Edgar Lungu.
Samia gang Samiaagain2025 Lucas Mwashambwa etc. Ni kweli hakika Dkt Samia kupitia wasaidizi wake wamefanya vitu vya ajabu mno jamani. Hivi unafungia kanisa, unakama watu na kuwauwa wazi wazi. Hahaha sisi yetu macho jamani naamini Mungu aliye hai atajibu
 
Nguvu ni ya muda. Watu unaowaonea leo wanaweza kukuongoza kesho. Na jiulize siku hiyo ikifika watakuchukuliaje? Hebu kisa hiki cha Edgar Lungu kiwe onyo. Usitumie madaraka kukandamiza watu. Kwa sababu bila kujali jinsi unavyopanda juu, siku moja meza itapinduka.
Kwa kuhofia muda wa nguvu kuisha ndio maana watu huamua kubadili katiba ili wafe wakiwa na nguvu za kuwatia watu nguvuni.
 
Mimi nilidhan ni Rais wa Generation za kina Mugabe, Nyerere na kina Des Santos. Kumbe ni wa juzi tu?
Sasa kaondoka na madaraka?
Mnamo mwaka 2017, Edgar Lungu alikuwa Rais wa Zambia. Wakati huo, mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, alikuwa kiongozi wa upinzani tu. Lungu hakupenda kupingwa, hivyo alifanya kile ambacho viongozi wengi wa Afrika hufanya; alitumia mamlaka ya nchi kuwaadhibu wapinzani wake. Aliagiza Hakainde akamatwe na kutupwa gerezani.
 
Naingia kwenye hoja moja kwa moja pasipo kuwachosha wala kuwapotezea muda. Naomba niwapitishe kwenye kisa kichungu lakini chenye nguvu kinachotokea Zambia leo, ambacho kila dikteta wa Kiafrika anapaswa kuzingatia kwa umakini mkubwa sana.

Mnamo mwaka 2017, Edgar Lungu alikuwa Rais wa Zambia. Wakati huo, mpinzani wake mkuu, Hakainde Hichilema, alikuwa kiongozi wa upinzani tu. Lungu hakupenda kupingwa, hivyo alifanya kile ambacho viongozi wengi wa Afrika hufanya; alitumia mamlaka ya nchi kuwaadhibu wapinzani wake. Aliagiza Hakainde akamatwe na kutupwa gerezani.

Lakini mnamo 2021, mambo yalibadilika. Wananchi wa Zambia walipiga kura, na meza ikapinduka. Hakainde Hichilema akachaguliwa kuwa Rais. Edgar Lungu sasa akawa upinzani. Akawekwa kando na akawa hana udhibiti tena.

Ilipofika mwaka 2025 Edgar Lungu akaanza kuumwa. Hali yake ilihitaji matibabu ya haraka nje ya nchi. Familia yake iliomba ruhusa kutoka kwa Serikali ya Hakainde Hichelema ili asafirishwe hadi Afrika Kusini kwa matibabu.

Lakini serikali ya Hichelema ikachelewsha ruhusa ya Lungu kwenda kutibiwa. Ruhusa haikuja haraka. Mchakato ulikuwa wa polepole, na kila walipozidi kuchelewa kulifanya hali ya afya ya Lungu kuzidi kudorora.

Mpaka walipomruhusu Lungu kusafiri, walikuwa wamechelewa. Alitua Afrika Kusini, lakini afya yake ilikuwa tayari imezorota kupita kiasi. Ndani ya siku chache, Edgar Lungu alifariki.

Sasa taifa linaomboleza, lakini uchungu katika moyo wa familia yake ni mkubwa zaidi. Wanaamini kwamba ikiwa serikali ingemruhusu kuondoka mapema, huenda angali hai hadi leo.

Katika uamuzi wa ujasiri na wa kimhemko, familia imekataa mazishi ya serikali. Hawataki serikali ambayo wanalaumu kwa mateso yake kumlaza. Badala yake wameamua kumzika Lungu huko Afrika Kusini.

Ndiyo, kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika, mkuu wa zamani wa nchi atazikwa katika nchi ya kigeni. Hii sio tu kuhusu Zambia. Huu ni ujumbe kwa viongozi wote wa Afrika wanaotumia madaraka kunyamazisha upinzani.

Nguvu ni ya muda. Watu unaowaonea leo wanaweza kukuongoza kesho. Na jiulize siku hiyo ikifika watakuchukuliaje? Hebu kisa hiki cha Edgar Lungu kiwe onyo. Usitumie madaraka kukandamiza watu. Kwa sababu bila kujali jinsi unavyopanda juu, siku moja meza itapinduka.

Pumzika kwa Amani Edgar Lungu.
ibirisi wa ccm wao mateso kwa Lisu na chadema ni Dili na Fursa wamechukua bilon 15 huko Hazina kienyeji kwa kazi maalum ya kuidhoofisha kuihujumu chadema wizi wa pesa za walipa kodi, mateso ya chadema ni biashara kubwa ya Amos makala Bashungwa IGP Polisiccm na chawaccm na ibirisi wengine wa ccm
 
We bwege Tanzania na Zambia kwenye suala la siasa ni vitu viwili tofauti. LinganishaTanzania ya CCM na China ya CPC. Mtaokoteza kila takataka ila sisi tuna siasa yetu ya kipekee Afrika.
Wewe umesahau watu walikuwa hawavai nguo za CCM kukatisha Kariakoo
Lolote linaweza kutokea acha kukariri maisha
 
Uzuri ni kuwa huyu hafi ataishi milele yote
FB_IMG_1750520309337.jpg
 
Hiyo nchi ina historia ya aina yake, nakumbuka Chiluba alishamuweka kifungoni Kaunda.
Historia haidanganyi na Mungu hadhihakiwi. Ipo siku Tundu Lissu atamfungulia Samia mashtaka bandia ya uhaini au hata kumnyima ruhusa ya matibabu afe kwa maradhi.
 
Hapana.

Hili halikuwa sahihi kufanywa na serikali ya Hichilema Haikande.

Ndiyo; huyo Lungu alistahili kuonyeshwa matokeo ya ubaya wake; na nadhani njia nzuri ya kufanya hivyo ni kumfanyia kinyume na alivyokuwa akifanya yeye. Hii ingekuwa ni fundisho zuri zaidi na adhabu stahiki kwake.

Ndiyo, najuwa ubinaadam haufanyi hivyo. Hapa duniani hakuna malaika, lakini ni muhimu kufanya jitihada za kuwa tofauti na hao wengine wanaowatesa wenzao bila ya sababu za msingi; kama hawa wanaowateka na kuwaua waTanzania sasa hivi.
Ubaya ubwela. No reforms, no election. Dawa ya moto ni moto. Malipo ni hapa hapa duniani.
 
We bwege Tanzania na Zambia kwenye suala la siasa ni vitu viwili tofauti. LinganishaTanzania ya CCM na China ya CPC. Mtaokoteza kila takataka ila sisi tuna siasa yetu ya kipekee Afrika.
Wewe unashauri nini kifanyike ili kuepukana na hizi siasa za kishetani za Afrika mkuu?
 
Umeandika ukweli mtupu mkuu Afica sijui tuna matatizo Gani aisee yaani mtu akiwa mpinzani anaonekana ni hatar Kwa usalama wa nchi ni ujinga ujinga tu wa viongozi .
Viongozi wengi wa Afrika ni majizi wakubwa wa rasilimali za taifa. Wanataka wale bila kubugudhiwa na wapinzani.
 
Back
Top Bottom