Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Mustafa Kamal ataturk ni raisi wa kwanza wa Uturuki, atakumbukwa kuungana na dola za Uengereza na Ufaransa kuivunja dola ya kiislamu ya Khilafah tarehe 3 Machi 1924 , na kuigawanya dola hiyo vijinchi vidogo vidogo na kuweka vibaraka wao katika uongozi ili kuongoza kwa maslahi yao. Mmoja wa vibaraka wao akawa ni huyu Mustafa kamal aliyenzisha taifa jipya na kuliita Turkey.
Samahani kwa bahati mbaya hii unayoleta si historia, ni kama Hekaya za Abunuwasi.
Kama Mustafa Kemal Ataturk ni maarufu kwa jambo fulani ni kuzuia ugawaji wa mabaki ya Milki ya Khalifa na kuunda Uturuki wa kisasa.
1. Yale unayoita "dola ya kiislamu ya Khilafah" ilikuwa Milki ya Osmani (Ottoman Empire) iliyotawaliwa na Waturuki (Mkuu alikuwa sultani mwenye cheo cha Khalifa) na kutawala pia nchi za Waarabu (Syria, Iraki, Lebanoni, Palestina, Yemen, na Hejaz yaani sehemu ya Uarabuni). Ndani ya eneo la Uturuki ya leo takriban robo ya wananchi hawakuwa Waturuki bali Wakristo Wagiriki, Waarmenia na Waassiria.
2. Milki ya Osmani iliingia katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia upande wa Ujerumani ukashindwa pamoja na Ujerumani ikipigana na Urusi, Uingereza na wananchi katika sehemu zilizotafuta uhuru wao, kama Waarabu na Waarmenia.
3. Wakati wa Vita Kuu Mustafa Kemal alikuwa jenerali ya jeshi la Sultani=Khalifa alikuwa maarufu akitetea Mlangobahari ya Dardaneli dhidi ya uvamizi wa Uingereza hivyo kuzuia kukamatwa kwa mji mkuu na Uingereza.
4. Baada ya kushindwa vita Sultani=Khalifa alikubali Mkataba wa Sevres ya 1920. Kanuni za mkataba huu zililenga kugawa milki yote: Hejaz (pamoja na Makka) ilipewa uhuru, Irak na Palestina iliwekwa chini ya Shirikisho la Mataifa (league of Nations) na kukabidhiwa kwa Uingereza, Syria na Lebanoni pia chini ya Shirikisho la Mataifa na kukabidhiwa kwa Ufaransa. "Ukanda wa Milangobahari" (zone of straits") ilitengwa na kuwekwa chini usimamizi wa kimataifa moja kwa moja. Maeneo ya mashariki-kaskazini zilizokaliwa na Waarmenia yaliunganishwa na Jamhuri ya Armenia (awali ya Kirusi). Maeneo ya Wakurdi yalipangwa kuwa na mamlaka ya ndani na nafasi ya kupiga kura kuhusu uhuru. Maeneo ya magharib kabisa yaliyokaliwa na Wagiriki wengi walipewa pia mamlaka ya kujitawala na nafasi ya kupiga kura baadaye kuhusu maungano na Ugiriki. Tangu 1919 wanajeshi kutoka Ugiriki walishika tayari mji wa Smyrna (Izmir) na mazingira yake, Wafaransa na Waingereza waliingia Istanbul.
Maeneo kadhaa katika rasi ya Anatolia yalipangwa kubaki kama “Milki ya Osmani”
5. Baada ya uvamizi wa Istanbul na Uingereza na Ufaransa na kutangazwa kwa mkataba wa Sevres Mustafa Kemal aliungana na Waturuku wengine akaita “Mkutano Mkuu wa Waturuki” akatangaza serikali ya Khalifa=Sultani kuwa wasaliti akajenga jeshi jipya na kupigana na Wagiriki na Waarmenia.
6. Katika vita hii inayojulikana kama “Vita ya Uhuru wa Uturiki” Mustafa Kemal alifaulu kufukuza Wagiriki. Waingereza , Wafaransa na Waitalia walichoka vita wakaondoka. Urusi baada ya mapinduzi yake ya 1917 haikushiriki tena katika vita hii baada Vita Kuu. 1922 Mkataba wa Lausanne ulikubali Uturuki mpya katika mipaka yake jinsi ilivyo leo.
7. Bunge jipya likamchagua Mustafa Kemal kuwa kiongozi. Bunge likaamua kutenganisha vyeo vya Sultani na Khalifa. Usultani ulifutwa na Sultani Mehmet V. alifukuzwa nchini akahamia Italia. Shemeji yake Abdulhamid alichaguliwa na bunge kuwa khalifa mpya na mkuu wa dola, lakini bila mamlaka.
8. Baada ya miezi michache Mustafa Kemal alipata kura nyingi katika bunge kubadilisha katiba tena na kufuta pia ukhalifa. Mustafa Kemal akawa rais wa Uturuki. Abdulhamid alihamia Ufaransa alipoishi hadi mwaka 1944 akiwa mchoraji wa taswira na mtaalamu wa vipepeo. Baada ya kifo chake alizikwa Makka kwa amri wa Mfalme Saud.
9. Mustafa Kemal aliheshimiwa kama mwanzilishaji wa Uturuki wa Kisasa akapewa jina la „Baba wa Waturuki“ = Atatürk“.
10 Mustafa Kemal alichukua hatua nyingi kubadilisha Uturuki kuwa nchi ya kisasa. Aliona Uislamu kuwa sababu kubwa ya udhaifu wa taifa lake hivyo hakukataza Uislamu lakini alitenganisha serikali na dini, lakini kwa kuuunda taasisi za kusimamia misikiti zote.Alilenga kuzuia athira ya maimamu na mashehe katika shughuli za serikali. Aliwapa wanawake haki ya kupiga kura, alikataza nguo za kidini na hijabu ya wanawake.
11. Hadithi kuhusu kuzikwa kwake ni kitoto, haina msingi wowote. Mwili wake uliwekwa katika jeneza alipokufa Istanbul tarehe 10.11.1935 na kubebwa kwa manowari hadi Izmit, kutoka huko kwa treni maalumu hadi Ankara. Pale jeshi lilibeba jeneza hadi jengo la Bunge na maelfu walipita mbele yake. Mwili uliwekwa katika jeneza kubwa ya jiwe (sarcophagus) iliyokaa katika makumbusho kuu. Kwa miaka iliyofuata jengo la pekee lilijengwa kwa kutunza masalio yake na hapa yapo tangu 1953. Soma kwa undani zaidi hapa https://en.wikipedia.org/wiki/Death_and_state_funeral_of_Mustafa_Kemal_Atatürk#Transfer_to_the_capital_city
Wananchi wa Ankara jinsi alivyoaga jeneza ya Mustafa Kemal 1935