Kifo cha ghafla cha Mfugale sawa na Prof. Chachage: Kuna viashiria vyote vya kupewa sumu. Serikali ichunguze

Kuna mahali mmoja alisema according to him ... ngoja nimfuate na nitarudi naye hapa kwenye kikao ...... kwa hali hiyo kulikuwa na tuhuma ambazo late alitakiwa kujibu.....

Anyway mmesema afya yake alikuwa imedorora ukiongeza na hayo ya kikao lazima moyo ushindwe kuhimili.

Ameondoka ni nini kitafuata, muda utaongea.
 
Yaani unasema kabisa kuwa ni wazi amepewa sumu halafu unahitisha kwa kuomba uchunguzi?! We jamaa uko sawa upstairs!
Hauelewi kuwa kazi ya uchunguzi ni kuweka mambo kuwa wazi, sasa kama wewe unasema “ni wazi” tayari, unataka kuchunguza nini!
 
Ni kupoteza nguvu na kuongeza uchungu. Huwezi ishinda serikali kwa namna yoyote ile
 
SAWA.
Mengi uliyoandika ni sahihi. Lakini ushuhuda wako hauna msingi wowote katika kuondoa uwezekano wa COVID-19 kuhusika.

Na hayo uliyoeleza, siyo kwamba ndio sehemu kamilifu ya matatizo yanayoambatana na COVID-19; kwa sababu bado kuna mengi yasiyofahamika juu ya ugonjwa wenyewe; na ukichukulia kwamba siyo wagonjwa wote ni lazima waonyeshe dalili hizo na kwa nyakati hizo ulizotaja wewe.

Ulijua kwamba Mfugale kabla hajafariki hakuwa na baadhi ya dalili hizo, hata kama alikuwa halalamiki juu yake? Siyo watu wote huonyesha dalili hizo ulizotaja kwa ukubwa wa kuwatia hofu na kuanza kutafuta msaada, hasa ukichukulia tabia za watu wengi kujihisi kuwa miili yao ni imara. Wanasubiri hadi hali iwe ngumu zaidi kabla ya kutafuta msaada.

Kinachozungumziwa hapa ni kutojua ni nini hasa kinaweza kuwa kimesababisha au kimechangia kifo cha Mfugale. Ni kazi ndogo sana sasa kupima na kujua kama marehemu alikuwa na COVID-19 au hapana.

Hii ni hatua moja ya kujaribu kutambua sababu za kifo cha ghafla.
 
Ni kupoteza nguvu na kuongeza uchungu. Huwezi ishinda serikali kwa namna yoyote ile
"Huwezi ishinda serikali"(?)
Kwa vile serikali hizi ni za kidhalimu, na wananchi wake mmejiweka tayari kukubali kwamba hamuwezi kuishinda serikali hata kama serikali hiyo inawafanyia udhalimu! Inawanyima haki zenu.

Hii ni taabu sana ya kuwa na raia wenye mawazo kama haya.
 
Si lazima kupeleka mwili nje ya nchi, uchunguzi unafanyika hapa hapa, ikilazimu kwa msaada wa wataalam toka nje; au hata sampuli kupelekwa nje.

Kama wao kama ndugu hawajaridhishwa na maelezo ya sababu za kifo cha ndugu yao, wanayo haki ya wao kutafuta ukweli.
 
Mwendazake je?
 
Moderator uzushi kama huu mnaacha wa nini?

Au mnaona mama ni mpole ndio maana mnaacha habari kama hizi ambazo zinaweza kuligawa taifa?

Hebu futeni huu ujinga
 
Halafu haijawahi kuelezwa wapi uchunguzi ulifikia wala mtuhumiwa ni nano na kwanini hajakamatwa. Na huyo ndio makam mwenyekeiti, wengine je
Ni uongo,mangula hakupewa sumu,wanasema yule mbilikimo eti alimpa sumu,,sasa mangula akaamua kusimamia harusi ya mbilikimo ili kuwahakikushia kua ile habari ni fake.
Pili makonda,hakumpiga mitama warioba,,ilikuwa ni fake news,,warioba mwenyewe alikiri kuwa makonda alikuwa akijaribu kumlinda warioba..
 
Kama imefanyika ataitoa huyo daktari au jopo la madaktari waliofanya......kama kuna sampuli zimechukuliwa kwenda kwingineko itabidi wasubiri hayo majibu ili kukamilisha ripoti yao, sawasawa?

Hayo maelezo yako sasa yaunganishe na hoja yangu ile ya msingi, refa wao na uwanja wao… utatokaje?
 
Kwa sasa,na korona hii,mtu akisema ansjisikia vibaya,hapo hapo wahisha hospital chap chap,,ukichelewa tu,,kwa heri
 
Mpwa unazungumzia kifo cha Mfugale au unajizungumzia wewe?? Umeanza vyema sana na hii iko wazi na kuna Uzi mwingine kama huu hapa hapa JF ila sasa kuanza kujisifia wewe mwenyewe, hapa umechemka!
 
Hayo maelezo yako sasa yaunganishe na hoja yangu ile ya msingi, refa wao na uwanja wao… utatokaje?
Hata wataalamu wanaweza kwenda chaka kubainisha sababu hasa ya kifo, wakati mwingine kifo kinabaki kuwa fumbo....
 
Niliwahi kusikia kwamba Serikali haifanyii kazi taarifa za mtandao...
 
Kifo kipo tu kila mtu atakufa, mbona wakifa watu wa kawaida (pangu pakavu) huwezi kusikia habari za namna hiyo?

Au wenye pesa na mamlaka wao hawatakiwi kufa?
 
Hata wataalamu wanaweza kwenda chaka kubainisha sababu hasa ya kifo, wakati mwingine kifo kinabaki kuwa fumbo....

Ni fumbo kwa kuwa tu kinakuja bila taarifa, ila baada ya hapo ni lazima sababu ijulikane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…